Mbowe ahusishwa na UFISADI wa kuimaliza NSSF



Haya ashura upo hapo hadi sasa ?? au bado ??
 

hili jambo lipo sana hapa lakini wanafaa kupuuziwa ! nitakuja kujadili vizuri hapa muda si mrefu !
 

Mtanzania,

nimekuuliza hili swali over and over again kuwa Mbowe anadaiwa kiasi gani na terms za deni lake ni zipi lakini naona umeamua kukaa kimya....

Wakati mwingine NSSF wamesema kuwa Mbowe alipewa miaka mitano ya kulipa deni lake na wakati mwingine wakafungua kesi ya kudai kuwa pesa yote waliyoamua wao NSSF ilipwe. Kama mahakama za Tanzania haziamua swala muhimu kama hili je hiyo kesi ya mafisadi inayokuja ambayo hata Kikwete mwenyewe yumo zitaamua?

Bado nataka hii thread iwe hapa juu kabisa ili ijadiliwe kwa undani na uongo na ukweli wa hili deni la Mbowe ujulikane!
 

Kama wameanza kubadili story kuwa Mbowe kachoma benki na mara sio Mbowe ni Nyirabu na Nyerere unategemea watafungua kesi mahakamani bila ushahidi?

UKiona watu wameanza kuongea kuwa Mbowe anatembea na mke wa Mkapa au Kikwete basi ujue kuwa wameishiwa. Na uzuri ni kuwa JF imeaanza kuwaanika taratibu ili wajulikane!
 

Mwk
Binafsi nadhani maelezo ya Masaka(kuhusu Mbowe versus Anna na Salma) yanaelekea upande mwingine tofauti na mwanzilishi wa mada. Naweza kuwa nimekosea.
 
Mwk
Binafsi nadhani maelezo ya Masaka(kuhusu Mbowe versus Anna na Salma) yanaelekea upande mwingine tofauti na mwanzilishi wa mada. Naweza kuwa nimekosea.


Mwaka huu hapa JF tutasoma mengi naona mikakati ya maafisadi inafanya kazi.Naona group la watu wenye vijimambo vya kijimba wameingia kama nyuki. Naamini mkakati ni kuandika mambo ya kijinga kwa wingi ili kukatisha tamaa watu makini kuingia na kuja kuchangia hoja muhimu.Mwisho wa yote ni kuifanya JF idharaulike.Watanzania njaa kwelikweli pesa na maafisadi zafanya kazi.
 
Mwk
Binafsi nadhani maelezo ya Masaka(kuhusu Mbowe versus Anna na Salma) yanaelekea upande mwingine tofauti na mwanzilishi wa mada. Naweza kuwa nimekosea.

Una hakika gani kuwa Masaka na aliyeanzisha hii mada sio the same person au the same group? Karibuni kumekuwa na tabia ya watu kuwa na multiple log ins na kuanza kuendeleza mada za kushambulia JF na kupongezana kwa fujo nyingi.

Fuatilia sana uone kuwa kuna trend hapa na inatafutwa sababu hapa ya kufanya mada kama hii ihamishwe halafu uone watakavyojazana hapa wakimpondea Ole na Mods wengine kuwa mada zao za Mbowe zinahamishwa!

Watu wako kwenye mission ya kuharibu hadhi ya JF na bahati nzuri JF inawasubiria kama kawa ili waaibishwe!
 

Hii mission yao imeshashindwa on arrival.

Na washindwe tena walegeee kabisa maana hilo halitatokea hata wafanye nini. Wanajaribu kuwatoa watu ili wasifuatilie report ya kamati ya madini ambayo iko karibu kabisa kuvuja hapa JF kama ilivyo kawaida. Wakicheza hii game watakutana na moto wa JF kwa vile hapa tuko always five steps ahead!

Yaani katika mambo yote wao wanaleta hoja kuwa Mbowe katembea na wake wa maraisi wawili wa Tanzania? Hii inasaidia nini kuweka madawati kwenye ile shule ambayo michuzi kaiweka kwenye blogu?
 

BINTI MREMBO WA KIAFRIKA ....HII ANZISHIA THREAD YAKE TUJIMWAGE....!
lingine ni kuwa wana-JF...please please...matusi na kasha zisizo na msingi tuache.....!Hoja inapotolewa ni hoja tu ndo ijadiliwe........! tusitoke nje ya mada waheshimiwa....!
 
BINTI MREMBO WA KIAFRIKA ....HII ANZISHIA THREAD YAKE TUJIMWAGE....!
lingine ni kuwa wana-JF...please please...matusi na kasha zisizo na msingi tuache.....!Hoja inapotolewa ni hoja tu ndo ijadiliwe........! tusitoke nje ya mada waheshimiwa....!

Muda huo wa kumwanzishia Shigongo haupo ndugu yangu. The guy nilimfuta kabisa maishani mwangu pale alipomwandama Amina Chifupa (RIP) kwa habari za uongo kabisa toka kwa Nchimbi bila kujali kabisa maombi yake anayodaganya watu kila siku huko kanisani kwake! Akianzishiwa thread hapa atakuwa anapanda cheo.

Kwa sasa mimi nawasubiria haapa wanaodai kuwa Mbowe katembea na mke wa Mkapa na anamfukuzia mke wa Kikwete (poor mama salma)!
 

HAPO MWANDISHI HAKUSEMA KUWA MBOWE ALICHOMA BOT.....ZILIZOCHOMWA NI NYARAKA ZA GREENLAND BANK ILIYOFILISIKA.....!
WAJUMBE TUSIPOTOSHE MADA ......HILI LA GREENLAND BANK NI JIPYA......NA HILI LA SISTER WA MBOWE KUTORUDI TZ LINAHITAJI MAJIBU ZAIDI YA CHENGA.......!
 

Tatizo liko kwako na "yule aliyeanzisha mada" kuelezea hili na sio kulaumu watu ambao hawajasoma unachosema kujua wewe bila kukisema in the first place!
 
Tatizo liko kwako na "yule aliyeanzisha mada" kuelezea hili na sio kulaumu watu ambao hawajasoma unachosema kujua wewe bila kukisema in the first place!
YAMEKUWA HAYA TENA.....! WACHANGIAJI NA WASOMAJI......! MADA ILIYOPO INASEMA "MBOWE NI FISADI MZOEFU" MTOA MADA AMELETA USHAHIDI WAKE JAMVINI( ambao chanzo anakijua mwenyewe na huenda habari hii wahusika(?)hawana) MWENYE KUJUA ZAIDI KUHUSU USHAHIDI HUO AULETE.....,NA WENYE KUFUMBULIWA MACHO TUMEFUMBULIWA....! NI VIZURI MBOWE MWENYEWE(maana nasikia haonekani humu)AJE NA MAJIBU MBADALA......!(mbona la NSSF kalitolea jibu japo lina mashaka?)HOJA NYINGINE ANASHINDWA KUZITOLEA MAJIBU.........!(vogue,BOT,greenland,chiku abwao....nk?)(
 

Kama Mbowe akianza kujibu mambo kuwa anatembea na mke wa Kikwete au alitembea na Mke wa Mkapa basi atakuwa amekosa kazi kabisa.

Wanaccm, haya mambo ya kutunga kashfa za ngono na story zisizoeleweka hayatapunguza juhudi za kupambana na ufisadi mnaofanya hapo bongo. Katika hili mahesabu umechemsha.. tafuta lingine.. labda uibue lile mliloanzisha mwaka jana kumpaka Slaa matope!
 

Halafu mkimaliza kuwachafua wapinzani mtakuwa mmefanikiwa kufanya nini? hii nchi inahitaji mabadiliko makubwa sana kama hii ndio top brass ya ccm hapa mtandaoni!
 
Niliwahi kusema hapo juzi kuwa kabla ya mkutano wa NEC hapa Butiama kuna mengi yataanzishwa ili kutuhamisha na haswa kwenye kushinikiza serikali ya mseto kule znz na mafisadi wetu wa EPA kurudisha fedha zetu watajwe na kupelekwa mahakamani.

Nipo Butiama hapa ulinzi unatisha sana sana kiasi kwamba huwezi kuamini kuwa huu ni mkutano wa NEC utafikiri wanakuja kujadili kupindua nchoi wakati wao ndio wenye nchi.

Mengi hapa yana kuja na baada ya siku moja ama mbili utayasikia magazeti fulani ya Habari Corruption pamoja na majira linalomilikiwa kwa kiasi kikubwa na yule Manji mwenye kutuibia mabilioni kwenye majengo ya NSSF pale ubungo yakiandika na kusema wametoa kwenye mtandao .

Ushahidi ni muhimu sana ,Mbowe anatakiwa kuwa makini zaidi ili kuweza kuwajua wabaya wake kwani hapa kuna mbinu za ziada.......KABLA YA NEC KUTAKUWA NA MAMBO. ila wajue wengine tayari tumetia timu humu kijijini ili kuweza kuwahabarisha wana JF nini kinaendelea hapa.
 
Halafu mkimaliza kuwachafua wapinzani mtakuwa mmefanikiwa kufanya nini? hii nchi inahitaji mabadiliko makubwa sana kama hii ndio top brass ya ccm hapa mtandaoni!


Mwafrika wa Kike, naomba tu nikupe idea, topic kama hii unaikuza bure. In order for these topics to cease, let them die a natural death by all of us giving them silent treatments. In my opinion U are giving them more ammunition by even discussing.

Silent Treatment sometimes works!!!

my 1 cent.
 

Asante M K ..

Fuatilia pia ujue kama wataongelea huu udaku kuwa Mbowe anatembea na mke wa Kikwete!?
 

Moelex23,

Heshima mbele mkuu! Tofauti ni kuwa sina nia ya kuacha hii topic ife (as of yet). Ningekuwa nataka ife ningeiacha long time ila kwa sasa naiweka hapa juu ili kufutilia mbali kabisa huu udaku na upuuzi unaoletwa hapa na wanaccm kuwa Mbowe ametembea na Mke wa Mkapa na pia anataka kutembea na mke wa Kikwete.

Demokrats wanapigwa bao kila mwaka na republicans hapa USA kwa sababu wakiona topic za kipuuzi na kidaku kama hizi basi wanaamua kuzipuuzia kwa kudhani kuwa zitaisha zenyewe na kumbe wenzao wamepania (muulize JK mwaka 2004).

Siasa ni perception na sometimes udaku kama huu ukiachwa tu kuendelea baadaye kuna watu wanadhani kuwa ni ukweli na inakuwa too late kufuta hiyo perception. Kumbuka kuwa Kikwete ni rafiki mkubwa wa Kichaka (ambaye ni republicans) kwa hiyo hizi zote wanazoleta hapa kina mahesabu zinatoka kwenye kitabu cha republicans. Kwa hili mafisadi hawapewi breki.

Wana JF wengine wanaendelea kuchangia threads zingine na mambo yanaendelea kama kawa mkuu!
 
is mbowe a threat? AM I MISSING SOMETHING?? Come on CCM people..have faith in ya party...its stronger than that...lol
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…