Mbona Waziri Dorothy Gwajima yupo kimya sakata la Pauline Gekul?

Nijuavyo mimi ni Rais tu ndiye hawezi kushitakiwa (Sasa hivi ninasikia wameongezeka Spika, CJ, n.k.)

Maana yake wengineo wote (akiwemo NW) wanashitakika and so wanaweza kuchunguzwa vizuri kabisa hata wakiwa na nyadhifa zao.

Hiyo aya ya mwisho ninafikiri ni mahakama tu ndiyo inapaswa kuthibitisha. Otherwise, haumtendei haki. Tuhuma zinapaswa kuthibitishwa kabla ya kuanza kumshushia hizi nyuzi.

Siku moja nawe utatuhumiwa (bila kujali una hatia) halafu jamii nzima ikuhukumu, ndipo utajua umuhimu wa presumption of innocence mpaka mahakama iamue vinginevyo. That's karma.
 
Waziri hupaswi hata kutuhumiwa, ni vile tu viongozi wa Kiafrika hukaza mafuvu sababu ya kiburi na uchu wa madaraka wa kutokujiwajibisha

Mahakama ikimsafisha ataweza kupewa dhamana ya uongozi tena...
Usafishaji wa mahakama unakuja baada ya presumption ya innocence yake. Nyuzi zenu humu zipo kimhemuko sana. JF imekuwa ya vilaza siku hizi.
 
Nadhani yuko kimya sababu suala lipo ktk mikono ya Police, asije akaharibu upelelezi.
 
Rahisi ❌️
Rais ✅️

Kama kuandika tu ni shida, comment yako haishangazi.
Yes, nimekosea nakubali. Lakini huo ndio ukweli na ndivyo katiba yetu ilivyo. Imempa madaraka makubwa raisi ya kufanya hivyo. Kuteua na kutengua anavyojisikia wale aliowateua bila hata kutoa sababu. Wengine utasikia watapangiwa majukumu mengine ila huyu sababu haikutajwa na huo mstari wa atapangiwa majukumu mengine haukuwepo.
Hivyo upende au usipende, ndivyo ilivyo.
 
Right to presumption of innocence until the court proves otherwise. Ninashangaa Samia ametumia kigezo gani kumtumbua! Sifa za kijinga na mob psychology zinatuharibu Watanzania.
Kiongozi hupaswi kutuhumiwa au ata kuhisiwa kuwa unafanya jambo la utovu wa kimaadili.Yeye Gekul kama alikuwa na ushahidi yule dogo anapanga kumuua angeripoti kwenye vyombo vya usalama.Unakuaje Naibu Waziri wa sheria alafu unakuwa namba moja kuvunja sheria!
Kama yule dogo angekufa mbele yake Gekul,ungekuja hapa na huu utetezi?

Sent from my V2111 using JamiiForums mobile app
 
Huyo Gekul hakubaliki hata hapa babati huwezi kuleta bifu na mamalishe yeye ndio alilianzisha na atalinywa zitaletwa Hadi picha hapa akiwa na Serengeti boys sa hv ni kuwalipua tu tumechoka sasa
 
Double standard.
Dkt. Gwajima D
Please.
Sidhani kama mfumo wa kiuongozi unamruhusu Waziri kutolea tamko tukio lililofanywa na Waziri mwenzake. Hivyo msitegemee tamko lolote lile kutoka kwake. Kuna kitu kinaitwa collective responsibility. Ndicho kitakachomzuia kuongea chochote kumhusu Waziri mwenzake.

Na isitoshe hilo suala lenyewe tayari lipo kwenye vyombo vya dola(polisi) kwa ajili ya uchunguzi. Hivyo hao ndiyo wenye mamlaka na jambo hilo kwa sasa.
 
Ninakubaliana na wewe. Na kwa kuwa viongozi wetu wote, kuanzia CCM hadi upinzani, wana tuhuma za kutosha sote kwa umoja wetu tupaze sauti waachie nafasi zao za madaraka... Tusimng'ang'anie Gekul pekee.
 
Anasoma upepo kwanza!!
 
Yaani unataka waziri mzima aje aropoke hapa jamba ambalo liko polisi tayari? Tuache ujuaji wa kipopoma!
Kwani taasisi na makundi mbalimbali yanayoongelea jambo hilo unadhani hawajui kuwa liko polisi? Aacheni utoto, ni sheria ipi inakataza kuongelea jambo kama hilo likiwa polisi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…