Mbowe acha mzaha na Damu za watu

Mbowe acha mzaha na Damu za watu

My Son drink water

JF-Expert Member
Joined
Nov 30, 2016
Posts
4,932
Reaction score
13,306
Nimekusikia majuzi ukisema, CHADEMA ipo tayari kuwasamehe kina Halima Mdee na wenzake waliokimbilia CCM kwa tamaa za pesa za ubunge.

Unachotaka kufanya ni kutudharau sisi wanachama wote wa CHADEMA na wote waliomwaga Damu zao kwa ajili ya Chama. Yaani Halima Mdee na wenzake eti wasamehewe na wanarudi kwenye Chama kama zamani kwa lipi?

Yaani they're the best of all members around Tanzania?

Kwamba bila hao wasaliti CHADEMA haiwezi be kuwepo?

Aisee acha mzaha na Damu za watu Mbowe,hao ni nyoka tayari hawawezi tena kurudi kuwa Binadamu.

Mtu Kama Halima Mdee alikuwa na dhiki gani ya kununuliwa na CCM?

Miaka 10 ya Ubunge,mshahara zaidi ya mil 10 kwa mwezi na mafao yote hayo Bado hakuridhika akakimbilia CCM kisa kakosa Ubunge baada ya kuporwa,who the hell are they?

Waache wafie huko CCM, kila aliyeondoka wakati wa mapambano hatumtaki, umeshatuuliza siye wanachama kuwa Tupo tayari hao wasaliti warudi?

Tunakuheshimu sana tunaomba ujiheshimu na usichafue hali ya hewa.

Ukiwarudisha hao wasaliti,pia mrudishe Ben Saane, Mawazo, na pia mrudishie Tundu Lissu afya yake na Aquilina pia tutaomba umrudishe.

Mbowe nitakuchukia maisha yangu yote na usithubutu kabisa.

Wewe siyo Mungu wa kusamehe watu hovyo hovyo tu.

Na ukiwa mbishi be prepared to pay the price, na CHADEMA itafia huko.
 
Hivi yale makato wanayokatwa wabunge ufipan hawa wamama huwa wanayawasilisha km taratibu za vyama zinavyoelekeza
 
Nilivyoelewa alisema wale walioondoka wakirudi wanaweza kupokelewa lakini hawa covid 19 hawakuondoka Bali walifukuzwa baada ya kukisaliti chama. Kama Mdee na genge lake wakisamehewa mimi nachana kadi na kamwe sitakaa nijiunge chama chochote wala kupiga kura.
 
Mangi aache pesa!! Wewe ndo uache mzaha kwa Mbowe. Siasa ni fursa, Kuna fursa hapo kwa wabunge 19 wa viti maalum
Akili hizo angekuwa nazo Nelson Mandela,South Africa isingekombolewa,hakuna mtu aliyekuwa anapewa fursa za pesa Kama Nelson Mandela,alichagua utu kuliko pesa,ndo maana ameondoka Duniani akiwa na heshima kubwa kuliko mtu yoyote Africa.
Pesa si lolote mbele ya utu.

Sent from my Infinix X688C using JamiiForums mobile app
 
Mbowe umemsikiliza au umeambiwa?

Kama wewe ni chadema kweli msikilize mwenyewe kisha uanzie hapo.

Ila kama wewe umejifunika bendera ya chadema kumbe ni wale wanaougulia awamu ya tano, pole sana kwani utatoka patupu.
 
Nilivyoelewa alisema wale walioondoka wakirudi wanaweza kupokelewa lakini hawa covid 19 hawakuondoka Bali walifukuzwa baada ya kukisaliti chama. Kama Mdee na genge lake wakisamehewa mimi nachana kadi na kamwe sitakaa nijiunge chama chochote wala kupiga kura.
Safi sana mkuu,na ndicho nilichopanga kukifanya,nitachana kadi ya CHADEMA,nitabaki bila Chama na Nitamchukia Mbowe Kama stupid killer

Sent from my Infinix X688C using JamiiForums mobile app
 
Mimi kusema ukweli pamoja na mapungufu ya Mbowe kama kiongozi ndani ya Chadema na kwingine lakini ni mmoja wa kiongozi bora sana na mwenye busara sana na hana mihemko ,hakika nasema wazi Mbowe ni mtu nanusu...Mbowe ana shaurika Mbowe ana utu sana tena kupita viongozi wowote wa upinzani.
Mbowe huwa ana teleza sana kama binadamu na kama kiongozi lakini kamwe Chadema awawezi kuwa na kiongozi aina ya Mbowe.
 
Huo uwezo wakumzuia mbowe hauna, utaishia kupiga kelele humu jf.
Mbowe kaweka pesa mbele, na ana misukule ya kutosha na subiri uone kama utafurukuta.
Kama una uchungu sana ungeanza kumsema alipokuwa anakamua ruzuku za chama
 
Pole sana ,niamini kuwa Mbowe anajua namna hao mnaowaita wasaliti walivyofika bungeni,na atawasamehe na Mambo yataendelea
 
Nilivyoelewa alisema wale walioondoka wakirudi wanaweza kupokelewa lakini hawa covid 19 hawakuondoka Bali walifukuzwa baada ya kukisaliti chama. Kama Mdee na genge lake wakisamehewa mimi nachana kadi na kamwe sitakaa nijiunge chama chochote wala kupiga kura.
Hakuna tofauti kati ya hao walioondoka wenyewe na akina Mdee kwani kimsingi wote ni wasaliti. Kama ni lazima kuwasamehe waliojiondoa wenyewe basi hao 19 nao wasamehewe pia.
 
Kwa UVIKO 19 twende taratibu.
Ni wachache kuliko umma imani ya chama.
Hao wabaki hukohuko kwa ndugai.
Mbowe awe kilometa kadhaa na agenda ya UVIKO 19

UTU UTU UTU UTU UTU
 
Back
Top Bottom