Mbowe aachiwa huru na wenzake watatu baada ya DPP kuwasilisha hati ya kutotaka kuendelea na kesi

Hii inaonyesha nchi hii inamateso sana.

Kama wanafanya haya kwa Mbowe.. Mtu wa kawaida akibambikwa kesi si anafia jela?

Mbowe amesaidiwa sana na Wanasheria kuonyeasha udhaifu wa kesi.. Je ni watu wangapi wapo ndani hawana wanasheria?

Tunalalamika jela zimejaa na mahabusu lakini nina imani kesi nyingi ni za kutengeneza hasa kama mtu anakuchukia.. Anakutengenezea kesi hata ya kubaka au wizi.. Unakwenda na maji.

Tuombe hasa Katiba ibadilike kidogo hata polisi wataogopa kutengeneza kesi
 
Umejibu jambo tofauti na nililoandika!
 
Mbowe na wenzake walikuwa huru siku nyingi sana kabla.

Wenye akili walijua hivyo mapema sana.

Hii kesi ilikuwa inaleta aibu za reja reja.

Ila tumejifunza mengi sana kupitia hii kesi.

Sote ni binadamu na tuna madhaifu mengi sana.

Madhaifu ambayo yameingilia hadi mifumo tuliyojiwekea wenyewe.

Kesi ya Mbowe na wenzake itusaidie kujielekeza, kujiendesha na kujisimamia vizuri.

Kwa pamoja tuhamasishe upatikanaji wa Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi
 
Serikali wamekuwa wajanja Sana Mana kupitia kwa mbowe tayari magaidi walikuwa wanatengenezwa kweli na rebels waangekuwa wengi. Tayari hata jeshi lilikuwa limeshagawanyika hivyo mama angepinduliwa soon.
 
Kufutwa Kwa kesi hii kumeiletea heshima nchi yetu kwa maana haikuwa na afya kwa Taifa letu. Tunaishukuru serikali Kwa kuliona hili. Kazi iendelee na WaTanzania tuimbe wimbo mmoja tu sasa wa maendeleo.
 
Huwezi kufungua kesi ya madai kwenye shauri ambalo final decree haijatolewa. Kumbuka bado nole prosequie is not bar for subsequent proceedings basing on the same fact , hivyo wakikamatwa tena hawawezi kuweka P.O ya autrefois acquit ,autrefois convict au res subjudice , kulikuwa na mswada wa kubadilisha hicho kifungu cha nole kiwe bar sikumbuki kama mswada huo umesainiwa kuwa sheria
 
Usanii ndani ya sanaa

Unamtesa mtu kama utaishi milele wakati wote ni udongo na tunaoza na kuwa funza

Baada ya kuzikwa haufiki mwaka unakuwa umeoza

Tenda wema, Ishi kwa Furaha na Amani
Watu hawajali. Wanapowatesa wengine wao ndio raha yao mkuu
 
Sipendi Mbowe na wenzie waendelee kuwa mahabusu, lakini pia sipendi kusikia ameachiwa kwa MSAMAHA! Kama ni hivyo, basi kesi iendelee tuzijue mbivu na mbichi!

Na nina imani, kwa ushahidi uliotolewa, bila UJAJI WA MCHONGO, kulikuwa hakuna KESI hapo!
Hajaachiwa kwa "msamaha" kutoka kwa yeyote yule.

Kutokuwa na nia ya kuendelea na kesi kwa DPP sio msamaha,bali inaonyesha ni jinsi gani mtu/watu/kikundi kinaweza kupanga mateso kwa mtu/watu ilimradi tu katiba inawapa nguvu hiyo, bila hata ya kuwa na punje ya ushahidi wa kuishawishi mahakama.
 
Kwa Nchi yetu ilipofikia tupiganie katiba mpya kwa nguvu kubwa zaidi ili asitokee Tena kuongozi wa kuumiza watanzania wenzake kwa mambo ya kisiasa .Napenda Watanzania tuoendane na tusibaguane kwa itikadi za kisiasa.Kama mtu amekosea basi ahukumiwe kwa sheria na sio kisiasa.Tuipiganie nchi yetu ipate katiba mpya kwa maendeleo ya Tanzania.
 
Leo comte na Crimea watajiharishia damu.
Pambafu kabisa.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Mkuu usiwe pumbavu kiasi hiki!

Mtu kasota rumande karibia mwaka, na ndio lengo la ccm hilo au wewe ulifikiri ccm wanataka nini zaidi ya hicho?

Utakuta mnaanza kushangilia kama mazuzu! Yani ni sawa na mtu anakubutua makofi ya kutosha alafu baadae anakuambia nenda tu, kisha unaanza kushangilia!
[emoji23][emoji23][emoji23]

Sent from my SM-T295 using JamiiForums mobile app
 
Umeongea point sana Mkuu, niliwahi kwenda Magereza moja hivi kumcheki ndugu yangu aliyekuwa amefungwa huko,nilisikitika sana niliposikia baadhi ya wafungwa kuwa walisingiziwa tu na kwasababu ya kukosa watetezi wamebakia wanaozea Gerezani.Dunia hamna haki,haki inapatikana kwa MUNGU tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…