Mbowe ahusishwa na UFISADI wa kuimaliza NSSF

Tunasoma katika historia ya mwanadamu kuwa amepitia katika vipindi vikuu vitano vya maisha vinavyoitwa mifumo au modes of production.Mfumo wa kwanza kabisa unaitwa primitive communalism(ujima) mfumo wa pili unaitwa ukabaila(feudalism) na mfumo wa tatu unaitwa utumwa(slavery) na mfumo wa nne unaitwa ubepari(capitalism) ambao msingi wake ni mtaji yaani capital,na mfumo wa tano ni ujamaa(socialism) ambao msingi wake ni utu na usawa wa binadamu,wenzetu warusi walienda mbali zaidi na kuunda mfumo wao ambao unaitwa ujamaa uliokomaa(communism) ambao hata hivyo haukufua dafu mbele ya ubepari japo bado vipande vyake vipi.

Kwa sisi waafrika mifumo yetu miuwa ilikuwa african socialism na huo ujima,lakini badala ya sisi kuamua kwenda kwenye ubepari moja kwa moja au ujamaa uliokithiri tumeunda mfumo mpya wa maisha uitwao Ufisadihata sijui kwa kiingereza neno sahihi ni lipi maana unainclude egoism,corruption,embellezlement,nk.
Mfumo huu ni mbaya kabisa na hatari zaidi duniani,ni hatari hata kuliko ubepari wenyewe.Kwani ubepari wenyewe hauna egoism sana kama huu mfumo wetu sasa.Na kwakuwa umeshakuwa mfumo basi kila mtu ameambukizwa mfumo huu sio sisi wana jf tunaojadili hapa wala hao viongozi na watu mbalimbali tunaowajadili hapa.wote ni mafisadi katika level moja au nyingine.Tinachotofautiana hapa ni degree ya huo ufisadi ambao mimi huita degree of chumpability,that all human beings are chumperble but we differ in te degree of chumperbility
Usiniulize hiyo lugha ina maana gani,tafakari message yangu na kama utatafakari kwa kina sana utagundua namaanisha nini ila ukidandia gari kwa mbele waweza jikuta unajadili usichokijua.Nasema huu mfumo umeathiri watanzania kiasi kwamba hata watoto wanaozaliwa wanavuviwa ufisadi.Maana mtoto anazaliwa katika mazingira ya ufisadi,anahudumiwa katika mazingira ya ufisadi hadi anakua mkubwa.Kutokana na mfumo huu mtu anajifunza kutoa rushwa akiwa chekechea,kwani akitaka kuwahi shue lazima atoe rushwa ili awahi,na kila huduma.Sio kwamba anapenda bali mfumo unamlazimisha kwa kuwa ndio njia ya maisha.Inashangaza sana kuona hata wanafunzi wa shule za msingi kwa sasa wanawafuata walimu wanawabembeleza kuwaongezea maksi,au kuwashawishi kupitia alama za miili yao(paralinguistic features),sasa kisheria hakuna kitu kinachoenda bure,kilatini tunasema quid pro quoyaani kwa kiiingereza nothing goes for nothing.Mwalimu naye hawezi kutoa maksi bure atataka kulipwa in kindambapo ni moja ya malipo yaliyokuwepo kwenye mfumo wa ukabaila.In kind kwa sasa maana yake ngono,lakini awapo mwanaume atalipa in cash,ambayo pia ni mfumo wa maisha ya ukabaila.Kwani mwalimu huyu huenda kwake hela si shida sana,sasa akimwambia demu huyo ampe laki moja ni wazi atashindwa njia ilobaki ni ngono basi.Hivi ndivyo tunavyoanza kuharibika.
mfumo huu hauishii hapo unaenda hadi kwenye shule za sekondari,high schools, na vyuo vikuu.Siku hizi hata kugombea uhead prefect tu lazima uwe na kampeinazi ambao lazima uwalipe na uwaahidi feva ukiingia madarakani.Humo DARUSO na serikali za wanafunzi wa vyuo vikuu ambao tunawategemea waje kuwa viongozi wetu waadilifu tena na wao wenyewe wanaongoza maandamano kupinga ufisadi kuna ufisadi kibao.Hivyo nachokiona sasa ni kulalamikiana kwamba aah bwana wewe umechukua kingi kuliko mimi haiwezekani rudhisha bwana.Kila mtu anapiga debe bovu mwenzie atoke aingie yeye naye aibe aende.Huo ndio mfumo tulionao sasa.
Kwa mantiki hii hakuna mtu msafi serikalini wala walionje ya serikali bali waliopo wana afadhali kidogo kuliko hao wa serikalini.Msingi mkubwa wa mfumo huu wa ufisadi ulipo sasa ni mtaka cha uvunguni sharti ainame

Kwa mantiki hiyo kila mtu akijichunguza hapa jf hata kama dhamiri yake inamsuta atagundua kwamba katika hali moja au nyingine katika maisha yake amewahi kutoa ama kuomba rushwa ama upendelea fulani.Si kwakuwa anapenda kwakuwa tu alilazimishwa na mazingira.Huyo mbowe tunayemjadili hapa ndio ni mtu mahiri lakini si msafi kwa 100% wala kiongozi yeyote tutakayempigia debe hapa hatakuwa 100% pure.Analau basi tupate wale ambao tukiwarate watapata above 75% hapo ndio tutakuwa tumefikia lengo.

Lakini kikubwa nani katufikisha hapa? hili wala sio la kubishaniwa ni baba mwenye nyumba,na ninaposema baba mwenye nyumba sio jk namaanisha chama kinachotawala.Kwakuwa hicho ndicho chenye dhamana ya kushikilia mfumo wa nchi na kuandaa sera,basi kinawajibika moja kwa moa na hali hii na pia kama wakikubali hili wao wenyewe pia wanawajibika kutuondoa hapa tulipo.Kama wanayo nia wanaweza kama hawana hata watawale miaka 200 ijayo hatutafika popote.Imefikia hatua serikali zetu za kiafrika kwa sasa ni hatari kuliko hata ukoloni.Adui yetu mkubwa kwa sasa sio IMF wala WORLD BANK ni serikali zetu ambazo.World bank sawa watatupa dola milioni mia moja tujenge daraja na masharti magumu na riba ya kurudisha lakini pamoja na hayo tukishapokea huko kwenye daraja nangurukuru zitafika milioni ishirini.Je,hapa tuwalaumu world bank?

Ukitaka kujua ufisadi ni mfumo basi test ni ndogo sana ni hii hapa,leo teuliwa kuwa waziri kaa miaka kumi afu usijenge nyumba ya maana jenga bangaloo moja tu linaloendana na mshahara wako na nunua kasuzuki kamoja kakutembelea baada ya kuacha uwaziri.Watu watakucheka watakwambia mmh lile ndo jinga kweli yaani limekaaa pale kisimani limeshindwa kuchota pesa na ona sasa si bora angekuwa mkuu wa shule ya msingi tu.What does that mean,we everuday encourage people who go to power to continue with maladministration na ufisadi.

Naomba kuwasilisha hoja
 

Hivi kweli ni mtanzania wa aina gani wewe unayeshupalia watu wenye migogoro ya mikopo halafu unawaacha wale waliofanya muflis nchi hii na kupelekea mambo kama haya..na mengineyo ambayo athari zake ni vifo,maradhi na njaa!MTANZANIA GAZETI AMA MTU?
 
Mbowe ni mfanyabiashara sasa hivi, tena hii ina include hata zile ambazo ni chafu machoni mwa raia wema mbele ya jamii. Hivi kuna mtu anayeamini kwamba huyu mtu akiingia ikulu ataacha hizi biashara? Expect worse than Mkapa, hiyo itakuwa ni chance kwake ku expand scale ya operations zake.
 
wewe kana ka nsungu, umetumwa nini na hao mafisadi kuja kumchafua mbowe ? lol, (joke)
lakini ulichosema ni kweli !
 
wewe kana ka nsungu, umetumwa nini na hao mafisadi kuja kumchafua mbowe ? lol, (joke)
lakini ulichosema ni kweli !

No price Kada can buy my freedom of speech!I know its a joke but thats the truth from my point of view.
 

Does it mean Kada unakubaliana na views zangu kwa Mkapa?Yeye amefanya large scale business alipokuwa ikulu, and I expect Mbowe to do more than him akiingia nyumba kubwa.Mind you Mkapa alikuwa ha exist kwenye ulimwengu wa biashara laipochukuwa kiti kikubwa!
 

absolutely ! nakubaliana na unachosema, nilikuwa namaanisha watu wa hapa watakuja kukwambia unalipwa uje kumchafua mbowe ( kwa kusema your views) !

Sheikh Nkapa alifanya large scale wakati yeye sio mfanyabiashara, akiingia mfanyabiashara sijui atafanya kufulu gani aiseee ! i cant picture that out !
 

Kada you are talking the talk my mate!Mfanya biashara yeyote atakeyeingia ikulu ataendelea na biashara zake, labda atakachofanya ni kubadilisha majina tu ya wamiliki!I think Mbowe is better off as a businessman, akiingia ikulu ataendelea kula vichwa kwa kwenda mbele katika kipindi chake cha miaka kumi, jamani tusije tuishia kujuta wabongo kama wenzetu wakenya walivyompa ulaji Kibaki.Kitila upo kaka?
 

JF Tumeingiliwa na watu ambao wanaonekana kuwakilisha kikundi fulani. Na wapo kwa ajili ya kupaka watu wengine matope. Mimi naona ni vyema kama wamepewa kitu kidogo, wale na wakae kimya, siyo kuandika habari zisizo na kichwa wala miguu. Nadhani Mbowe haja kataa kama alikopa hizo pesa. Na ninavyomfahamu huyu mwana harakati anajua kabisa ni hela za walala hoi yuko tayari kuzirudisha, ila ni wajibu wa NSSF kumuonyesha ni kiasi gani halali anachodaiwa. Hoja iko wazi Mbowe anadaiwa na hajakataa na wote tunajua hilo. Je yako wapi majina ya mafisadi wa EPA na KIASI WALICHOPEANA KWA SIRI???MIMI naona hiyo ingekuwa na mantiki zaidi kwa Watanzania kuliko kumuandama mtu ambaye amekopa kwa ufuata taratibu sahihi.
 

na sidhani kama hii case is anywhere near the end, maana kwa ufahamu wangu ni kwamba itaibuliwa over and over especially kwenye siasa !
 
No price Kada can buy my freedom of speech!I know its a joke but thats the truth from my point of view.
Mnahanya nini wakati hata sio time ya uchaguzi?presha mapema yote hii?Dont you guys recognize and respect the fact that we still have a president?and that there are some issues we need to discuss during this defining moment?I ALWAYS SAY THAT "IT IS TIME TO EMBARK OUR SELVES WITH POLITICS THAT MAKES SENSE IF WE'RE TO MOVE OUR COUNTRY FORWARD!"
 

GOOD!!!!YOU BETTER STAY WITH YOUR THOUGHTS
 
Hiyo ni janja ya serikali ya CCM naona hiyo ya Richmond inawauma bado
 
kuna jambo muhimu la kitaifa tunalijadili kiushabiki na kinafiki hata tunajitia upofu wa akili. sisi ni sawa na panya wanaoacha kujadili jinsi gani watamfunga paka kengele badala yake wanajadili milio ya paka wanaowala!

sielewi viwango vya ufahamu na elimu walivyonavyo watu wanaoshindwa kutambua tofauti kati ya kukopa na kuiba kwa kutumia dhamana ya cheo ulichopewa na wenzako ili uwaongoze kulelekea kwenye mafanikio ya pamoja!

Tatizo siyo kukopa kwa Mbowe NSSF bali ni pale gazeti linalomilikiwa na mtu anayehushishwa na kashifa nyingi za kuitafuna nchi yetu (ROSTAM AZIZI),gazeti la Rai lilipoandika kuwa "Mbowe aifilisi NSSF!

kwa hiyo NSSF wenyewe kwanza wanakanusha kwamba hawafilisiwi kwa deni wanaomdai Mbowe,pili wanatuhabarisha kwamba kesi kuhusu deni hilo iko mahakamani.Ndiyo maana Mwanakijiji anauliza kama ni busa kwa Mbowe kulipa deni ambalo kesi yake iko mahakamani?

na ingawa kuna watu humu ndani wanataka tuamini kuwa Mbowe hataki kulipa deni,lakini ukisoma kwa makini utaona kuwa mbowe hakatai kulipa deni bali anataka mantiki ya kwa nini alipe kiwango anachoamini kuwa ni zaidi ya kiwango cha deni kimahesabu

katika biashara kuna kitu kinaitwa "bad Debt" au deni lisilolipika,na hii ni hali ya kawaida kabisa kwenye taasisi za kifedha "financial institutions" lakini mabishano kati ya Mbowe na NSSF si kwamba mbowe deni lake halilipiki bali ni kiwango cha deni lenyewe na kiasi cha fedha kilicholipwa

hoja za kipuuzi humfanya mtoa hoja aonekane mjinga au ametumwa!
 
sielewi viwango vya ufahamu na elimu walivyonavyo watu wanaoshindwa kutambua tofauti kati ya kukopa na kuiba kwa kutumia dhamana ya cheo ulichopewa na wenzako ili uwaongoze kulelekea kwenye mafanikio ya pamoja!

Mkuu,

Mimi nina elimu ya Ngumbaro, je vipi inakusaidia kupata conclusion yako?

Je mwenzetu una elimu ya kiwango gani?
 
kwanza lazima uelewe kwamba neno Ngumbaro maana yake ni mtu mzima kwa hiyo tuliamua kuiita elimu ya Ngumbaro tukimaanisha elimu ya watu wazima.

kwangu mimi kuna tofauti kati ya kusoma na kuelimika,kusoma kunahusiana na mitihani wakati elimu inahusiana na uwezo wa kupambana na mazingira yako na jinsi unavyopambana na matatizo yanayokukabili kwa wakati.

kwa mfano msomi anaweza kujua 2+2=4 lakini akashindwa kujua kama kura mbili ukijumlisha na kura mbili nyingine zinapatikana kura nne zitakazowesha kuondoa utawala usiojali maslahi ya taifa madarakani. mantiki yangu hapa unaweza kuwa msomi wa sheria lakini usiwe na elimu ya sheria na wakati huo huo unaweza kuwa na elimu ya sheria lakini usiwe msomi wa sheria!

ingawa kuna mahusiano ya karibu sana kati ya kusoma na kuelimika lakini pia kuna ukweli usiokanika kwamba kuna wasomi wengi tuu lakini matendo yao yanawaonyesha kwamba hawajaelimika.

kuhusu Mbowe na NSSF hata mtu mwenye kiwango kidogo sana cha elimu na uelewa anaweza kabisa kutambua tofauti iliyopo kati ya Mbowe aliyekopa kihalali na anayepigania haki yake mahakamani na wale mafisadi waliotumia ofisi za umma na madaraka tuliyowapa kujitajirisha kiharamu
 
Kigarama hili somo ndugu yangu!

Kuna mtu huko nyuma alitolea mfano kuwa mbona Aden Rage alifungwa kwa deni... lakini mtu huyo hajatokea leo na kutuhabarisha kuwa Mahakama Kuu imefutilia mbali hukumu ya mahakama ya chini na kumfutia adhabu yote kwani hatia aliyopatikana nayo haikuwa sawasawa na Hakimu hakuzingatia ushahidi uliotolewa.

Hii ndio sababu watu wanaenda mahakamani hadi hatua za mwisho za rufaa. Kwanini watu waone kuwa ati kwa vile Mbowe ni mwanasiasa basi alipe deni tu wakati ana kesi mahakamani iliyofunguliwa na NSSF? Kwanini tusiache mkondo wa sheria ufuate njia yake hadi mwisho na kama baada ya mchakato huo kuisha na Mbowe akakaidi amri ya mahakama basi sisi sote itabidi tumpigie kelele kuwa atii amri halali ya Mahakama?

Kwanini alipe deni tu ili kujijengea mazingira mazuri ya kisiasa hata kama deni hilo ni la kihuni?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…