KadaMpinzani
JF-Expert Member
- Jan 31, 2007
- 3,715
- 92
Suala la deni NSSF CCM walilitumia wakati wa uchaguzi mkuu 2005. Haya waliyoyaandika Rai sasa yalisambazwa sana 2005 lakini magazeti yakakataa kuandika. Ni gazeti moja tu la MZALENDO ndio likaandika.
NSSF wamepewa maelezo wasilimalize ili swala ili Mbowe aendelee kuwa na kitanzi. Ni mahakama pekee sasa itasema wazi anadaiwa bei gani na naamini mahakama ikisema, atalipa.
Kwa nini NSSF hawataki kusema wanadai kiasi gani wala hawataki majadiliano?
Asha
Dada Asha,
Usitufanye wana JF mbumbumbu kweli kweli. Kuna mabaraza mengi tu ya kushughulikia migogoro ya kibiashara Tanzania.
Pia kuna mahakama kuu, Mbowe hajaenda huko kote kudai kabambikiziwa deni.
Case aliyofungua Mbowe ni tofauti kabisa, ni case ya kudai amri ya mahakama isitekelezwe, kitu ambacho ni tofauti.
Alikuwa na miaka mingi tu ya kumaliza deni lake lakini hakufanya hivyo. CCM sio wajinga kwamba watawaambia NSSF, wamkabe tu Mbowe bila sababu. CCM wanatumia weaknesses zilizopo ili kuwakamata wanasiasa wa upinzani. Weaknesses nyingi ni kwenye mambo ya biashara. Ndio mbinu hizo hizo hata mafia wa Italia wanatumia. Hawawezi kumkaba mtu asiye na tatizo, sana sana wataishia kumuua. Wao wanakuvuta na kukuingiza kwenye scandal, kisha wanahakikisha unabaki kuwa nao.
Mbowe baada ya kuamua kuwa mwanasiasa tena wa upinzani, alitakiwa alimalize hili deni la NSSF. Maana kwa kukopa NSSF tu tayari kuna tatizo hata kama angelikuwa analipa ontime.
Haya ashura upo hapo hadi sasa ?? au bado ??