Mbowe alimpigia simu Rais Samia kumpa pole akiwa Dubai

Mbowe alimpigia simu Rais Samia kumpa pole akiwa Dubai

Determinantor

Platinum Member
Joined
Mar 17, 2008
Posts
59,045
Reaction score
94,974
Kwenye Space ya Maria inayoendelea, Mheshimiwa Lema anasema kuwa Mheshimiwa Mbowe alimpigia simu Rais Samia na kumpa pole kifuatia kifo cha Dkt Magufuli.

Wakati huo Mheshimiwa Mbowe alikuwa Dubai na kwamba Rais alimuahidi Mheshimiwa Mbowe kuwa Mara baada ya msiba kuisha, wangekutana na kuijenga Tanzania mpya, huku Mama Samia akiahidi na kumhakikishia Mheshimiwa Mbowe "kufutana machozi" wote.

Akimaanisha kuwa hata yeye alikuwa "ameguswa" na utawala uliopita.

Mheshimiwa Lema amesisitiza kuwa kama ni Uongo, basi Mama Samia ashike msaafu aape kama ni uongo.

Kwa hiyo Rais Samia aliongea na gaidi? Akaahidi kufutana machozi na gaidi?
 
Lema anajaribu kujaza matambala ili viatu vya dr Slaa vimtoshe lkn wapi bado vinampwaya tu dah... Kwa sasa hivi hata Mbowe anajutia alichokifanya 2015. Maana hela alizopewa zishamwishia na chama pia kinamfia aisee!!!
 
  • Thanks
Reactions: mmh
Listeners wako online kwa muda huu ni zaidi ya 3,700

Screenshot_20210810-232524.png
 
Wanaouliza kwa nini Mbowe amekamatwa sasa na si vinginevyo wanasahau kuwa Mbowe, Lema, Meya wa zamani Ubungo Boniface walikamatwa mara baada ya matokeo ya uchaguzi mkuu kutangazwa na kabla Rais hajaapishwa kwa kuchochea maandamano yasiyo na kikomo kupinga matokeo. Mambosasa alihojiwa na vituo vya ITV na TBC na kutoa madai hayo hayo ya ugaidi.
 
Wanaouliza kwa nini Mbowe amekamatwa sasa na si vinginevyo wanasahau kuwa Mbowe, Lema, Meya wa zamani Ubungo Boniface walikamatwa mara baada ya matokeo ya uchaguzi mkuu kutangazwa na kabla Rais hajaapishwa kwa kuchochea maandamano yasiyo na kikomo kupinga matokeo. Mambosasa alihojiwa na vituo vya ITV na TBC na kutoa madai hayo hayo ya ugaidi.
Acheni ujinga wewe, unavunja Sheria za JF na unaweza kupata Ban
 
Kwenye Space ya Maria inayoendelea, Mheshimiwa Lema anasema kuwa Mheshimiwa Mbowe alimpigia simu SSH na kumpa pole kifuatia kifo cha JPM. Wakati huo Mheshimiwa Mbowe alikua Dubai na kwamba SSH alimuahidi Mheshimiwa Mbowe kuwa Mara baada ya msiba kuisha, wangekutana na kuijenga Tanzania mpya, huku Mama Samia akiahidi na kumhakikishia Mheshimiwa Mbowe "kufutana machozi" wote. Akimaanisha kuwa hata yeye alikua "ameguswa" na utawala uliopita.

Mheshimiwa Lema amesisitiza kuwa kama ni Uongo, basi Mama SSH ashike msaafu aape kama ni uongo!

Kwahio SSH aliongea na Gaidi? Akaahidi kufutana machozi na Gaidi??

Hadithi za kubumba hizi. Mtu hata kabla hajaapishwa aanze kutoa ahadi za aina hiyo? Maybe if she had been waiting for that moment for a long, long time, which I know that wasn’t the case!
 
Back
Top Bottom