Mbowe ahusishwa na UFISADI wa kuimaliza NSSF


Watanzania wanakopa kitapeli. Wanajua watacheza na mahakama zetu deni litapotea. Kwa nini fedha za WAFANYAKAZI wetu wa kawaida kabisa wafaidike wachache?
 
Katiba mpya inayokuja viongozi kama hawa ambao wameshindwa kuongoza kampuni mpaka imefilisika kwa kutokuwa wabunifu inabidi wasichaguliwe kuwa viongozi. Kama ameshindwa kuongoza kampuni ya watu 200 atawezaje kuongoza CHADEMA yenye watu milioni 2 ? Hii ina maana kuwa hata CHADEMA wanaongozwa na mtu asiye na upeo na wao vile vile wamefilisika kisiasa
 

Kweli makada mmeishiwa hoja....kampuni inapokwama kibiashara ni menejiment au wamiliki ndio wenye matata? SUKITA SI ILIKUFA MBONA MAPAKA LEO CCM ipo ofisini...grow up cadres
 
Watanzania wanakopa kitapeli. Wanajua watacheza na mahakama zetu deni litapotea. Kwa nini fedha za WAFANYAKAZI wetu wa kawaida kabisa wafaidike wachache?

Mkuu Deni la Mbowe Hotel Ltd si kubwa kihivyo!!!!! Ni kwa vile ni siri ya mkopaji na mkopeshaji but tungeliweka hapa. Kuna watu wamekopa NSSF mihela ya nguvu na hawawatiwi hadharani japo ni defaulters. Mbowe amewekwa hapa na magazetini kwa sababu ya kisiasa zaidi. Hebu Ramandhani Dau atoe hadharani transparent list ya defaulters na kiasi cha deni? Kama ni mwanaume anajiamini afanye hivyo!!! Kuna madudu NSSF!!!! Sikatai mkoppaji kulipa deni but nachukia pale ambako mdaiwa anatuhumiwa kwa sababu ya kisiasa zaidi. But Watanzania tumshaamka hatudanganyiki kabisa. Mbona mlileta habari za Slaa na Josephine na bado JK wenu akapigwa chali akaokolewa na UWT?
 
Kweli makada mmeishiwa hoja....kampuni inapokwama kibiashara ni menejiment au wamiliki ndio wenye matata? SUKITA SI ILIKUFA MBONA MAPAKA LEO CCM ipo ofisini...grow up cadres


Tena CCM imeua vingi.......SUKITA, Mradi wa mabasi ya wanafunzi (UVCCM), Ambassador Hotel pale Morocco iliwashinda mpaka wakauza jengo, Shule za jumuiya za wazazi wa CCM ziko hoi bin taaban....lakini kazi kufuatilia issue za Mbowe wakati wao CCM wanayo mengi na makubwa.

Naamini siku CCM ikitolewa madarakani yatafumuka mambo mengi sana ya ajabu jinsi walivyokuwa wakijichukulia hela ovyo ovyo ....kama yanavyojulikana sasa ya kina Ben Ali wa Tunisia. Na hii ndio sababu watafanya mbinu zote chafu kuhakikisha wanabaki madarakani.
 

Hakuna hata chembe ya siasa kwenye deni hili. Aliyetoa tangazo lile ni Receiver/Manager aliyeteuliwa na NSSF. Halafu, kulipa deni na hasa deni lenyewe linapokuwa ni fedha za UMMA na zimekopwa na KIONGOZI wa KITAIFA anayeongoza Watanzania wengi tu ni sehemu ya MAADILI mema tunayoyapigia kelele humu!
 
Naomba connection kati ya Mbowe Hotel Limited na Freeman Mbowe

Nijuavyo mimi hiyo hotel haikuwa ya Freeman bali ya baba yake aliyeitwa Mbowe na iko chini ya kampuni iitwayo Mbowe Hotels Ltd . Freeman anaweza akawa na shares na watu wengine wengi tu kwa hiyo kufilisiwa haina maana Mbowe kafilisiwa
 

Kwa kuwa CCM walifanya haya na Mbowe naye afanye hivo? Tofauti itakuwa ipi sasa! Combat na shati za kijani?
 
Kwa kuwa CCM walifanya haya na Mbowe naye afanye hivo? Tofauti itakuwa ipi sasa! Combat na shati za kijani?
Sikumaanisha hivyo ....wanachotakiwa kufanya ni kuweka siasa pembeni [level playing field to all] ....kama mtu anadaiwa adaiwe kwa haki na akishindwa afilisiwe. Unakumbuka mambo ya CIS(Commodity Import Support) tangu enzi za Mwinyi na ni zaidi ya TShs 180 billioni.....ni makada wangapi wa CCM wanadaiwa ROSTAM akiwemo mpaka leo hatujasikia hatua zozote ingawa walijifanya kuja na mkwara wakati fulani.
 
Hebu iondoeni CHADEMA kwenye mada hii. CHADEMA ni zaidi ya Mbowe sasa.

mkuu ukiwa muongo usiwe msahaulifu (kilaza)...............

umehitimisha bandiko kwa sentensi hii hapa chini:

"Tungemkabidhi Nchi mwaka 2005........!"

hivi 2005 Mbowe alikuwa anagombea kupitia chama gani?

una maana gani unaposema.............

"Hebu iondoeni CHADEMA kwenye mada hii"

jamani nyiee?

watu wa CCM bwana.

yaani mtu ukiwa CCM unakuwa kiburudisho kabisaaaaaaaaaaaa!
 
Taratibu za kimahakama zimefuatwa. Siasa hapa ni kitu gani? Mbowe ameniangusha.
 

Kwa hiyo kila anayetaja jina la Mbowe kwa mabaya yake ni CCM? Umakini alionao Mh Mbowe kwenye biashara na siasa hashindwi kulipa fedha hizi za walalahoi.
 
Mkuu wildcard nimeipenda hii, unaanzisha topic na unaisimamia vilivyo.
Hata hivyo humu jf kunawatu wanadhani viongozi wao ni malaika
 
mh inaonekana wengine hamjawahi kuuza hata karanga humu! nikupe quiz.unadhani wote wanaochukua mkopo hawana real cash ya kutekeleza jambo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…