Mbowe alivyokimbiwa na wafuasi wake ni kama Yesu alivyoachwa solemba na wanafunzi wake akakamatwa na jeshi la Rumi

Today I've confirmed without a doubt that, Mbowe is a public servant and a secret card bearer.

And it'll take ages for most Tanzanians to demystify this ploy.​
 
Mchungaji Msigwa alipogundua kuwa Green guard na vibaraka wao (Police) hawawezekani, akaamua aunganenao.
 
Soma vizuri Biblia usikurupuke.
Yohana 18
8 Yesu akajibu, Nimekwisha kuwaambieni ya kwamba ni mimi; basi ikiwa mnanitafuta mimi, waacheni hawa waende zao.

9 Ili litimizwe lile neno alilolisema, Wale ulionipa sikumpoteza hata mmoja wao.
 
Soma vizuri Biblia usikurupuke.
Yohana 18
8 Yesu akajibu, Nimekwisha kuwaambieni ya kwamba ni mimi; basi ikiwa mnanitafuta mimi, waacheni hawa waende zao.

9 Ili litimizwe lile neno alilolisema, Wale ulionipa sikumpoteza hata mmoja wao.

Unafikiri kwa nini Petro alimkana Yesu kama hawakumkimbia?
 
Yesu naye alikuwa mwenyekiti kama alivyo Mbowe, Yesu aliwatendea watu wengi miujiza na kufanya makubwa sana ambayo yalivuma na kuwa maarufu katika Judea, Samaria, mama nchi jirani.
Bado sijasoma andiko zima; lakini nimeangalia michango yote iliyo wasilishwa hadi sasa kwenye mada yenyewe na jinsi ulivyo fuatilia na kuweka maoni yako kwenye michango hiyo.

Wakati nikianza tena kusoma mada yenyewe; nilipofika tu kwenye mistari hiyo niliyo nyanyua hapa; mara nikaanza kupoteza hamu ya kuendelea na andiko lote.
Nadhani nime hitimisha na kujiridhisha sasa ninavyo yaelewa maandishi yako humu.

Unajitambulisha mwenyewe kuwa ni "Mwandishi na Mtunzi"! Utambulisho huo pekee una maana pana sana; ikiwemo uandishi makini au utunzi tu wa mambo kadri yanavyo kuingia kichwani.

Kwa hiyo, nimejiridhisha sana, hapa hakuna la kuchukulia kwa uzito unaostahili kwenye maswala kama haya yanayo ikabili nchi yetu sasa hivi. Hakuna uzito katika maandishi yako unao endana na maswala mazito yaliyo mbele yetu. Ni uandishi tu wa makala zinazoyumba yumba; zisizo na msimamo maalum.

Haya ndiyo maoni yangu ya mwisho kuhusiana na makala zako hizi humu JF. Wakti nikiagana na uandishi wako huu, nimekumbuka kama huko nyuma pia niliwahi kukusoma; na pengine maoni yangu hayakuwa tofauti sana juu ya makala hizo na haya ya leo.
Nimalize kwa kurudi pale pale pa mwanzo. Tanzania imeingia katika awamu mpya kabisa. Sina shaka hata kidogo kwamba hatimae mabadiliko makubwa yatafuata. Hakuna wa kuyazuia mabadiliko haya katika muda wa uhai wa kizazi hiki.
 
Unafikiri kwa nini Petro alimkana Yesu kama hawakumkimbia?
Umesema Petro!
Unaelewa maana ya maneno haya;

Marko 14
27 Yesu akawaambia, Mtakunguwazwa ninyi nyote kwa ajili yangu usiku huu; kwa kuwa imeandikwa, Nitampiga mchungaji, na kondoo watatawanyika.
 
Watanzania ni watu. Usiwa underestimate.
Polisi sio wajinga kufanya wiki nzima HIKI walichokifanya.

Mtu ni mtu Mkuu.
Ukipuuza kidogo mambo huweza kubadilika kwa namna itakayokushangaza
"Ukicheka na nyani utavuna mabua".

CDM walipewa 4R, kesi za kubambikiziwa na Magufuli zikafutwa, waliokuwa ukimbizini Canada na Belgium wakarudi, walikuwa wanadai fidia ya hela walizonyang'anywa wakapewa.

Ila walimkosea sana Rais kwa namna ya haiba yake, wakasahau kuwa URais ni Taasisi. Kuna wakati wamekuwa wanatoa matamko utadhani CDM ndiyo wako Ikulu

Sasa nawataarifu tu kuwa wana deal na TAASISI
 
Uanjua
Yaani tatizo kubwa saan la CDM ni kutokuwa na watu wa mikakati wenye kuweza kudadvua issues.Nafasi waliopewa na Mama ilikuwa ni bahati ambayo haitaka itokee tena.
 

Hatari Sana
 
Umesema Petro!
Unaelewa maana ya maneno haya;

Marko 14
27 Yesu akawaambia, Mtakunguwazwa ninyi nyote kwa ajili yangu usiku huu; kwa kuwa imeandikwa, Nitampiga mchungaji, na kondoo watatawanyika.

Hujanijibu lakini
 
 
Nyie wazee wa falsafa na teolojia bana. Ila thanks kwa andiko murua, hujawahi kuniangusha katika kuupa ubongo tafakuri jadidi.
 
U
Umejenga hoja critically japo mimi nina maoni tofauti kidogo.

Kwanza uelewe mtu asiye na silaha hawezi kupambana na mwenye silaha na hastahili kulaumiwa kwa sababu askari akikupiga kirungu utavunjika au akikupiga risasi utakufax huwezi kujifuta. Hivyo lazima muandamanaji atumie busara sio kujipeleka.

Pili polisi waliblock barabara zote zinazoenda kwenye assembly points za maandamano hao waandamanaji wangefikaje pale?

Mbowe na wenzake walijua kabisa hiki kikichotokea leo kuwa kingetokea wao sio wageni wa hatua za watawala lakini bado walisisitiza kuandamana kwa sababu walikusudia dunia ione jinsi serikali inavyominya demokrasia kwa kutumia mabavu na serikali imeingia mtegoni, tayari taswira ya serikali kimataifa imechafuka. Unawezaje kutumia silaha nzito dhidi ya raia wako ambao hawana silaha na wanaandama kuonyesha hisia zao ,, hapo serikali imeingizwa kingi.

Mchi za magharibi zimeona kuwa uchaguzi unakaribia hivyo serikali ya CCM imeamua kuwafanyia violence wapinzani ili wasiweze kujiandaa kushiriki uchaguzi au uchaguzi usiwe huru na haki.

Serikali ilitakiwa iwaache CHADEMA waandamane ili kuhadaa ulimwengu kuwa Tanzania kuna demokrasia lakini kwa ilichofanya hasa ukizingatia maanda.ano yalikuwa ni kupinga watu kutekwa, kupotezwa na kuuawa jambo ambalo pia nchi za magharibi wanalipigua kelele basi serikali isingezuia maandamano ili kuwahadaa nchi za magharibi.

CHADEMA leo wameibuka washindi kwa kudraw sympathy ya ulimwengu wa kidemokrasia wakati serikali imeadhirika na pia kutakuwa na cost. kiuchumi
 
Hujanijibu lakini
Hakumkimbia.
Ndio maana wakati wamekuja kumkamata Yesu Petro ndio aliyemkata sikio mmoja wa wale waliokuja kumkamata Yesu.

Peter alimfuata aone mwisho wake.

Mathayo 26
58 Na Petro akamfuata kwa mbali mpaka behewa ya Kuhani Mkuu, akaingia ndani, akaketi pamoja na watumishi, auone mwisho.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…