Mbowe ahusishwa na UFISADI wa kuimaliza NSSF

kwanza lazima uelewe kwamba neno Ngumbaro maana yake ni mtu mzima kwa hiyo tuliamua kuiita elimu ya Ngumbaro tukimaanisha elimu ya watu wazima.

kwangu mimi kuna tofauti kati ya kusoma na kuelimika,kusoma kunahusiana na mitihani wakati elimu inahusiana na uwezo wa kupambana na mazingira yako na jinsi unavyopambana na matatizo yanayokukabili kwa wakati.

kwa mfano msomi anaweza kujua 2+2=4 lakini akashindwa kujua kama kura mbili ukijumlisha na kura mbili nyingine zinapatikana kura nne zitakazowesha kuondoa utawala usiojali maslahi ya taifa madarakani. mantiki yangu hapa unaweza kuwa msomi wa sheria lakini usiwe na elimu ya sheria na wakati huo huo unaweza kuwa na elimu ya sheria lakini usiwe msomi wa sheria!

ingawa kuna mahusiano ya karibu sana kati ya kusoma na kuelimika lakini pia kuna ukweli usiokanika kwamba kuna wasomi wengi tuu lakini matendo yao yanawaonyesha kwamba hawajaelimika.

kuhusu Mbowe na NSSF hata mtu mwenye kiwango kidogo sana cha elimu na uelewa anaweza kabisa kutambua tofauti iliyopo kati ya Mbowe aliyekopa kihalali na anayepigania haki yake mahakamani na wale mafisadi waliotumia ofisi za umma na madaraka tuliyowapa kujitajirisha kiharamu

Kigarama,

Ushauri wa bure, jiepushe na mijadala ya nani ni msomi na nani sio msomi. Unachofanya ni sawa na kumnyoshea mtu kidole kwamba mjinga yule na kusahau kwamba kuna vidole vitatu vimeelekezwa kwako na vinakuambia na wewe je? Mbona mjinga zaidi ya huyo unayemsema?

Diversity haiko tu kwenye maumbo ya watu au rangi peke yake, bali iko hata katika
jinsi wanavyofikiri. Kuwa na mawazo tofauti juu ya jambo haina maana nani kasoma au kaelemika na nani hajaelemika.

Kuelemika kwa binadamu kunaonekana sio katika hoja bali katika uwezo wa kupambana na mazingira yanayokuzunguka.

Inaniwia vigumu hapa JF kuamini kwamba hao wanaojiita wameelemika, hawezi kujadili hoja bila lugha za kashfa, kama huko ndiko kuelemika, basi tunaishi kwenye dunia tofauti.

Kama suala la Mbowe na NSSF is not an issue? kwanini linasumbua watu sasa miaka 18? kwani ni watu wapoteze muda kama hakuna issue?

Hakuna anayebisha kwamba makosa yanatofautiana kwa ukubwa na effect yake. Lakini haina maana kwasababu kuna ufisadi basi watu wasijadili wanasiasa wanaokopa NSSF na kuwaacha wanyonge wanasota kwenye mabank. Msimamo wangu ni ule ule mikopo yote ya NSSF na NPF ina mazingira ya corruption na cronysm, ndio maana huwezi kukuta watu maskini wanakopa huko. Sasa kama unatofautiana na argument hiyo, toa mawazo yako na sio kuanza kuhoji kama watu wengine wameelemika.

Ukitaka tujadili mabo ya kuelemika na kutokuelemika, fungua thread nyingine. Huko ndiko onyesha jinsi ulivyoelemika ili na sisi tusioelemika tujifunze.
 
Kigarama hili somo ndugu yangu!

Kuna mtu huko nyuma alitolea mfano kuwa mbona Aden Rage alifungwa kwa deni... lakini mtu huyo hajatokea leo na kutuhabarisha kuwa Mahakama Kuu imefutilia mbali hukumu ya mahakama ya chini na kumfutia adhabu yote kwani hatia aliyopatikana nayo haikuwa sawasawa na Hakimu hakuzingatia ushahidi uliotolewa.

Hii ndio sababu watu wanaenda mahakamani hadi hatua za mwisho za rufaa. Kwanini watu waone kuwa ati kwa vile Mbowe ni mwanasiasa basi alipe deni tu wakati ana kesi mahakamani iliyofunguliwa na NSSF? Kwanini tusiache mkondo wa sheria ufuate njia yake hadi mwisho na kama baada ya mchakato huo kuisha na Mbowe akakaidi amri ya mahakama basi sisi sote itabidi tumpigie kelele kuwa atii amri halali ya Mahakama?

Kwanini alipe deni tu ili kujijengea mazingira mazuri ya kisiasa hata kama deni hilo ni la kihuni?

Mwanakijiji,

Labda ujibu hili swali, je kwa wewe ni OK kwa wanasiasa na matajiri kukopa NSSF wakati members wengine wa hiyo mifuko hawawezi kukopa huko?

Refer hiyo article nyingine kwamba waliowahi kukopa NPF walikuwa Sumaye na gavana wa bank kuu pamoja na wafanyabiashara wachache, why?
 
Mimi nimeomba iundwe tume ya kuchunguza pesa na matumizi ya NSSF kuanzia mwaka 1990 lakini naona watu kimyaaaa... katika hili hakuna atakayejua ukweli kama NSSF wenyewe wanajichanganya kwenye press releases zao na kesi yao mahakani dhidi ya Mbowe.

Kuna mengi sana yalisemwa wakati skendo ya Manji na pesa za NSSF imeanza kuandikwa na Thisday. Serikali ya Kikwete iko kimya tuli katika hili na mwisho wa yote Kikwete amemteua Mkullo kuwa waziri wa fedha.

Uchunguzi huru ndio utamweka kila mtu huru au hatiani hapa - iwe Mbowe, Mkullo, Manji, ROstam Azizi, Sukita ya ccm, au Kikwete mwenyewe!
 
Swali la kuwa ni "Ok"? ni misleading in nature. Swali lingekuwa ni je wanasiasa, matajiri na wananchi wengine wana haki ya kukopa kutoka NSSF kwa mujibu wa taratibu na sheria zilizopo? Jibu langu ni "ndiyo" wote wana haki sawa.

Sasa, swali la pili ambalo ndilo unaloashiria ni kuwa "je kwanini wanasiasa na watu matajiri ndio wanaonekana kukopeshwa wakati wanachama na watu wa "kawaiwa" hawakopeshwi, ni sawa hilo"? Jibu ni hapana si sawa.

Lakini ni kosa kulaumu anayekopa badala ya kumlaumu anayekopesha. Kama wanaokopesha wana masharti yanayowapendelea matajiri (wawe wanasiasa au vinginevyo kwa sababu sidhani kama Katibu wa Tawi la chama cha kisiasa umemuweka kwenye kundi la "wanasiasa wanaokopeshwa).

Kama mfumo uliopo umetengenezwa kiasi kwamba watu wamatajiri (wawe wanasiasa au vinginevyo) ndio wameweza/wanaweza kukopa NSSF hilo siyo kosa la wale wanaoenda kukopa basi ni kosa la waliotengeneza mfumo huo. Kama tajiri (mbowe, sumaye, n.k) wameona kuwa kuwa wanaweza kukopa kwa kutumia sheria zilizopo na "loophole" kwanini liwe kosa lao kwenda kukopa?

Hivyo badala ya kumlaumu Mbowe kwa kukopa kihalali tulaumu waliomkopesha, kwani wasingetaka wangeweza kumzuia asikope. Ni kosa la mfumo siyo kosa la mkopaji yoyote yule.

Sasa anayekopa anazo haki fulani na haki mojawapo ni haki ya kwenda mahakamani au kutafuta ulinzi wa kisheria anapoona hatendewi haki (kama alivyofanya Rage) na siyo kukubali deni au madai yasiyo na msingi kwa vile tu yeye ni mwanasiasa au mtu tajiri basi alipe tu deni ili yaishe.

Kwanini hauko tayari kuona Mbowe anatafuta haki yake mahakamani badala ya kutaka alipe tu ili yaishe, asijiharibie kisiasa?
 
Mwafrika wa Kike,

Nakubaliana na wewe kwamba wote akina Makata, Mkullo, Sukita na wengine ni wahusika katika masuala ya NSSF na NPF.

Mimi simtetei mtu, toka mwanzoni nimesema hata huyo waziri wa fedha, wala hastahili kuwa hapo kwani madhambi yake kule NSSF ni mengi. Suala la Manji na NSSF tulishalijadili sana.

Sina uwezo wa kuunda tume zaidi ya kutoa maoni hapa JF. Naamini deals zote za NSSF na NPF ni dodgy, zikichunguzwa itaonekana tu corruption au cronysm imetumika.
 
Swali la kuwa ni "Ok"? ni misleading in nature. Swali lingekuwa ni je wanasiasa, matajiri na wananchi wengine wana haki ya kukopa kutoka NSSF kwa mujibu wa taratibu na sheria zilizopo? Jibu langu ni "ndiyo" wote wana haki sawa.

Sasa, swali la pili ambalo ndilo unaloashiria ni kuwa "je kwanini wanasiasa na watu matajiri ndio wanaonekana kukopeshwa wakati wanachama na watu wa "kawaiwa" hawakopeshwi, ni sawa hilo"? Jibu ni hapana si sawa.

Lakini ni kosa kulaumu anayekopa badala ya kumlaumu anayekopesha. Kama wanaokopesha wana masharti yanayowapendelea matajiri (wawe wanasiasa au vinginevyo kwa sababu sidhani kama Katibu wa Tawi la chama cha kisiasa umemuweka kwenye kundi la "wanasiasa wanaokopeshwa).

Kama mfumo uliopo umetengenezwa kiasi kwamba watu wamatajiri (wawe wanasiasa au vinginevyo) ndio wameweza/wanaweza kukopa NSSF hilo siyo kosa la wale wanaoenda kukopa basi ni kosa la waliotengeneza mfumo huo. Kama tajiri (mbowe, sumaye, n.k) wameona kuwa kuwa wanaweza kukopa kwa kutumia sheria zilizopo na "loophole" kwanini liwe kosa lao kwenda kukopa?

Hivyo badala ya kumlaumu Mbowe kwa kukopa kihalali tulaumu waliomkopesha, kwani wasingetaka wangeweza kumzuia asikope. Ni kosa la mfumo siyo kosa la mkopaji yoyote yule.

Sasa anayekopa anazo haki fulani na haki mojawapo ni haki ya kwenda mahakamani au kutafuta ulinzi wa kisheria anapoona hatendewi haki (kama alivyofanya Rage) na siyo kukubali deni au madai yasiyo na msingi kwa vile tu yeye ni mwanasiasa au mtu tajiri basi alipe tu deni ili yaishe.

Kwanini hauko tayari kuona Mbowe anatafuta haki yake mahakamani badala ya kutaka alipe tu ili yaishe, asijiharibie kisiasa?

Mwanakijiji,

Nyerere aliposema ni makosa kutoa na kupokea rushwa alikuwa na maana yake.

Kosa ni kwa pande zote na wala sio upande mmoja. Mikopo ya aina hiyo inaongozana na rushwa au favours za kisiasa. Ni makosa ya hiyo management ya NSSF au NPF lakini pia hao wanaotumia favours ili kupata hiyo mikopo.

Bila kushughulikia pande zote mbili, huwezi kutatua madhambi ya jamii. Utaishia kuwa kama Makamba, kuwaandama Changudoa na kuwaacha wanaonunua sex. Kama kitu hicho ni kosa basi wahusika wote wana makosa.
 
mzee mwenzangu salama uko leo? Naona umerundika mambo mengi sana toka mkopo hadi machangudoa!

Kosa la mtu kukopa ni nini? Na sasa naona umesogeza magoli zaidi na kuleta tuhuma za rushwa. Sikumbuki kama kwenye stori ya Rai walisema lolote kuhusu rushwa. Are you suggesting that Mbowe alihusika na rushwa ili kupata mkopo au you accusing him of the same?

Kama unaamini kuwa Mbowe alitoa rushwa ili apate mkopo basi unayo kesi ya "wote walaumiwe". Is that the case?
 
Nimesema mimi naamini mikopo yote ya NSSF na NPF ina mazingira ya corruption na cronysm. Hayo ni mawazo yangu wala sio mawazo ya RAI. Sijamtuhumu Mbowe au mtu mwingine yeyote.

Ndio maana toka mwanzo nimesema kwa mimi hata ile tu kukopa NSSF tayari kuna issue. Kama NSSF wanakopesha basi watutangazie ili na wengine tukakope. Hii ya kuitana pembeni ina mazingira ya rushwa.
 
Unahitaji qualifications zipi uweze kupata mkopo ? Naomba kujua ili nami nianze mapema kama Mlalahoi.
 
Mtanzania, suala la NSSF kukopesha halina mjadala kwani ushahidi upo kuwa wanakopesha. Sasa, kwa upande wako badala ya kutuhumu corruption na cronysm au "mazingira ya rushwa" bila kutuambia masharti ya ukopeshaji yalikuwaje n.k sidhani kama ni sahihi.

Sasa angalau nimekuelewa kuwa ni "mawazo" yako kwani yanaweza yasiangalie ukweli na hayako tayari kuangalia ukweli kwa sababu umeshaconclude kuwa kuna kuna "kuitana". Ninayaheshimu mawazo yako kwa sababu najua hata mimi kuna vitu ambavyo naweza ambavyo najua kabisa havina msingi katika ukweli.
 
Unahitaji qualifications zipi uweze kupata mkopo ? Naomba kujua ili nami nianze mapema kama Mlalahoi.

Lete michapo ya Butiama, hata mimi nasubiri hizo qualifications. Wengine tumesumbuliwa kweli na hayo mabank lakini kumbe wajanja wanachota tu.

Mkullo hafai hata kuwa waziri wa fedha.
 
Mwanakijiji,

Nimesema mimi naamini mikopo yote ya NSSF na NPF ina mazingira ya corruption na cronysm. Hayo ni mawazo yangu wala sio mawazo ya RAI. Sijamtuhumu Mbowe au mtu mwingine yeyote.

Ndio maana toka mwanzo nimesema kwa mimi hata ile tu kukopa NSSF tayari kuna issue. Kama NSSF wanakopesha basi watutangazie ili na wengine tukakope. Hii ya kuitana pembeni ina mazingira ya rushwa.

Mtanzania,

Ukianza masuala ya mikopo mbona utaenda mbali.
Mwambie mama Makongilori pale Tabata aende benki yoyote hapo bongo uone kama atapewa mkopo wa kuinua biashara yake ya genge la nyanya na nazi.

Mikopo ni issue na sio rahisi hata kwa hao wanaotangaza kuwa wanatoa mikopo! umesahau kilichotokea mikopo ya mabilioni ya Kikwete?
 
Lete michapo ya Butiama, hata mimi nasubiri hizo qualifications. Wengine tumesumbuliwa kweli na hayo mabank lakini kumbe wajanja wanachota tu.

Mkullo hafai hata kuwa waziri wa fedha.

Uzoefu wangu unaonyesha kuwa wafanyabiashara wana nafasi nzuri sana ya kupata mikopo kuliko watu wengine (hasa wafanyakazi - hata wale wa serikalini). Inaonekana benki zina strict collateral assessment system kuliko tunavyodhani.
 
MWK,

Nenda kajaribu ndio utajua. Kama hujuani nao pamoja na kuwa na collateral
kwa TZ bado ni tatizo.

Tena kwa siku hizi, wanakimbilia wafanyakazi kwasababu kuna quarantee
watapata pesa zao mwishoni mwa mwezi.

Sio lengo la hii thread lakini ukitaka zaidi nitumie PM.
 
Sasa na sisi tunaofanya kazi nje ya nchi tutapata mikopo wapi maana hakuna tunayemjua na hakuna namna ya kuchukua mishahara yetu?

Mambo mengine sihitaji hata kuanza rants zangu nisijeuzi watu bure ingawa bado naita kichwa cha Mkullo kwenye sahani (calling for Mkullo's head).

Tutawasiliana kimya kimya mkuu tusijeanika strategy zetu hapa bure na kina Jiitu Patel nao wakaanza kuzitumi wasivyokuwa na hiyana majambazi wale!
 
Hivi Mbowe hajalipa kweli deni lake ? Unaweza kusema Mbowe hajalipa hadi uje na misemo ?
 
wewe ni mtu mzima na unasoma magazeti, unataka kuniambia hujui kama anadaiwa au hadaiwi ? ebu cop ile makala ya mara ya mwisho halafu useme kama anadaiwa au la....hadi akasema anahitaji maongezi kwanza then ndio alipe..hukumbuki hapo ? Maswali mengine nafikiri itakuwa vizuri umuulize Mbowe au NSSF lakini tunachodjadili hapa ni deni kulipwa !
 
Bado Noma La Kuiba Magari Uk Nalo Litamfuata. Mzee Alikuwa Akiingiza Mavogue Ya Wizi.
 
Back
Top Bottom