Mbowe ahusishwa na UFISADI wa kuimaliza NSSF

Mbowe ahusishwa na UFISADI wa kuimaliza NSSF

Kwa maoni yangu fedha za NSSF ni fedha za wananchi/ wafanyakazi masikini ambao wamewekeza kwa lengo la kujiwekea akiba ili kukabiliana na matatizo ya umasikini. Hata hivyo, mwanasiasa huyu machachali ambae amekuwa akikemea ufisadi hapa nchini kwa nguvu zote, tayari ameshakuwa fisadi mkubwa wa fedha za wananchi masikini hata kabla ya kuingia Ikulu. Aidha, kama kweli ni mwanasiasa anayejali masilahi ya nchi na watu wake anapaswa kuzirejesha pesa anazodaiwa, halikadhalika, kwa kuchelewa kulipa fedha kwa muda huo hajawatendea haki wananchi ambao amekuwa akiomba kura kwao za kumfikisha Ikulu.
Pamoja na madai yake kwamba siyo yeye anayehusika na deni hilo bali ni kampuni yake ukweli unabaki kwamba kampuni hiyo ni mali yake Freemon Mbowe na Wakurugenzi wenzake akiwemo Dr Lilian Mtei Mbowe ambaye ni mke wake. Je Mbowe anaweza kujivua kutoka katika kashifa hiyo?
 
Ni nini kinawafanya washindwe kumfilisi?
Amekopa ameshindwa kulipa, solution nikuifilisi Bilicanas!
Hapo shida ipo wapi?
Hii kitu imeachwa iendelee kuelea lea iwe mtaji wa kisiasa?
 
Hello,
Ninaamin if every one of us genuinely turns to truths,transparency and walking the talk - Tanzania will be a best place to live and celebrating unbleavable successess,so Mboye has to answer the shutuma before the crowd au mnaonaje?
 
Heshima Mbele,

Mbowe aifilisi NSSF

[FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif]*Adaiwa milioni 1200, hataki kulipa
*Atumia sheria kukwepa asifungwe
*Adai iliyokopa ni kampuni si yeye

na mwandishi wetu

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, anakalia kiasi kikubwa cha fedha za Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), kwa kukataa kulipa deni alilokopa.

Mbowe anadaiwa wastani wa sh milioni 1200 (sh bilioni 1.2), kutokana na deni alilochukua mwaka 1990 kwa nia ya kufanya upanuzi wa Mbowe Hotel ya jijini Dar es Salaam, maarufu kama Bilcanas.

Kwa kutumia mamilioni aliyokopa kutoka NSSF Machi 10, mwaka 1990, Mbowe aliweza kupanua Mbowe Hotel kwa kujenga mgahawa wa Hard Rock, kumbi za Bilcanas, Much More na Sugar Mama, ambazo amekuwa azitumia kwa ajili ya biashara tangu wakati huo.

Kumbukumbu zilizopo zinaonyesha kuwa deni la mkopo huo aliouchukua kwa kutiliana saini kati yake na Shirika la Hifadhi ya Jamii (NPF), ambalo baadaye lilibadilishwa jina na kuwa NSSF, sasa limekua na kufikia zaidi ya sh milioni 1200. Deni hili linatokana na mkopo aliouchukua na riba inayotokana na deni hilo.

Wakati wa kuchukua mkopo huo NPF (wakati huo) iliwakilishwa na Mustafa Mkulo, aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo, huku Mbowe Hotel ikiwakilishwa Mbowe mwenyewe aliyetia saini. Pande zote mbili zilikuwa na mwakilishi mmoja. Mkulo kwa sasa ndiye Waziri wa Fedha.

Kwa mujibu wa mkataba wa mkopo kati ya Mbowe na NSSF, ambayo ilichukua majukumu ya NPF, Mbowe Hotel ilikopeshwa sh milioni 15, mwaka 1990. Ibara ya 5, ya Mkataba wa Mkopo kati ya Mbowe Hotel na NSSF yenye vifungu 5.01, 5.02 na 5.03, iliweka bayana kuwa riba ya mkopo huo ilikuwa asilimia 31, na kwamba kila mwaka iwapo riba isingelipwa kwa wakati nayo ingetozwa riba ya asilimia 31.

Kifungu cha 6.01 na 6.02 cha mkataba wa mkopo huo kati ya Mbowe na NSSF vinaeleza kuwa Mbowe Hotel ilitakiwa kulipa deni hilo kwa mikupuo sawa mitano katika kipindi cha miaka sita. Mwaka wa kwanza wa mkopo Mbowe Hotel haikutakiwa kulipa kitu kwa nia ya kuipa fursa ya kujiimarisha katika biashara kwa mwaka wa kwanza.

Malipo hayo yalipaswa kufanyika kila ifikapo Desemba 31, kuanzia mwaka 1991, ambapo kila mwezi alistahili kulipa sh 3,000,000 kama deni la msingi na riba ya asilimia 31 kama ilivyokubaliwa kwenye mkataba.

Wakurugenzi wa Mbowe Hotel, Manase A. Mbowe, Freeman Aikaeli Mbowe na Dk. Lilian Mtei Mbowe, kwa sababu wanazozijua wao waliamua kuacha kulipa deni hilo bila mawasiliano ya aina yoyote na NSSF wala juhudi za wazi za kuonyesha nia ya kulipa hadi mwaka 1993, walipoamua kulipa sh 3,000,000 kati ya deni lote.

Kwa mujibu wa mkataba wa mkopo, hadi mwaka 1993, wakurugenzi hao walistahili kuwa wamelipa wastani wa sh milioni 9,000,000 katika deni la msingi, lakini walikaa kimya hali iliyolitia wasiwasi shirika la NSSF.

Baada ya kutoa malipo ya sh 3,000,000, wakurugenzi hao walikaa kimya na ilipofika Septemba 1996, NSSF iliamua kufungua kesi Mahakama Kuu. Kesi hiyo ya madai No. 277 ya mwaka 1996, ilikuwa ikidai Mkopaji alipe deni la msingi sh milioni 12 zilizokuwa zimesalia pamoja na riba.

Hatua hii iliwafanya wakurugenzi wa Mbowe Hotel kuomba suala hilo walimalize nje ya Mahakama. Hata hivyo, hawakuendelea kulipa hadi mwaka 1998, walipopewa tishio la kufungwa jela ndipo waliamua kulipa kwa mkupuo sh milioni 12.

Hadi wanatoa malipo hayo, deni lilikwishakuwa na kufikia wastani wa sh milioni 145.38, na kimsingi makubaliano ilikuwa ni kwamba deni hilo lingelipwa katika muda wa miezi 24 tangua tarehe ya makubaliano.

Hata hivyo, Mbowe na wakurugenzi wenzake waliamua kutoendelea kulipa deni hilo badala yake wakaamua nao kuchukua mkondo wa kisheria kwa kutumia wahasibu kukokotoa tena hesabu za riba, bila mawasilianao na NSSF, na kisha wakachagua kiasi wanachotaka kulipa wao.

Mbowe Hotel ikitumia kampuni ya uwakili ya Nyange, Ringia & Co., walifanya kazi ya kuwasiliana na wahasibu mbalimbali kisha kuwasiliana moja kwa moja na wakili wa NSSF, Ademba Gomba, kutaka deni la riba lipunguzwe.

Mgogoro na mvutano kati ya Mbowe Hotel uliendelea, huku riba ya deni nayo ikizidi kuongezeka na ilipofika Oktoba 11, 2002 Meneja wa Fedha wa Bilcanas Group Inc, Godbless Naftal, kupitia barua yake yenye Kumb. No. BGI/NSSF/MHL02/02/01, alikokotoa hesabu na kutaka wakurugenzi wa Mbowe Hotel walipe wastani wa sh 31,959,369.86, kwa maelezo kuwa kanuni iliyotumiwa kukokotoa riba ilikosewa.

Januari 16, 2003 NSSF kupitia kwa Mussa S. A. kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu, alimjibu Naftal kwa barua yenye Kumb. No. NSSF/LA/F.131/10/89/135, akimweleza kuwa NSSF imekataa mapendekezo yake (Naftal) na hivyo wanapaswa kulipa deni lote kwa mujibu wa hukumu ya za Mahakama Kuu za mwaka 1999 na 2001.

NSSF na Mbowe Hotel waliendelea kupigana ngwala mahakamani na kwenye bodi za usuluhishi hadi ilipofika Oktoba, 2006 ambapo Jaji Manento alihukumu wakurugenzi wa Mbowe Hotel watiwe mbaroni na kufungwa jela kwa kushindwa kutekeleza amri ya mahakama ya kulipa deni lao.

Wakili wa Mbowe Hotel, Herbert Nyange, aliwasilisha katika Mahakama ya Rufaa hati ya kiapo ambayo muhuri wake umegonjwa Oktoba 30, 2006 akipinga wakurugenzi wa Mbowe Hotel kukamatwa kwa maelezo kuwa Mahakama Kuu ilikwenda nje ya mipaka kisheria kwa kutaka wakurugenzi wakamatwe.

“Uamuzi wa amri ya kukamatwa kwa walalamikaji (wakurugenzi wa Mbowe Hotel) ulifikiwa kwa misingi ya wazi ya uvunjaji wa kanuni juu ya wajibu wa wakurugenzi dhidi ya deni au uamuzi dhidi ya shirika, hivyo ni kinyume na sheria,” alisema Nyange katika barua hiyo ya kupingwa kukamatwa kwa akina Mbowe.

Hata hivyo, kutokana na Mbowe kuona mambo yanaendelea kuchacha, Desemba 14, mwaka 2006, mmoja wa wakurugenzi wa Mbowe Hotel, Dk. Lilian Mtei Mbowe, aliamua kutoa malipo ya wastani wa sh milioni 50 kwa NSSF kwa hundi mba 298492, iliyoambatana na barua yenye Kumb. No. BGI/NSSF/MHL06/01, huku akitaka warejee kwenye meza ya majadiliano badala ya kufungwa jela.

Barua hiyo pia iliomba NSSF irejee barua ya Kampuni ya Ushauri wa Fedha ya Morgan cKlien Associates iliyoteuliwa na Mbowe mwaka 2004 kushiriki majadiliano na usuluhishi juu ya jinsi ya kulipa deni hilo.

Kampuni hiyo iliyokuwa chini ya Afisa Mtendaji Mkuu, Hubert Mengi, ilitoa maelezo mengi yenye kuonyesha kwa nini Mbowe Hotel ilishindwa kulipa deni lake kwa wakati. Anasema katiak moja ya vielelezo kuwa fedha zilipotolewa na NSSF mwaka 1990, nchini Tanzania hakukuwapo vifaa vya ujenzi.Mengi anaeleza kuwa Mbowe Hotel walilazimika kuagiza vifaa vya ujenzi kutoka nje ya nchi, na lilijitokeza tatizo lingine kwamba benki nchini hazikuwa na fedha za kigeni, hivyo Mbowe Hotel ililazimika kusubiri kwa muda mrefu kupatiwa fedha hizo za kigeni.

Kwa maelezo hayo, anasema Mbowe Hotel walichelewa kupata vifaa na mradi ukashindwa kukamilika kwa wakati hali iliyosababisha wakurugenzi wake washindwe kulipa deni hilo kwani walikuwa hawafanyi biashara.

Baada ya mivutano yote hiyo, Mbowe Hotel wamealikwa kwenye NSSF kujadili jinsi ya kulipa deni hilo linaloendelea kukua lakini hadi jana vyanzo vyetu kutoka NSSF vilionyesha kuwa wakurugenzi wa Mbowe Hotel wameamua kukaa kimya.

Kutokana na hali hiyo, ni wazi NSSF inaendelea kupoteza mapato yake yanayokaliwa na wakopaji wa aina hiyo, ambapo mwenendo usipodhibitiwa shirika linaweza kufilisika sawa na ilivyotokea kwa mashirika mengi nchini
[/FONT]​

Kwa kumbukumbu zangu huyu jamaa alisoma UK huku alishaanza kujihusishana mambo ya kihuni muda mrefu. Lakini anakipaji cha kutoa mambo ya ukweli na maendeleo ya taifa hili. Huu uhuni nadhani ni hula yake. Tuu?
 
AEIOU,
huu sio uhuni ni ubatilifu wa fedha za umma in other words ni kama sakata la RICHMOND how do we call kile kilichotokea......
not Hujuma ni UFISADI kwasababu jamaa is a PUBLIC FIGURE
 
Nafikiri huyu jamaa RA baada ya kuumbuka sasa anatumia vyombo vyake vya habari(RAI) kuwalipua wenzake.
Sijaona kosa lolote kwani kesi iko mahakamani na jamaa MBOWE analipa hizo fedha
Mbona hao jamaa waliokula hela za BOT wanazirudisha na hata hawajashtakiwa?
 
AEIOU,
huu sio uhuni ni ubatilifu wa fedha za umma in other words ni kama sakata la RICHMOND how do we call kile kilichotokea......
not Hujuma ni UFISADI kwasababu jamaa is a PUBLIC FIGURE

Kwa nini nyie watu hamuelewi kabisa defn ya Ufisadi, ubadhilifu etc Hivi huu jamaa hiyo fedha ameiba au ailokopa? kama alikopa amekataa hilo deni lake halali? Je, NSSF wanarusiwa kukopesha na sheria iliyounda taasisi hiyo? Je, huko mahakamani hukumu ilisha tolewa na iko vipi?

Jiulizeni maswali mengi ndipo mchangie hapa sio kuleta tu umbea na maneno yasiyo eleweka!
 
Mimi napenda kupongeza NSSF kwa kusimamia bila uoga suala la wakopaji ambao hawataki kulipa madeni hayo na kuchangia hali duni ya maisha inaowaandama watanzania. Sasa kwa vile tunajua Sukita na wengine wengi nao walikopa itakuwa vyema kama wakiendeleza moyo huo huo wakishujaa kuelezea umma kama hawa WOTE walilipa deni lao na kama sivyo, ni hatua gani zilichukuliwa dhidi yao? Nimesoma mahali kuwa kuna waliokopa Sh milioni 240 mwaka 1995, naomba mungu kuwa wawe wamelipa maana kutokana na hizi hesabu za hawa mashujaa ( milioni 15 hadi bilioni 1.2) sijui hilo deni litakuwa limefikia kiasi gani hivi leo!

Amandla!
 
Kwa nini nyie watu hamuelewi kabisa defn ya Ufisadi, ubadhilifu etc Hivi huu jamaa hiyo fedha ameiba au ailokopa? kama alikopa amekataa hilo deni lake halali? Je, NSSF wanarusiwa kukopesha na sheria iliyounda taasisi hiyo? Je, huko mahakamani hukumu ilisha tolewa na iko vipi?

Jiulizeni maswali mengi ndipo mchangie hapa sio kuleta tu umbea na maneno yasiyo eleweka!

Safi. Tatizo ni uelewa pia. Wana JF wanajua kuchambua mambo kwa staili iliyo sahihi lakini kwa hapa wengi mmechemsha, hasa hao walioingia jana.

Tatizo lingine hapa ni vyombo vyetu kama NSSF kuingilia kazi za wengine .Kwani wao ni Financial institution?
kwani sisi wanachama tulishawapa mandate ya kupesha fedha zetu?
Hata kama wameona ni sawa kukopesha je masharti na taratibu za kukopesha wanazijua?

Mimi nahisi pia hawakuwa na rehani ,collateral, ndio maana wameshindwa kuatach mali. halafu wanashindwa kujastify 15m for 1.2 bil.wakati kesi iko mahakama kuu. Mwenye huo makataba aumwage hapa tuuchambue kwanza.

Eleweni mtu kushindwa kulipa deni sio ufisadi ,wizi ,wala ubadhirifu. Ni biashara tu. Mbona wengi tu wanshindwa kurudisha mikopo kuanzaia Pride hadi NMB? Naho ni mafisadi?

Nasema NSSF wafuate taratibu za kibiashara kujipatia hizo hela na sio kumchafua Mbowe hapa JF.
 
Hivi,kukopa pesa na kushindwa kulipa ni ufisadi? mmh sasa naona hii maana ya ufisadi siku hizi ni pana sana kiasi haina limit,sasa napata hoja kuwa huenda hata kupigana na mtu ni ufisadi,kuchelewa kazini ni ufisadi,daladala kukatisha ruti nao ni ufisadi,hata kuendesha kwa spidi kali ni ufisadi.

Hainiingii akilini kama kweli kila kila kuwa ufisadi,unajua mie hata suala la manji na NSSF nilitofautiana na watu wengi sana akiwemo mengi kumshambulia manji.Jamani sheria ya mikataba ipo wazi,ni arrangement kati ya watu wawili,bila kujalisha subject matter ni nini,maadamu nssf walikuwa na mandate ya kukopesha pesa basi walikuwa na mkataba binafsi kati ya nssf na mbowe.Sisi hapa kama mbowe amedafult kulipa tunaotakiwa kuwalaumu ni nssf kwa kushindwa kumfatilia alipe na kushindwa kutumia good practice of lending ili kuweza kujua wanayemkopesha ni nani na je ana uwezo wa kulipa?Suala la mbowe hapa kushindwa kulipa halina loote linalohusiana na ufisadi,labda kwa sasa kwa kuwa yeye ni public figure anachopaswa ni konesha mfano kulipa hilo deni kitu ambacho ni moral au political responsibility tu.Kwa ufupi kinahusiana na maadili zaidi kuliko sheria zinazohusiana na ufisadi.

Vivyo hata katika lile suala la manji na nssf kuwa alikopa hela kwao halafu akajenga majengo akawauzia kwa gharama kubwa huo ni ujanja tu wa kibiashara unaoonesha pia uozo au uzubavu ulioko nssf.Kwani sheria ya mikataba iko wazi kwamba "consideration need not be adequate" kwa maana ya kwamba hata gari la TZS 15,000/- bado unaweza kuliuza kwa TZS 100,000 ili mradi hukulazimishwa au kushurutishwa na mtu yeyote na wakati unafanya hivyo ulikuwa na akili timamu.Hivyo iwapo nssf walifanya hivyo wakiwa na akili timamu(sound mind),pasipo shuruti(undue influence) wala vitisho(coercion) basi mkataba uwe kati ya manji na wao au mbowe na wao ni halali.Ila sisi kama wanajf hii sasa ni nafasi yetu kuchunguza pale nssf tua watu wa aina gani ambao wanatuingiza hasara kwa kutupotezea mapesa yetu mengi.To fight mbowe or manji is to fight a wrong enemy,our real enemy is NSSF.
 
Hili jambo liko mahakamani ni vema tukaiachia mahakama itoe mamuzi yake ingawa hilo kuliko sisi kuchangia jambo hili katika mitazamo ya kiitikadi labda katika upande mwingine twende mbali zaidi Asilimia 31 ni riba gani kubwa namna hii? huu ni wizi hata hao NSSF nao waliangalie hili! kakopa 15m karudisha 3+12+50=65m na bado anadaiwa 1.2bn Duu! Jamani! hii kiboko.

Haya Mhesh. Mbowe jitetee utetezi wako wa kwanza haujatukolea lete utetezi wenye mvuto. Pia limalize hili maana linachafua jina.
 
Hivi ni Mbowe peke yake anayedaiwa na NSSF? Au ni peke yake anayefanya ubishi kulipa deni lake? In all fairness ingekuwa vyema basi orodha ya wale wote wanaodaiwa na NSSF ingewekwa wazi kama ilivyofanywa hili la Mbowe. Whats good for the gander.......!
 
Hili jambo liko mahakamani ni vema tukaiachia mahakama itoe mamuzi yake ingawa hilo kuliko sisi kuchangia jambo hili katika mitazamo ya kiitikadi labda katika upande mwingine twende mbali zaidi Asilimia 31 ni riba gani kubwa namna hii? huu ni wizi hata hao NSSF nao waliangalie hili! kakopa 15m karudisha 3+12+50=65m na bado anadaiwa 1.2bn Duu! Jamani! hii kiboko.

Haya Mhesh. Mbowe jitetee utetezi wako wa kwanza haujatukolea lete utetezi wenye mvuto. Pia limalize hili maana linachafua jina.

aje kufanya nini wakati kuna watu kawaajili hapa 24 hours. maana mwanakijiji amekuwa hana mapumziko ni kama mfanyakazi wa ndani. ndio utaona anaingia na MWAFRIKA WA KIKE, KOBA, MADELA NA SASA ANAKUJA NA BEN.

NA UPANDE WA PILI KUNA KITILA ANAKUJA NA ASHA ABDALLAH NA FUNDI MCHUNDO HUU NDIO UNAFIKI ALIKUWA NA PEN NAME LA MWANASIASA AKAJIFANYA KUJA LIVE NA KITILA MKUMBO LAKINI SASA ANAKUJA NA KANZU YA FUNDI MCHUNDO NA WAKATI MWINGINE ANAVAA BAZEE(ASHA ABDALLAH) HUKO NI KUJIDANGANYA .

KWA MTAJI HUO AJE KUFANYA NINI MBOWE? VIBARUA WANAMWAGA ZEGE.
 
Dawa ya deni ni kulipa! Sasa kama Mbowe alikopa alipe! period!

NSSF refutes Mbowe loan loss reports
By Zephania Ubwani, Arusha

The National Social Security Fund has denied that it has lost billions of shillings through a loan extended to Mbowe Hotels Limited 18 years ago.

It confirmed, however, that it has a case in court against the firm owned by a top Opposition leader over unsettled debts. Mr Yacoub Kidula, the fund's director of planning, investments and projects told journalists that the row has been �unnecessarily politicized�. "This matter is in court.

Why don't we wait for the outcome of the case?" he asked, adding that it was not true NSSF had lost lots of money because of the loan. NSSF, then known as the National Provident Fund (NPF), extended a loan of Sh15 million to Mbowe Hotels Limited in 1990 for the expansion of its hotel in Dar es Salaam.

The loan was to be repayed over six years but that had not been the case until now, he said. Mr Kidula was reacting to media reports last week that Mbowe Hotels owed NSSF Sh1.2 billion.

"Reports that NSSF was bankrupt because of the loan are not true. What I know is that our case against Mbowe Hotels is still in court," he reiterated. Emphasising that the hotels firm does not owe NSSF Sh1.2 billion, he said the amount could be just a half of that figure or less, declining to specify the actual amount owed.

Legal experts at the fund headquarters were working on the matter which has been in court since 1996, he said.

A section of the media reported last week that NSSF was owed Sh1.2 billion by Mbowe Hotels Limited of Dar es Salaam in unpaid loans. The firm belongs to Mr Freeman Mbowe, the national chairman of Chadema, who contested the presidency in the 2005 General Election.

Other directors of the firm are Manase A.Mbowe and Dr Lilian Mtei Mbowe. The loan was to be used for refurbishment of the old Mbowe Hotels in the heart of Dar es Salaam, leading to setting up of Hard Rock Restaurant and Bilicanas Club

Source: The Citizen
 
Reports that NSSF was bankrupt because of the loan are not true. What I know is that our case against Mbowe Hotels is still in court," he reiterated. Emphasising that the hotels firm does not owe NSSF Sh1.2 billion, he said the amount could be just a half of that figure or less, declining to specify the actual amount owed.

Chinga uko wapi hapo?

Unaona hata mkurugenzi wa planning wa hiyo NSSF anasema kuwa Mbowe hadaiwi kiasi kikubwa namna hiyo na nyie wengine mlikaa hapa na kiulifanya la kisiasa na nakumbuka wiki iliyopita niliwaasa na kuwaambia kuwa hili kamwe haliwqezi kumfanya Mbowe na CHADEMA kukaa kimya dhidi ya mafisadi na ufisadi,

Balile na Ra8i you have to come out na kutuambia hiyo figure mliitoa wapi?

Mambo yanaendelea kuwa hadharani taratibu tuu kila kukicha.

CCM mnaendelea kumpa Mbowe media coverage ya bure kwa kusema uongo ambao mnajua kuwa siku akiujibu mtakuwa mmeangukia pua......

Niko namsubiria CHANGA abishane na huyo aliyetoa figure ya kuwa Mbowe anaweza kuwa hadaiwi kiasi hicho na yeye aseme kiasi hicho alikitoa wapi.....
 
NSSF refutes Mbowe loan loss reports
By Zephania Ubwani, Arusha
THE CITIZEN

The National Social Security Fund has denied that it has lost billions of shillings through a loan extended to Mbowe Hotels Limited 18 years ago.

It confirmed, however, that it has a case in court against the firm owned by a top Opposition leader over unsettled debts. Mr Yacoub Kidula, the fund's director of planning, investments and projects told journalists that the row has been unnecessarily politicized. "This matter is in court.

Why don't we wait for the outcome of the case?" he asked, adding that it was not true NSSF had lost lots of money because of the loan. NSSF, then known as the National Provident Fund (NPF), extended a loan of Sh15 million to Mbowe Hotels Limited in 1990 for the expansion of its hotel in Dar es Salaam.

The loan was to be repayed over six years but that had not been the case until now, he said. Mr Kidula was reacting to media reports last week that Mbowe Hotels owed NSSF Sh1.2 billion.

"Reports that NSSF was bankrupt because of the loan are not true. What I know is that our case against Mbowe Hotels is still in court," he reiterated. Emphasising that the hotels firm does not owe NSSF Sh1.2 billion, he said the amount could be just a half of that figure or less, declining to specify the actual amount owed.

Legal experts at the fund headquarters were working on the matter which has been in court since 1996, he said.

A section of the media reported last week that NSSF was owed Sh1.2 billion by Mbowe Hotels Limited of Dar es Salaam in unpaid loans. The firm belongs to Mr Freeman Mbowe, the national chairman of Chadema, who contested the presidency in the 2005 General Election.

Other directors of the firm are Manase A.Mbowe and Dr Lilian Mtei Mbowe. The loan was to be used for refurbishment of the old Mbowe Hotels in the heart of Dar es Salaam, leading to setting up of Hard Rock Restaurant and Bilicanas Club and Casino.
 
Yamekuwa haya tena ?
Haya wale wenye kuchonga mpo ?
 
KIDULA HASEMI UKWELI na kusema kuwa hii issue imekuwa politicised si kweli. Hivi kidula alitegemea nini wakati MBOWE ni mwanasiasa? Obviously watu waanza kuquestion links zikoje

in short kidula anaanza kubehave kama MUSTAFA MKULO na kusema ukweli i think its about time akaretire maana at most amekuwa mkorofi na wala si mtu wa kumsikiliza kwenye hili

again those are just my thoughts
 
NSSF refutes Mbowe loan loss reports
By Zephania Ubwani, Arusha
THE CITIZEN

The National Social Security Fund has denied that it has lost billions of shillings through a loan extended to Mbowe Hotels Limited 18 years ago.

It confirmed, however, that it has a case in court against the firm owned by a top Opposition leader over unsettled debts. Mr Yacoub Kidula, the fund's director of planning, investments and projects told journalists that the row has been unnecessarily politicized. "This matter is in court.

Why don't we wait for the outcome of the case?" he asked, adding that it was not true NSSF had lost lots of money because of the loan. NSSF, then known as the National Provident Fund (NPF), extended a loan of Sh15 million to Mbowe Hotels Limited in 1990 for the expansion of its hotel in Dar es Salaam.

The loan was to be repayed over six years but that had not been the case until now, he said. Mr Kidula was reacting to media reports last week that Mbowe Hotels owed NSSF Sh1.2 billion.

"Reports that NSSF was bankrupt because of the loan are not true. What I know is that our case against Mbowe Hotels is still in court," he reiterated. Emphasising that the hotels firm does not owe NSSF Sh1.2 billion, he said the amount could be just a half of that figure or less, declining to specify the actual amount owed.

Legal experts at the fund headquarters were working on the matter which has been in court since 1996, he said.

A section of the media reported last week that NSSF was owed Sh1.2 billion by Mbowe Hotels Limited of Dar es Salaam in unpaid loans. The firm belongs to Mr Freeman Mbowe, the national chairman of Chadema, who contested the presidency in the 2005 General Election.

Other directors of the firm are Manase A.Mbowe and Dr Lilian Mtei Mbowe. The loan was to be used for refurbishment of the old Mbowe Hotels in the heart of Dar es Salaam, leading to setting up of Hard Rock Restaurant and Bilicanas Club and Casino.

Hii story bado mbichi kabisa. Bado nasisitiza msimamo wangu wa kumchunguza Mkullo na wadosi wa NSSF katika hii story ya deni la Mbowe. Inabidi pia Mbowe aiombe mahakama impe ruhusa kuzungumzia hili swala nje ya mahakama ili kupambana na mbinu chafu za mwizi na mkoloni Rostam Azizi anayetumia magazeti yake kupindisha habari.

Hili saga ndio limeanza tu kwani hata JK mwenyewe itabidi aulizwe kuwa anajua nini kuhusu kuhusika kwa mapesa ya NSSF wakati ambao Mkullo alikuwa mdosi huko.

Hii story ya Mbowe na NSSF is the best connection so far ya JK na Mkullo.... na bado nasema kama nilivyosema mwanzo! Keep it coming .....
 
na zaidi ya yote hayo je tutaruhusiwa kujadili MBOWE na uhusiano wake na NSSF?

ama thread itahimishiwa kwenye hoja nzito na vibweka vya wakubwa
 
Back
Top Bottom