Wasalaam waungwana,
Kwanza kabisa niseme wazi kwamba suala la Mbowe Hotel Limited kufilisiwa ni la kisiasa ndio maana nimeshawishika kuliweka jamvini ili wananchi waelewe.
Kwa muda mrefu hili suala limekuwa likiibuliwa na watu mbalimbali ili mradi wamchafue Mh. Freeman Mbowe mbele ya macho ya wananchi.
Ukweli wa jambo lenyewe uko hivi,
Mwaka 1990 Machi NSSF na Mbowe Hotel Limited waliingia kwenye mkataba wa Mkopo wa Shilingi Milioni 15. Mkopo huo ulikuwa unalipwa kwa kipindi cha miaka sita na nyumba iliyopo moshi iliwekwa rehani ya mkopo huo.
Hakukuwa na Personal Guarantee ya Wakurugenzi wa Mbowe Hotel wala mali nyingine yeyote iliyowekwa dhamana. Baada ya muda fedha hizo zilichelewa kutolewa kutokana na ukiritimba wa kudhibiti manunuzi ya fedha za kigeni. Wakati zinatoka project iliyokuwa inatakiwa kufanyika ikawa imekuwa twice expensive. NSSF wakaombwa waongeze kiwango cha mkopo wakakataa!! Kipindi hicho ndio siasa za mageuzi zimeanza!! Kwa kukomoa wakaamua kuudai mkopo ulipwe wote na kipindi chochote cha kuzozana wakaendelea kupile up interest.
Mbowe Hotel Limited wakalipa principal sum na interest waliyoona ni sahihi kwa kuamini suala hilo limeisha badala yake NSSF wakaenda mahakamani kimya kimya wakapata Exparte Order (Hukumu ya Upande Mmoja) na ndiyo wanayoitumia mpaka leo kudai interest ya mkopo ambao umeshalipwa!
Cha kushangaza walipooombwa watoe nakala ya hukumu hiyo wakakataa. Mpaka leo haijawahi kuonekana wala kutolewa! Badala yake wanatumia mbinu chafu ikiwa ni pamoja na kutishia kuwafungua wakurugenzi wa Mbowe Hotel Limited!
Riba inayosemekana kudaiwa ni sh Mil. 256+ mpaka sasa.
Suala la msingi ambalo NSSF wanaficha ukweli ni kwamba "security/dhamana pekee ya mkopo huo wa Mil. 15 ni nyumba yenye thamani ya shilingi Mil 70 iliyotolewa kama dhamana" na HAKUNA mali au kitu kingine chochote kilichotolewa kama dhamana!!
Kwa yeyote anayejua ni kwamba, mkataba wa mkopo kama mkataba mwingine ni makubaliano. Sasa kama NSSF walikubali kwamba dhamana ya nyumba itatosha kushikilia mkopo huo kulikoni sasa hivi wanataka kushika mali nyingine ambazo hazikuwahi kuwekwa kama dhamana? Mamlaka hayo na haki hizo wanatoa wapi?
Mh. Freeman Mbowe siku zote amekuwa mstari wa mbele kutaka kumaliza suala hili kwa haki na ustaarabu lakini NSSF wamekuwa wazito!! Na badala yake wanatumia mbinu chafu ili kumchafua!!
Sasa, unawezaje kumteua mtu awe receiver/manager wa Mbowe Hotel Limited badala ya kumteua awe receiver/manager wa property iliyowekwa kama dhamana??? hii ni akili ya sheria au matope??
Utaratibu umeshafanyika kuhakikisha umma unajua ukweli kuhusu hili suala kwa kutumia vyombo vya sheria i.e Mahakama. WanaJF na wale wote wenye mapenzi mema wataliangalia hili suala kwa jicho la haki badala ya ushabiki. Kwa wanao subiri wakiamini ni kashfa au anguko la Mh. Freeman Mbowe watakuwa wanakosea na watasubiri sana!!
Nawasilisha.