Labda kama wewe ni mnufaika na hizo copper kufika hapa mjini, yaani waweze kutoa makontena bandarini kuyasombelea kwala washindwe kutoa copper kwala kuileta bandarini!!? Hiyo treni itakayo kua inazoa hizo kontena bandarini, ikisha zishusha hapo kwala inarudi tupu!!?
Wewe unajua adha ya foleni ya kushusha copper!? Embu anza kuuliza madereva nini kinawapata mpaka anamaliza harakati za kushusha hiyo copper, pia umeshawahi kutumia morogoro road hicho kipande cha manzese, bigbrother mpaka kuvuka tbl ubungo!? Wapo wanao tumia barabara ya ubungo maziwa watakusimulia japo hua haina msongamano, pale tabata mwananchi mpaka karibu na TIOTI unapajua!!? Mnaweza ganda kwenye foleni lisaa lizima mnasubiri gari igeuze au imefunga njia akitarajia apate nafasi ya kuingia upande wa pili, ama wewe hua unatumia king'ora kupita huko unakuta barabara zimesha safishwa ndio maana hukuti adha hizo!!?