Uchaguzi 2020 Mbowe adhalilisha vyama vyote vya upinzani nchini, adai havistahili kupewa haki ya kunadi wagombea wao

Uchaguzi 2020 Mbowe adhalilisha vyama vyote vya upinzani nchini, adai havistahili kupewa haki ya kunadi wagombea wao

Securelens

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2020
Posts
316
Reaction score
541
Leo kwa mara nyingine CHADEMA imeidhihirishia umma kuwa ni chama cha kidikteta na isiyoheshimu misingi ya demkrasia, uhuru na haki ya kisiasa ya kila chama na kila mtanzania.​

Dunia yote imeshangaa tamko la Mbowe leo akisisitiza huku akitokwa na povu kwamba CHADEMA na CCM tu ndivyo vyama pekee vinavyostahili kupewa fursa ya kujinadi Tanzania bara kwa madai kuwa upinzani upo baina ya vyama hivyo viwili, Amedai vyama kama ACT, CUF, NCCR, TADEA na vingine havistahili hata kupewa fursa ya wagombea wao wa urais kujinadi kwenye ratiba ya TUME na kwamba vyama hivyo ni uzibe kwa CHADEMA.​

Kwa chama kinachojinasibu kuwa ni cha demokrasia na kinachodai kina sera ya uhuru na haki kutoa tamko kama hili limeshtua dunia. Hii ni dhahiri CHADEMA ni chama cha kidikteta na kama ndicho leo kingekuwa madarakani Mbowe angevifuta vyama vyote hivyo na kubakiza CHADEMA pekee yake. Duniani kote katika mfumo wa demkrasia vyama vitogovidogo vipinna vinapewa haki sawa ya kunadi sera zao.​

Hata Marekani, Uingereza, Ujerumani n.k kuna vyama vidogo vidogo. Chama kidogo leo kinaweza kuwa chama kikubwa miaka 10 ijayo. Kwa nini vinyimwe fursa? Nafikiria uchaguzi wa 1995 chama kilichokuwa na nguvu na upinzania mkubwa kwa CCM kilikuwa NCCR-Mageuzi, hivi Chadema kingefutwa leo kingekuwa wapi.​

Kwa nini leo Chadema inaona NCCR -Mageuzi haistahili kupewa haki ya kunadi sera zao na mgombea wao wa Urais?, Hivyo hivyo kwa TADEA na vyama vingine.​

Watanzania na dunia inazidi kufahamu sura halisi ya CHADEMA. Watanzania wenzangu na wapenda haki na demokrasia, pingeni chadema kwa nguvu zote na tuiadhibu kwenye kura ya Oktoba 28.​

Hatutaki chama cha kidikteta na chenye ubinafsi kama CHADEMA na mgombea wake Lissu anayetoa lugha za dharau kwa wagombea wa vyama vingine hata ndani ya upinzani. Tupilia mbali Chadema, Tupilia mbali Lissu. Tunakwenda na Rais Magufuli.​

Tunakwenda na maendeleo na demokrasia.​
 
Na ndio maana hata wao wanadharaulika na CCM. Hiyo hesabu ni simple, wala haihitaji kuumiza akili.
 
Hiki chama kina dharau sana kwa vyama vingine. Ndio maana watanzania hawakiamini otherwise ingekuwa balaa.
 
Itoshe tu kuutahadharisha uongozi wa CHADEMA kuwa wamepanua wigo wa chuki dhidi yao. Sasa siyo kati ya wanachama wa CCM wanaochukizwa na dharau ya Lissu dhidi ya M/Kiti wao na mgombea Urais, ambaye bado ni Rais wa nchi, sasa watachukiwa na wanachama wa vyama vya siasa anavyoviita majina ya hovyo



Yawezekana uongozi wa CHADEMA hawamtakii mema mgombea wao wa Urais. Kama ukweli ndio huo, kauli hiyo ya Mbowe inawatosa wagombea wote wa chama. CCM na vyama vyote vimepata agenda ya kuibomoa
 
Walio punguani tu ndio wataichagua chama cha Mbowe. Watanzania watawapa Somo chungu, Oct 28.
 
Back
Top Bottom