Mbowe amepoteza sifa za kuendelea kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA

Mbowe amepoteza sifa za kuendelea kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA

William Mshumbusi

JF-Expert Member
Joined
Mar 27, 2012
Posts
1,761
Reaction score
2,391
Asante kwa kuamua kusoma peji hii. Naamini utajadili hoja ukiwa na fikra huru na c utumwa wa fikra.
Wapo watu wengi sana wanaozani kuwa kumkosoa mbowe ni kuitukana chadema hili si kweli kabisa.
Chadema itakuwa safi tu iwapo itamuondoa mbowe kwenye uwenyekiti.

Natambua mchango mkubwa wa mbowe katika kuijenga Chadema. Amefanikisha mipango mingi mizuri kama kuanzisha kanda, M4c na kuongeza wanachama. Pia kajitahidi sana kutatua migogoro mingi ya ndani bila kufukuza mtu. Kwa ujumla C mtu wa Visasi na anabusara kubwa sana juu ya uongozi.

Kwa sasa kwa heshima ya Mbowe naomba aandae utaratibu wa kumkabithi chama Kamanda mwingine anayeaminika uwenyekiti lakini asiwe Dr Slaa au Zitto.
SABABU ZA KUACHIA UONGOZI.;-

Uongozi mzuri ni kuacha madaraka Kistaarabu tena ukiwa bado unapendwa na unanguvu na kubaki kama mshauri.

2. Kuondoa dhana ya kung'ang'ania madaraka ndani ya Chadema.
1488314_185131778355725_308368871_n.jpg

3. Mbio nzuri ni za kupokezana vijiti ili atakaepokea aongeze kasi, mbinu na ari kufikia mabadiliko ya kweli.
4. Inaweza kupunguza propaganda kadhaa zidi ya Chadema
5. Tuweke tofauti kidogo na wapinzani kwa kukabidhiana madaraka bila kupinduana na kutokuwa na wafalme katika vyama kama ilivyo kwa NCCR, TLP, CUF NA UDP. Na ndio sifa ya Chadema toka awali. Alianza Mtei akaja Makani na Sasa mbowe tena kwa makabidhiano ya Amani

Kiongozi mpya awe na sifa zifuatazo

1. Awe Mwanaharakati na amedhamilia Kuikomboa Tz. Apimwe kwa alivyofanikiwa kuidhiti CCM jimboni kwake ata uchaguzi ukirudiwa leo CCM wasiambue kiti cha udiwani ata kimoja kwenye jimbo hilo. Kama ilivyokuwa kwa Wangwe na sasa Arusha. Hai kuwa na madiwani wengi wa CCM ni dosari kubwa sana kwa Mbowe

2. Awe na uvumilivu mkubwa sana wa kisiasa hasa za ndani ya CHADEMA ASIWE NA HASIRA AU KISASI AU MTAZAMO HASI KWA WATU WANAOTOFAUTIANA MITAZAMO. Hapa Mbowe alifanikiwa sana. Ila , Lema, Slaa, Lissu labda wafundwe sana ndipo wafikie sifa hii

3. Asiwe na maslahi binafsi Muwazi na mkweli na mwenendo usiotia mashaka.

CHADEMA LAZIMA ITAWALE MEDIA ZOTTE KWA NGUVU ZA MICHANGO YA UMMA KAMA MATANGAZO YA SERA ZAO kwenye magazeti, mikutano yao ya kitaifa kuwekwa laivu kwenye TV NA REDIO VIPEPERUSHI NA CD. Si kilamtu anaYEkwenda kwenye mikutano ya hadhara na haya mabomu yanavyorushwa HIVISASA.

Kitu nachojua MBOWE HAWEZI kukubali Chadema ijitangaze kwenye media au kumiliki media zake yani Redio, Tv stesheni na Gazeti kwani KUKIFANYA hivyo ni kuua soko la Media Zake na anachofanya ni kulinda Soko la Magazeti yake na Redio yake binafsi alizonazo Zinazouza habari za CHADEMA ZAIDI.

Nachochujua Chadema ilichobakiza hadi kuchukua nchi ni kumiki media zake tu. Hatua ambayo mbowe hawezi na baadhi ya wanamageuzi wenyefikira huru huweza kumuhisi kuwa ni Pandikizi na labda kaishakula vya watu na lengo lake sasa ni kuidumaza chadema. Yani ilipofikia ndipo hapohapo na hii kumkamatakamata ni kama maigizo tu ndani ya democrasia yetu. Kwani naona kama amepoooza.

Chadema kuendelea kuwa na Mbowe ni kujiandalia bomu litakalolipuka wakati wowote.

Mbowe ndiye aliyemfundisha Zitto siasa za kupiga Madili na ndiomaana aliingia ugonvi mkubwa na mwanaharakati Chacha Wangwe mtu wa haki.
Uzi wangu wa kwanza Jf ulihusu kufanana sana kwa Tabia kati ya Mbowe na Zitto ila ukafutwa. Ulisomeka Zitto anatofautiana nini na Mbowe?

Bora apewe chama mtu mwenye ari na moyo toka Moyoni Kama Lema au Tundu Lisu kuliko huyu tunayesema anabusara.
 
unataka ugomvi na mzee mtei? hujui kuwa chdm ni mali ya mtei na ukoo wake pamoja na marafiki
 
Anza na wale Masultani wa CUF, TLP, UDP, DP, SAU etc. Chadema Kimeishakuwa na wenyeviti Mtei, Bob Makani na Sasa mbowe-unataka Demokrasia gani zaidi ya hapo??
 
Bado anahitajika, nadhani utaheshimu mawazo yetu. Labda dhaifu ndo abadilishwe, mrema abadilishwe, cheyo abadilishwe etc
 
Mkuu,

Nikupongeze kwa kuwa huru na kuachana na utumwa wa fikra kama walivyo mashabiki wengine.

Hoja yako ni ya msingi sana, na nitoe rai yangu kwa wana CHADEMA kusu uhuru wa mawazo, ni vyema ukawa huru.
 
Matatamani sana Magamba amewapeleka puta kama sasa mnataka apumzike, bado hajachoka labda muongeze nguvu za TLP, CUF, NCCR na UDP; lakn dafu hamfui, maana CDM ni nguvu ya wananchi sasa hao vibaraka watasaidia nini mwanachi akishasema, muwaulize wakoloni mwananchia aliposema TANU ilikuwaje
 
Kweli watanzania wanahitaji mabadliko ila tatizo ni je wapinzani wamejipanga vizuri,Mbowe amefanya kazi kubwa sana ya kukuza chama ila bado kuna kazi kubwa ya kufanya.sasa pia kuna shida,kuna siku nilitoa ushauri Msemaji wa chadema akanitolea maneno ya dhihaka (kagame stlyle.LAZIMA CHADEMA MKUBALI KUSHAURIKA SIO KUNG"ANGANIA MADARAKA
 
hoja yako haina mashiko, kura za kamati kuu ndo zitaamua nani awe kama mbowe bado anapendwa aendelee, kama mbowe akikataliwa kwenye kura aheshimu pia maamuzi ya chama
 
Mkuu,

Nikupongeze kwa kuwa huru na kuachana na utumwa wa fikra kama walivyo mashabiki wengine.

Hoja yako ni ya msingi sana, na nitoe rai yangu kwa wana CHADEMA kusu uhuru wa mawazo, ni vyema ukawa huru.
Unaonekana usiku ukishakula magimbi,mchana dhambi ila usiku uovu
 
William, huwezi mkapokezana kijiti popote kule uwanjani, ipo sehemu maalum, anakuwepo mtu kesha jiandaa kukupokea! Tena sio sahihi kubadili makamanda wakati ushindi unakaribia, ni vyema zaidi kuimarisha hao walio kwenye mapambano kwa kuwapa ushirikiano ili kufanikisha. Tafakuri hii ni nzuri tu pale ambapo tumefika pale pa kupokezana ambapo wote tuwe tunapafahamu hata maadui/watani wetu.

Halafu nadhani historia inakukimbia haraka- tayari Chadema ni tofauti na vyama vingine. Tumekuwa (leo najidai) na Wenyeviti na makatibu kuanzia enzi zile za yule Mzee wa makampuni ya Sigara na yule wa Benk kuu. Sio kama TLP na NCCR au CUF!
 
Hujasema Kwanini Mbowe amepoteza uhalali wa kuwa mwenyekiti wa Chadema
 
Matatamani sana Magamba amewapeleka puta kama sasa mnataka apumzike, bado hajachoka labda muongeze nguvu za TLP, CUF, NCCR na UDP; lakn dafu hamfui, maana CDM ni nguvu ya wananchi sasa hao vibaraka watasaidia nini mwanachi akishasema, muwaulize wakoloni mwananchia aliposema TANU ilikuwaje

ushabiki wa siasa ni tofauti sana na wa mpira.
Kuwa sehemu ya mabadiliko ya kweli. Naamini Lema, Mdee wakifundwa wanaweza kuwa Wenyeviti wazuri.

Tunapojadili mabadiliko tunaijadili CHADEMA TU. Tlp, Udp, Dp, na Cuf ni Vivuli tu au ni sawa na kujifunika mwanvuri wa kuzuia jua CHINI YA MTI WENYE KIVURI AU MWANVURI WA mvUA CHumbani
 
Mbowe kwa sasa anakimbiza kila mkutano cjui ndiyo anataka aingie Magogon. Babu kimyaaa. But ukweli Mbowe hana mashiko sana kwa watz kwa ujumla. Angepewa Mkigoma hata mimi ningeingia cdm.
 
Kama nimeielewa vema hoja yako, ni dhahiri kwamba Mbowe hajapoteza sifa za kuwa mwenyekiti wa CHADEMA badala yake unatoa pendekezo la Mbowe kuondoka madarakani akiwa bado anapendwa. Hiyo haimpotezei sifa za kuendelea kuwa mwenyekiti. Lakini pia kama kiongozi anafanya vizuri binafsi sioni sababu ni kwanini aondoke. Maana tunaweza kumuweka mwingine halafu akatuulia chama. Kwanini tusimwache Mbowe akifikishe chama Ikulu ndipo aachie ngazi?

Kama mtu alikuwa kwenye running track anakimbia kwa nguvu zote, na yumkini anawashinda wengine wote hatuwezi kusema sasa aondoke wakati bado anashangiliwa ili aingie mwingine amalizie. Tutamtia nguvu ili amalize race yake kwa ushindi halafu baada ya hapo tutamwambia sasa pumzika. Tunataka Mbowe atupeleke Ikulu, then tumtangaze kama shujaa wetu.
 
Nadhani ungeanza wewe kuwa objective kwa kutoa tafsiri halisi ya demokrasia na kuonyesha misingi isiyotia shaka ya demokrasia katika kujenga hoja yako ambayo nina ujasiri wa kuipa jina 'short sighted analyisis'.

Kinachoamua uongozi wa kisiasa ni demokrasia na si vinginevyo.Huwezi kuzuia demokrasia kwa utashi binafsi.It's nonensense!
y
Demokrasia ni mchakato,haki za watu hazifungwi kwa njia yoyote wala maoni binafsi zaidi ya sauti itokanayo na ballot box.
 
Back
Top Bottom