Tuseme ukweli jamani, chadema ilikua ICU aliyekuja kuiponesha ni mama Samia. Leo 'mganga" aliyewapa mwarubaini na kuwatoa ICU ndiye huyohuyo wanamuona ni mchawi.
Hakuna" kiongozi" yeyote wa chadema sasa hivi anaefanya siasa kwa kuwa labda kuna sera au malengo wanayoyafata. "Viongozi" wote wa chadema sasa hivi ni wakandarasi wa kila mmoja kivyake. Hakuna sera, hakuna mpano, hakuna kuratibu.
Anaemlipa mmoja wao yeyote zaidi ndiye ataetangaziwa anachokitaka. Hili ni wazi kabis.
Sukuma ganga, inawatumia, haya gang inawatumia, wafanya biashara wlaiokuwa wanafaidika na misamaha ya kodi kupitia kanisa wanawatumia. Wafanya biashara walioumizwa bandarini wanawatumia.
Mafaruku ndani ya chadema ni mkubwa sana, kila mmoja sasa hivi amakula kwa urefu wa kamba yake.
Tusitegemee kabisa kuona chadema ikiwa chama cha ushindani wa kisiasa kama wengi wanavyotarajia. Sasa hivi humo ndani kuna ugomvi wa chini kwa chini wa nani hajatoa mgao fulani waliopokea kwa fulani. Kuna mparaganyiko wa hali ya juu ambao kwa kutazama kijuujuu hautauona.