Mbowe akiwa na vijana wake wa CHAUMMA

Hao waliofail hawakuwa ndani ya cdm. Yaani mifano yako imeshindwa kuonyesha cdm watakwama wapi.
 
Mnashangaza sana.Kupigwa na kusukumwa mpaka kuanguka ni assault. Wakati Sigrada anasukumwa ( kwa maelezo yako) alikuwa Chadema kindaki ndaki kwa hiyo unashangaa nini kwa polisi kutomsaidia. Tangu lini kunywa kumekuwa kosa la jinai? Sigrada angekuwa na nia ya kuiharibia Chadema angekimbilia polisi, sio baa. Aidha, Chadema walifanya nini waliposikia kuwa mwanachama wao yuko hospitali? Hata ingekuwa amelazwa kwa sababu nyingine na sio kupigwa, uungwana ilikuwa ni kwenda kumjulia hali hata kwa unafik.
Kwa akili yako tu ya kawaida, mtu apigwe mbele ya polisi wa CCM, wamwangalie tu, na wanavyotafuta upenyo wa kuwaonea CHADEMA, si wangeona wamepata sababu ya kuwatesa CHADEMA? Umewahi kumsikia yeyote ana kesi ya kumpiga sigrada?
Watafunguaje kesi kama victim hajatoa ushirikiano? Sigrada hakuwa na nia ya kuiharibia Chadema ndio maana alikaa kimya.
Sigrada na wenzake waliondoka Chadema bila shari kwa sababu tu waliona wazi kuwa uongozi mpya umewatenga na kutowatendea haki. Hata walipotoka, huwasikii wakitukana viongozi au chama chao cha zamani pamoja na kuwa Chadema na mashabiki wake wamekuwa wakifanya hivyo mara bila kukoma. Hata pale Heche alipotumia maneno ya ovyo dhidi ya Suzan Kiwanga hawakumjibu. Wakati wa kampeni za uchaguzi wagombea wake kama Catherine Ruge walifanyiwa fujo zaidi na mashabiki wa Chadema kuliko CCM.

Kwa upande mwingine haishangazi maana msimamo wa Chadema umekuwa mtu yeyote asiyekubaliana nao ni adui hata kama nae ni mpinzani. Msimamo huu hauna afya kwa chama chenu.

Amandla...
 
Katika ujinga unaowatafuna wapinzani wengi kama wewe ni kuweka matumaini yao yote kwa wanasiasa.. miaka michache iliyopita ni nyie mlikuwa mnasema "MWAMBA TUVUSHE".. Leo hii mnamtukana.
Umejuwaje kuwa mimi ni "mpinzani"; na ni wapi nilipoeleza "kuweka matumaini yangu yote kwa wanasiasa"; huoni kuwa unajiandikia tu vitu usivyojijuwa?

Wewe huo "ujanja" wa kujuwa "ujinga unawatafuna wapinzani" umeusomea shule gani na sasa kujiona ni mtaalam wa mambo hayo?

Hao waliokuwa wanaimba "MWAMBA TUVUSHE" umeongea nao wakakueleza maana yao ilikuwa inalenga jambo gani? Kama huyo "MWAMBA" wakati huo alionekana mambo aliyokuwa akifanya yalileta matumaini kwa hao waliokuwa wakimtungia hizo nyimbo; kwa nini wewe leo uhoji uelewa wa watu hao, unaowaita wewe "wajinga", na usihoji huyo "MWAMBA" aliyekengeuka na kuacha waliyokuwa wakisifia hao "wajinga" wakao?

Kwa nini usimlaumu "MWAMBA" na badala yake unalaumu "wajinga" ambao bado wanashikilia matumaini yale yale ya ujumbe aliotoa "MWAMBA".
Huoni kuwa wewe ndiye chizi kabisa badala ya hao unaowaita wewe "wajinga"?

Halafu na wewe unajihisi kabisa kuwa unazo akili za kujadili jambo la maana?
 
Ni kawaida kwa watu wanafiki kusema hawana upande.. mnafiki haoni aibu kumkana mtu wake hadharani. Wanafiki wengi leo mnamkana Mbowe hadharani.
 
Hahahah hapo wanasuburia sinia la mbuzi choma washibe wakajambe mbele😂
 
Ni kawaida kwa watu wanafiki kusema hawana upande.. mnafiki haoni aibu kumkana mtu wake hadharani. Wanafiki wengi leo mnamkana Mbowe hadharani.
Haya sasa; nieleze mtu anayemzidi unafiki Samia Suluhu Hassan; ambaye ndiye anayekufuga wewe, hadi kuchukua jina lake kabisa! hujui ulaghai mwingi alionao Samia?
 
Ndugu kalamu wewe ni mtu dhaifu sana kiakili kama unadhani ID ya JF ndo kipimo cha akili za mtu.
Katika mambo yanayodhalilisha kwa binaadam yeyote, ni kujitambulisha kuwa kama mali ya mtu mwingine. Hapo ulipo wewe utambulisho wako ni kielelezo sahihi kabisa ya ukosefu wa kujitambua mwenyewe kuwa ni binaadam anayejisimamia mwenyewe.
 
Katika mambo yanayodhalilisha kwa binaadam yeyote, ni kujitambulisha kuwa kama mali ya mtu mwingine. Hapo ulipo wewe utambulisho wako ni kielelezo sahihi kabisa ya ukosefu wa kujitambua mwenyewe kuwa ni binaadam anayejisimamia mwenyewe.
Tafuta hoja nzito kisha urudi.
 
Haya sasa; nieleze mtu anayemzidi unafiki Samia Suluhu Hassan; ambaye ndiye anayekufuga wewe, hadi kuchukua jina lake kabisa! hujui ulaghai mwingi alionao Samia?
Huna hoja ndugu. Nimeamua nikupuuze.
 
Mbona Tundu atatoka tuu...

Haya ushahidi walioutegemea wa video umekataliwa...
Sasa utaishawishi vipi Mahakama kwa maneno ya askari bila kuwa na udhibitisho wa mhusika ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…