Mbowe amepoteza sifa za kuendelea kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA

Mbowe amepoteza sifa za kuendelea kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA

We ndo x-husband wa josephine? Nikipata jibu ntarudi tena.
 
Hii hoja ingekuwa nzuri kama uchaguzi ujao Mbowe atang'ang'ania madaraka .... ila kwa sasa umewahi mno ukizingatia hiyo heading uliyoweka
 
"Mbowe amepoteza sifa za kuendelea kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA"!!!??? ....basi angalau kuhalalisha haya maelezo yako yasiyoeleweka malengo yake ungelituambia ni mwenyekiti wa chama gani kingine chochote aliye na sifa. Huyu huyu Mh. Mbowe ndiye ataipa cdm dola muda sio mrefu kwa taarifa yako!
 
Mushumbusi

Binafsi nimejiuliza sana Why umepost hii kitu. Uchaguzi wa CHADEMA ni this year,,wala hatujasikia Mbowe anasema atagombea tena au lah na offcourse CHADEMA inaendeshwa na KATIBA,,,it's very very bad unajaribu kuspin kitu ambacho kwa tunaokujua huna sifa ya kufanya hivyo. You hyprocritically pretend to be on the Side of Mbowe and not on the Side of CHADEMA management. CHADEMA ni wamoja you have to support them all as the Management and Working Together Ideology,,,,Unasema Lissu, Zitto, Dr Slaa hawafai kuwa wenyeviti labda wapewe Semina kidogo.

Umesahau au hujui kuwa Every person has his/her own Stregth and Weakness. Kama unaipenda CHADEMA unatakiwa kufuata misingi ya kutii Katiba ya Chama, Sheria na Kanuni zinazokiendesha Chama. Umeainisha weakness moja tu ya Ndg Mbowe na zilizobaki ni Streght, katika hali ya kawaida Mazuri yakizidi mabaya unachukua yale mazuri kwa matarajio ya kufanyia kazi yale madhaifu, nadhani unajua hivyo pia,,,,kwa nini sasa usiungane nasi ili tuendelee kushinikiza uanzishwaji wa hizo media unazozisema ingawa najua tayari ufafanuzi ulishatolewa kwamba suala hili linashughulikiwa na litafanyiwa kazi in Short Period.

Nakushauri popote pale ulipo wewe ndio uwe Media ya CHADEMA itangaze CHADEMA iingie mioyoni mwa watu, hakika wewe ni mmoja wa watakaofaidi matunda ya TANZANIA tuitakayo baada ya 2015 CHADEMA kukabidhiwa dola. Ni suala la muda,,,

ni mmoja kati ya wanasiasa wachache waupinzani wanaojua wanachokifanya.

Umenicot vizuri swala nalojiuliza kwa Mbowe kama wanachadema wanachangia Chama kwa moyo moja vipi Chadema washindwe kuanzisha media Zake?

Kwanini mbowe asimamie hilo kikamilifu. Bila Media CHADEMA KUCHUKUA NCHI 2015 Ni ndoto
 
unataka ugomvi na mzee mtei? hujui kuwa chdm ni mali ya mtei na ukoo wake pamoja na marafiki

Baba Mwenyekiti wa CCM, mke mjumbe wa NEC-CCM, mtoto mjumbe wa NEC-CCM, binadamu mwenyekiti wa CCM................... Hiyo kwao na kwako ni sawa!!
 
Slowly but surely for CCM..........

stupid01.gif
 
Kama Mbowe amepoteza sifa za kuwa mwenyekiti wa CHADEMA basi JK hajawah kuwa na sifa hata moja ya kuwa mwenyekiti wa CCM.
 
Ma.p.umb.av..u. mengine kama huyu William Mshumbusi Mi nikiwaonaga humu wananichafuga sana nafsi yangu mipuuzi wajinga sana!
 
Last edited by a moderator:
mbona sijaona mtu akimwambia mleta mada kua "umetumwa eenh" :smile-big:
 
mwekiti mwingine chadema utarajie baada ya miaka kumi ijayo wala siyo leo,mipango iko wazi kuwa mbowe ataendelea kuwepo sana halafu ukimuondoa mbowe wenye chama utawaambia nini.
 
kunaoja umejaribu kuzipanga lakini bado ushawishi wako upo chini ya kiwango.
Ebu kasome katiba ya chdm kwanza, alafu tafuta historia iliyo kamilika ya chdm ndipo urudi tena kuja kutushawishi.
Karibu tena.
 
mwekiti mwingine chadema utarajie baada ya miaka kumi ijayo wala siyo leo,mipango iko wazi kuwa mbowe ataendelea kuwepo sana halafu ukimuondoa mbowe wenye chama utawaambia nini.

huwa siungani na wanafiki kama wewe tupo kwenye kujenga na C kubomoa Chama.

Najua hata Mbowe mwenyewe anaelewa dhamira nzuri niliyonayo
 
kunaoja umejaribu kuzipanga lakini bado ushawishi wako upo chini ya kiwango.
Ebu kasome katiba ya chdm kwanza, alafu tafuta historia iliyo kamilika ya chdm ndipo urudi tena kuja kutushawishi.
Karibu tena.

Labda umeanza kusoma hoja ukichukulia mimi ni mpinzani wa upinzani ndio maana hukunielewa.

Tunaangalia hoja za kujenga tu hapa
 
Ni maelezo makini sana na inahitaji watu wenye akili huru kuchambua mambo na wenye kuona mbali sana kukuelewa ulichokikusudia.We kweli unaipenda CHADEMA.Watu wenye busara huwa wanasema hivi:Rafiki wa kweli ni yule anayekukosoa na rafiki asiye wa kweli ni yule anayakusifia tu.Bwana Mushumbusi kusema kweli haya mawazo yako ndiyo yalikuwa kichwani mwangu muda mrefu sana sema tu ndani ya CHADEMA kuna utamaduni mpya umejengeka wa watu kutopenda kuona Viongozi wakikosolewa na utahisiwa kama mtu unayetaka kukibomoa Chama kumbe lengo lako ni kukiboresha zaidi Chama ili kiwe Imara zaidi mbele ya safari.Nakubaliana na hoja yako kwa asilimia mia moja na kwa wale wanaokitakia mema Chama hiki cha Kizalendo watachukua hatua stahiki.Ushauri mzuri sana na wenye mawazo yenye vitamin zote muhimu za kuimarisha afya ya Chama chetu.
 
Nadhani ungeanza wewe kuwa objective kwa kutoa tafsiri halisi ya demokrasia na kuonyesha misingi isiyotia shaka ya demokrasia katika kujenga hoja yako ambayo nina ujasiri wa kuipa jina 'short sighted analyisis'.

Kinachoamua uongozi wa kisiasa ni demokrasia na si vinginevyo.Huwezi kuzuia demokrasia kwa utashi binafsi.It's nonensense!
y
Demokrasia ni mchakato,haki za watu hazifungwi kwa njia yoyote wala maoni binafsi zaidi ya sauti itokanayo na ballot box.

Mkuu usitupeleka huko tafadhali,Hatutaki kukumbuka machungu ya uchaguzi ya uliopita ndani ya Chama ambao ulikaribia kuchafua taaswira nzuri ya Chama chetu na Demokrasia kwa ujumla..Let's move...Let by-gone be by-gone.
 
Back
Top Bottom