Of course, msingeweza kupost hapa!
(Majira)
MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Bw. Freeman Mbowe, amekiri kudaiwa fedha na Shirika la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), lakini akakana tuhuma kuwa mkopo aliochukua ndio unalifilisi shirika hilo.
(Kichwa cha habari cha mtanzania kilisema "Mbowe aifilisi NSSF")
Pia amesema Watanzania wanapaswa kufahamu kuwa kama NSSF itafilisika basi ni kutokana na mabilioni ya fedha yaliyokopwa na wakopaji wengine wanaotajwa na ripoti mbalimbali za kampuni hiyo ya umma, ambao hawajawahi kutajwa, kushitakiwa wala kukamatwa na ni makada wa CCM.
Bw. Mbowe alitoa kauli hiyo jana Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari kutoa ufafanuzi kuhusu deni analodaiwa na NSSF ambalo alilikopa mwaka 1990 kwa ajili ya upanuzi wa kampuni ya Mbowe Hotels Limited ya jijini, ambayo yeye ni mmoja wa wakurugenzi wake mkurugenzi mwingine akiwa ni Dkt. Lilian Mbowe ambaye ni mkewe.
"Naomba ifahamike, deni ambalo nadaiwa na NSSF haliwezi kulifisi shirika hilo, bali watu wanaoweza kulifilisi ni waliokopa mabilioni ya fedha na hawataki kurudisha. Wengi wamekopa katika mazingira ya kutatanisha na ukiwachunguza walio wengi ni makada wa CCM.
Watu wasiwe na shaka kwani dossier ya wana CCM waliokopa mabilioni na ambao hawajarudisha hadi sasa, wapo wanajulikana lakini gazeti la Mtanzania lisingewanyoshea vidole hao! Tutawasaidia.
Ndiyo maana aliyekuwa Waziri Mkuu wa Awamu ya Tatu, Bw. Frederick Sumaye, aliwahi kusema ukitaka biashara zako zinyooke, hamia CCM," alisema Bw. Mbowe.
Alisema kwa mujibu wa mchanganuo wa kitaalamu, deni la sasa linalodaiwa na NSSF kwa kampuni yake ya Mbowe Hotels Limited ambalo halihusiani na masuala ya siasa wala CHADEMA, ni sh. 43,169,227 ambazo zinatokana na riba ya mkopo aliochukua.
Alisema fedha hiyo ni kidogo kwa upande wake na si kwamba ameshindwa kulipa deni bali kinachotakiwa kwanza ni kufanyika kwa mazungumzo ambayo yatahakikisha haki inatendeka na hasa kwa upande wake na NSSF.
Akifafanua zaidi kuhusu deni hilo, Bw. Mbowe
alisema kimsingi anadaiwa sh. milioni 15 ambazo alikopa mwaka 1990 kwa ajili ya shughuli za biashara na kwamba ameshazilipa ila deni lililopo sasa linatokana na riba ya mkopo huo.
Bw. Mbowe alisema hadi Juni 30 mwaka jana, kampuni yake imeshalipa jumla ya sh. milioni 75.5 ambazo kimsingi ni takribani mara tano ya kiwango cha fedha kilichokopwa na kampuni yake.
Hata ningekuwa mimi nisingekurupuka kulipa! Unalipa vitu mara tano ya deni lenyewe? C'mmon be real! Mbowe usilipe hadi hawa jamaa wabadili msimamo wao na terms, hili ni deni la kihuni! Sisi wenyewe Tanzania tuliwaambia wafadhili, too bad hatuwezi kulipa madeni yenu hata mtunyonge! Kuna madeni hayalipiki!
Aliongeza kuwa kampuni ya Mbowe Hotels Limited tangu mwaka 1996 imekuwa na nia ya kulipa deni hilo kwa kuandika barua kwa NSSF kutaka kukutana na kujadili suala hilo, lakini hadi sasa NSSF bado haijajibu barua hizo hivyo yeye na kampuni si kikwazo cha kulipa deni hilo, bali kikwazo ni NSSF yenyewe ambayo haitaki wakae na kuzungumzia suala hilo.
"Katika maisha ya biashara halali na ujasiriamali, kukopa ni jambo la kawaida. Utaratibu wa kupitia upya na kutathmini mikataba nalo ni jambo la kawaida kwa kila taasisi ya fedha inayojua wajibu wake na yenye nia njema. Mazingira ya biashara wakati wa michanganuo ya biashara hutofautiana kwa kiasi kikubwa na hali halisi hasa kutokana na udhaifu wa uchumi wetu hususan mfumuko wa bei," alisema Bw. Mbowe.
Si mpaka wakubali!
Aliongeza kuwa katika maisha yake ya biashara na uwekezaji kwa kupitia kampuni mbalimbali, aliwahi kukopa kwenye benki kadhaa kwa miradi inayotoa ajira kwa Watanzania wengi na kote huko amerejesha mikopo yote na hivyo alisisitiza kuwa ataendelea kukopa kwani ni njia muafaka kwake kujisaidia kimaisha.
Alisema mkataba wake na NSSF wa mwaka 1990 uligubikwa na mizengwe, kwani mwaka mmoja baada ya mkataba huo kusainiwa, aliomba kuongeza mkopo kwa ajili ya kukamilisha mradi lakini alikataliwa.
Bw. Mbowe alisema ataendelea kusimama katika haki hadi mwisho na yuko tayari kutumia gharama kubwa kuliko deni analodaiwa kuona uamuzi wa mwisho unakuwa wa usawa na haki.
Alisema kitu ambacho anakiona kwa sasa ni kuchafuliwa jina lake na chama chake kutokana na jitihada zao za kupambana na ufisadi katika maeneo mbalimbali ukiwamo wa EPA na Richmond.
Alisema pamoja na kuchafuliwa, bado atasimama imara kutetea maslahi ya Watanzania wote kwa kuhakikisha ufisadi unakwisha na yeye akiwa Mwenyekiti wa CHADEMA atahakikisha siku zote anapinga ufisadi.
Kuhusu Mwenyekiti wa Chama cha Sauti ya Umma (SAU), Bw. Paul Kyara, kuilingia suala hilo alisema inawekezana kuna watu wanamtumia katika kulichafua jina lake na inawezekana hajui mlolongo mzima wa tukio hilo.
"Sitaki kuwa msemaji wa Kyara, lakini picha ninayoipata hapa ni kwamba anatumiwa na watu kwa ajili ya kuharibu jina langu na chama changu.
"Kyara amekuwa akifuatilia chama chetu katika mambo mbalimbali hata uchaguzi mdogo uliofanyika Kiteto hivi karibuni, kumtafuta mbunge wa jimbo hilo baada ya CHADEMA kusimamisha mgombea naye alisimamisha wake kwa lengo la kutupinga, hivyo unaweza kuona ni mtu wa aina gani," alisema Bw.Mbowe.
Naye Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Bw. Zitto Kabwe, alisema kuwa pamoja na kuwepo kwa matatizo hayo, bado viongozi wote wa chama hicho wataendelea kumuunga mkono ili kuona haki inatendeka.
Pia alisema hayo yote ni katika kurudisha nyuma jitihada za kupambana na ufisadi, lakini wao wataendelea kuwa na msimamo wa kupambana na mafisadi wote na wananchi wawaunge mkono katika hilo.