kwanza lazima uelewe kwamba neno Ngumbaro maana yake ni mtu mzima kwa hiyo tuliamua kuiita elimu ya Ngumbaro tukimaanisha elimu ya watu wazima.
kwangu mimi kuna tofauti kati ya kusoma na kuelimika,kusoma kunahusiana na mitihani wakati elimu inahusiana na uwezo wa kupambana na mazingira yako na jinsi unavyopambana na matatizo yanayokukabili kwa wakati.
kwa mfano msomi anaweza kujua 2+2=4 lakini akashindwa kujua kama kura mbili ukijumlisha na kura mbili nyingine zinapatikana kura nne zitakazowesha kuondoa utawala usiojali maslahi ya taifa madarakani. mantiki yangu hapa unaweza kuwa msomi wa sheria lakini usiwe na elimu ya sheria na wakati huo huo unaweza kuwa na elimu ya sheria lakini usiwe msomi wa sheria!
ingawa kuna mahusiano ya karibu sana kati ya kusoma na kuelimika lakini pia kuna ukweli usiokanika kwamba kuna wasomi wengi tuu lakini matendo yao yanawaonyesha kwamba hawajaelimika.
kuhusu Mbowe na NSSF hata mtu mwenye kiwango kidogo sana cha elimu na uelewa anaweza kabisa kutambua tofauti iliyopo kati ya Mbowe aliyekopa kihalali na anayepigania haki yake mahakamani na wale mafisadi waliotumia ofisi za umma na madaraka tuliyowapa kujitajirisha kiharamu
Kigarama,
Ushauri wa bure, jiepushe na mijadala ya nani ni msomi na nani sio msomi. Unachofanya ni sawa na kumnyoshea mtu kidole kwamba mjinga yule na kusahau kwamba kuna vidole vitatu vimeelekezwa kwako na vinakuambia na wewe je? Mbona mjinga zaidi ya huyo unayemsema?
Diversity haiko tu kwenye maumbo ya watu au rangi peke yake, bali iko hata katika
jinsi wanavyofikiri. Kuwa na mawazo tofauti juu ya jambo haina maana nani kasoma au kaelemika na nani hajaelemika.
Kuelemika kwa binadamu kunaonekana sio katika hoja bali katika uwezo wa kupambana na mazingira yanayokuzunguka.
Inaniwia vigumu hapa JF kuamini kwamba hao wanaojiita wameelemika, hawezi kujadili hoja bila lugha za kashfa, kama huko ndiko kuelemika, basi tunaishi kwenye dunia tofauti.
Kama suala la Mbowe na NSSF is not an issue? kwanini linasumbua watu sasa miaka 18? kwani ni watu wapoteze muda kama hakuna issue?
Hakuna anayebisha kwamba makosa yanatofautiana kwa ukubwa na effect yake. Lakini haina maana kwasababu kuna ufisadi basi watu wasijadili wanasiasa wanaokopa NSSF na kuwaacha wanyonge wanasota kwenye mabank. Msimamo wangu ni ule ule mikopo yote ya NSSF na NPF ina mazingira ya corruption na cronysm, ndio maana huwezi kukuta watu maskini wanakopa huko. Sasa kama unatofautiana na argument hiyo, toa mawazo yako na sio kuanza kuhoji kama watu wengine wameelemika.
Ukitaka tujadili mabo ya kuelemika na kutokuelemika, fungua thread nyingine. Huko ndiko onyesha jinsi ulivyoelemika ili na sisi tusioelemika tujifunze.