Mbossa: Bandari kavu ya Kwala ni mara tano zaidi ya ukubwa wa Bandari ya Dar es Salaam

Kama kule baharini kwenye mlango hakuna ufanisi na ni kudogo haijalishi hata kama bandari kavu ni kubwa kama wilaya ya Namtumbo.
 
Labda kama wewe ni mnufaika na hizo copper kufika hapa mjini, yaani waweze kutoa makontena bandarini kuyasombelea kwala washindwe kutoa copper kwala kuileta bandarini!!? Hiyo treni itakayo kua inazoa hizo kontena bandarini, ikisha zishusha hapo kwala inarudi tupu!!?
Wewe unajua adha ya foleni ya kushusha copper!? Embu anza kuuliza madereva nini kinawapata mpaka anamaliza harakati za kushusha hiyo copper, pia umeshawahi kutumia morogoro road hicho kipande cha manzese, bigbrother mpaka kuvuka tbl ubungo!? Wapo wanao tumia barabara ya ubungo maziwa watakusimulia japo hua haina msongamano, pale tabata mwananchi mpaka karibu na TIOTI unapajua!!? Mnaweza ganda kwenye foleni lisaa lizima mnasubiri gari igeuze au imefunga njia akitarajia apate nafasi ya kuingia upande wa pili, ama wewe hua unatumia king'ora kupita huko unakuta barabara zimesha safishwa ndio maana hukuti adha hizo!!?
 
Point yangu kubwa ni bandari ya kwala itumike kwa mizigo ya transit tu

ova
 
Sahv kwa siku wanapeleka kontena mara 2 kuonekane kuna jaaa mama si anakaribia kwenda huko hv karibuni....

Ova
Vipi huko Kwala kuna plugs za reefers containers ?

Wanashusha na kupakia kutumia crane aina gani Reach stacker au handlers?

Itabidi nifike huko kuna fursa nizicheki
 
..eneo ni la hekta 500.

..lakini ni hekta 5 tu ndio zimejengwa yadi ya zege kwa ajili ya makonteina.

..msikilize vizuri mhusika toka tpa anayehojiwa.
Miaka yote hiyo wamejenga heka 5 TU za zege 🤔, CGA pitia na hapa
 
Pamoja na ukatili wa bwana yule, hakika alikuwa anaiunganisha nchi kimyakimya. Sema chawa sasa
 
Bandari kavu zijengwe Morogoro na chalinze kwani chakinze ni njia panda kubwa ya Tanga moshi Arusha na Morogoro ni njia panda kubwa zaidi mikoa mingi, wajenge huko ili kuokoa watanzania na foleni kubwa za magari ya mizigo toka bandarini
 
Bandari Kavu italiokoa jiji la Dar na kero kubwa ya Foleni ya magari ya mizigo kwani sasa yatakuwa hayaingii Dar
 
Nchini Africa kusini Bandari ni nyingi kubwa kwa nini Tanzania hawaimarishi Bandari zingine ili meli ziende huko kuondoa msongamano bandari ya Dar
 
Kama kule baharini kwenye mlango hakuna ufanisi na ni kudogo haijalishi hata kama bandari kavu ni kubwa kama wilaya ya Namtumbo.
Beba kontena kwa Reli weka nje ya mji kuindoa misongamano kwanza ufanisi utakuja kukiwa hakuna misongamano ya magari ya mizigo
 
Wangezijenga Bandari kubwa Lindi au mkuranga ziwe ni Bandari maalum kwa mizigo ya Ndani ya Tanzania tu, meli zisambae kusiwe na foleni ya Meli Dar, Bandari ya Dar, Tanga na Mtwara ziwe Bandari za mizigo ya kimataifa tu kama ilivyokuwa kule Darban South Africa ambayo ni bandari ya kimataifa na bandari za Capetown, East London, pot Elizabeth ni kwa ajili ya kutoa kuingiza mizigo ya ndani ya Nchi, ijengwe Bandari mpya kubwa au wafufue bandari ya Bagamoyo pia
 
Bahari ya Tanzania ni kubwa Mkoa wa Pwani uwe na Bandari yao kama ilivyokuwa Tanga na Mtwara
 
Itahujumiwa tu kama walivyohujumu reli ya kati kuanzìa ile miaka ya 1990 ili wasafirishe mizigo kwa kutumia malori yao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…