DUUH!!!
Wameshika kwenye kengele bwana MBOWE, hivi karibuni mkuu wa kanisa la Anglikana alisema kuwa "certain islamic laws must be accomodated akakazia kwa kusema sheria ya benki inayohusu riba ya kiislam inafaa kwa jamii yetu, ndoa na Divorce kwa kuwa hakuna mbadala katika sheria zingine.
Freeman Mbowe ni muhanga wa kauli ya archbishop Dr.Roman.
ilitakiwa kwa umoja wetu tutumie kesi ya Mbowe kuona athari za riba kubwa kwa wateja pale wanapokopa na si kumtetea "bwana mkubwa" kuwa hakuchukua nyingi.
JF kama tungekuwa makini hapa ilikuwa mwanzo wa kuwakomboa wanyonge wengine kama mimi, mwanakijiji,chinga n.k ambao tunapata riba kubwa kwenye mikopo. somo hili Professor Lipumba amekuwa akilitaja mara kwa mara.
lakini tumekalia kutetea mtu mmoja badala ya jamii nzima kama Mbowe anashindwa kulipa deni, inafika mahala mke wake anapelekwa mahakani na baba yake (Mzee Mtei) ni mtu mwenye heshima kwenye jamii, inakuwaje anapopatikana Kingwendu na mkopo wa benki?
hivi hamjawahi kuona nyumba zinapigwa mnada na inaandikwa kuwa kwa niaba ya mahakama nyumba kadhaa zitapigwa mnada siku ya jumapili na kampuni ya Majembe Auction Mart?
Miaka yote 18 kimewashinda nini kupiga mnada Billicanas
hatujiulizi inakuwaje hawa wanyonge waliokopa milioni moja au mbili inapelekea nyumba nzima kuchukuliwa? leo tunamtetea tu bwana Mbowe bila kutizama jambo hili kwa mapana na marefu.
well Mbowe atakingiwa kifua na pressure itatiwa kuwa sababu za kisiasa na asamehewe.
[COLOR="darkgreen"]Hatumkingii kifua tunasubiri maamuzi ya Mahakama[/COLOR]
swali kila anayedaiwa atumie kinga ya siasa? deni hili kalikopa kabla Chadema haijazaliwa wala vyama vingi.
Tukubali kuwa ni siasa zinatumika kumvuruga lakini alikopa kabla ya kuwa mwanasiasa na kama ni siasa deni hili lingetajwa 2005 wakati anagombea urais lakini hatukuona na huu si wakati wa kampeni za urais? au kuna kampeni za uchaguzi hivi sasa? kwa mujibu wa tume ya uchaguzi mimi sijasikia.
Chadema kama chama cha demokrasia kinaweza kumsimamisha Mwanakijiji au Chinga kwenye nafasi ya urais, lakini kujaribu kuibinafsisha nafasi ya urais kwa Mbowe tu ni kuiminya demokrasia kwa wengine.
Mbowe ni mwenyekiti wa chadema kwa kuchaguliwa hakupendekezwa wala kujipendekeza. uamuzi wa nani asimame kugombea urais ni chadema wenyewe, nijuavyo hauko juu ya mabega ya mtu mmoja ndani ya chadema
Jamani badilikeni tukitumia ujinga huu (uzezeta) itafika mahala hata jambazi ataingia upinzani na kuvamia mabenki akikamatwa tunasema siasa imetumika kumuharibu, Mahalu nae ni Chadema?
Nani unayemwita zezeta wakati uchambuzi wako ni wa kujikanyaga?
Mbowe kavamia Benki?
Sasa kama Mbowe kavamia Benki wale Maharamia walioiba EPA na sasa wanalindwa na Ameri Jeshi wa Majeshi ya Tanzania utawapa wasifu gani?
Hivi watu hawawezi kusema kuwa chepeo ni chepeo na si jembe?
Mbowe ni binadamu ana mapungufu yake vipi leo mnataka kumfanya malaika? na kibaya zaidi maisha yake hakujiandaa kama atakuja kuwa Mwanasiasa hivyo ana uchafu mwingi.
Naomba wataalam wa masuala ya benki waje hapa.kuna watu wengi hawatumii Credit Cards kwa kuogopa riba(Interest).
Milioni 15 ni fedha za umma na ni nyingi sana huhitaji kusoma Mzumbe University kulijua hilo.
$133,000,000,000 ni nyingi sana huhitaji elimu hata ya darasa la pili kujua kwamba ni udhaifu mkubwa kupigia kelele mkopo wa $15,000.00 na kuunyamazia wizi wa $133,000,000,000.00.
Labda tu wewe binafsi, baba yako, mama yako au mjomba wako ana hisa kwenye mgao wa fedha hizo.