mzee kuna makosa mawili katika swali lako:
a. Kwanza wakati Mbowe anakopa shirika alilokopa halikuwa NSSF ilikuwa ni NPF ambayo ilikuwa inaongozwa na sheria nyingine tofauti. Sheria ya wakati ule iliwezesha kukopesha na ndio maana Sukita, na vyombo vingine viliweza kukopa toka huko.
b. Kwa kuangalia website huwezi kuona yote ambayo NSSF inaweza kufanya kisheria. Hivyo nipendekeze uangalie sheria iliyounda shirika hilo ya mwaka 1997 Ibara ya 62.
Mwanakijiji,
Hii sio paper ya research ya kwenda kupatia Ph.D. NSSF inawakilisha yale yote ya kwake pamoja na ya shirika ambalo waliwarithi. Kwahiyo mtu akisema Mbowe alikopeshwa na NSSF yuko sawa kabisa na yule anayesema alikopeshwa na NPF. Labda kama ni thesis ambayo unatakiwa kila kitu kiwekwe wazi. Ni sawa na kuwaambia CCM wameongoza nchi miaka 40, wewe uanze kusema ni miaka 30 tu.
Kukopa kwa Sukita hakuna tofauti na kukopa kwa Sumaye. Mikopo yote hiyo ilijaa mizengwe ya kisiasa. Mmoja alikopa kwenye NPF wakati mwingine kwenye NSSF. Hakuna cha utofauti wa sheria wala nini. Ni mambo yale yale ya cronysm and corruption.
Suala la investment, NSSF wanafanya investments mbalimbali na ndio lengo lao hasa ili hiyo pesa ilipe. Lakini kikawaida hawakopeshi watu binafsi au mashirika binafsi. kama wangekuwa wanakopesha wangeweka wazi maana kukopesha wateja unahitaji kujitangaza na wala sio sawa na kujenga wenyewe nyumba na mkauza baadaye au mkapangisha ofisi.
Kama wanakopesha niambieni mimi niende nikawaone, je wana ofisi wapi inayokopesha?