G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,795
- 36,704
Watu hamjui tu ila hili sekeseke la Chadema na Samia tulianza nalo mwaka 2022 mwishoni. Ilikuwa ghafla sana mwenyekiti wetu alibadili "jia" angani.
Aliyosema Lissu leo ni ukweli mtupu. Ndani ya Chadema kulikuwa na vuguvugu sii la kitoto. Mnyika ni shahidi.
Mwenyekiti alikuja na mapendekezo kwamba kusiwe na mgombea urais mwenye nguvu ama asiwepo kabisa mwaka 2025. Pia akaja mpaka na orodha ya majimbo ambayo Chadema ingeachiwa mwaka 2025. Kama kuna mtu atabisha basi tutayaweka hadharani. Miongoni mwa hayo majimbo watu wake nanga zinapaa kweli kweli kwa sasa maana wana faida wataipata huko mbeleni. Sisi tuliuliza, kwanini tuingie kwenye makubaliano hayo? Mbona nguvu tunayo?
Kiukweli ni jambo baya sana kumsema kiongozi mwenye Legacy kama Mbowe lakini hapa mwishoni alituuza, alituweka rehani. Sisi wengine tulihoji kulikoni? Mbowe anafaidika na nini? Mbona uwezo wa kupata hata majimbo zaidi ya 100 tunao mwaka 2025? Leo tuingie kwenye maridhiano ya kudanganywa na majimbo chini ya 20 ili tu mtu avuke? Ili nani afaidike?
Yapo mengi kweli tutayasema wazi wazi siku za mbeleni ila Mbowe kwa hatua aliyokuwa amefikia si wa kumung'unyiwa tena maneno! Aliharibu pakubwa!