Mbowe amepoteza sifa za kuendelea kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA

Mbowe amepoteza sifa za kuendelea kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA

Yaan huwa sitaki kuamini Mbowe ni mwenyekiti,,elimu hana,opportunist mkubwa na hana sera zozote za maana.
Team Zitto
 
Hapa CHADEMA lazima tukiri bila kuutawala ulimwengu wa Media ili kuyafikisha mawazo ya Chama kwa umma mpana zaidi,ili kuhubiri sera za Chama,ili watu kuijua historia na mashujaa wa Chama ili kuwafanya Wananchi wajihisi wao ni sehemu ya CHADEMA,ili kuelezea malengo na madhumuni ya Chama kwa Watanzania na Tanzania kwa ujumla basi tusije kushangaa Chama Tawala kikirejea madarakani 2015.Nimependa mikakati iliyofanywa na uongozi wa sasa katika kukiimarisha Chama lakini nadhani ni wakati muafaka kwa Chama kama kutakuwa Uchaguzi wa ndani mwaka huu basi tutoe nafasi kwa watu wengine wenye sifa kugombea na wachaguliwe ili waje na mikakati mipya ya kupapambana dhidi ya Chama cha Mapinduzi nadhani mapambano ya kwenye media yatakuwa bora zaidi dhidi ya CCM kitu ambacho kinapuuzwa na Uongozi wa sasa.
 
mbona sikuelewi? dhana ya kupokezana vijiti ni safi kabisa. LAKINI, MBONA huwaambii CCM wenzako kuwa wakabidhi nchi kwa wengine nao waongoze? au dhana ya kupokezana vijiti ni kwa Chadema tu? mbona husemi kuna watu ndani ya CCM toka Enzi za mwalimu mpaka sasa bado wamekalia madaraka hadi wanaota kutu, hiyo huoni? Acha unafiki
 
Kama mtoa maoni, ulianza vizuri kiasi nikadhani kuna kitu twaweza pata toka kwenye maoni yako but umekuja kuharibu paragraph mbili Za mwisho.
 
Ukiacha ushabiki wa kijinga na akili za kushikishwa, hoja yako ni nzito na umeona mbali. Tatizo wengi wetu ndani ya CDM hatujitegemei kimawazo linapokuja swala la kujadili mambo ya uongozi ndani ya CDM. Ukitaka kuwafurahisha watu hapa sifa Mbowe, Slaa, halafu ponda Zitto.

Umenifungua macho sana kuhusu media. Nilikuwa najiuliza sana kwa nini CDM hawataki kuanzisha media zao. I see the point.
 
mbona sikuelewi? dhana ya kupokezana vijiti ni safi kabisa. LAKINI, MBONA huwaambii CCM wenzako kuwa wakabidhi nchi kwa wengine nao waongoze? au dhana ya kupokezana vijiti ni kwa Chadema tu? mbona husemi kuna watu ndani ya CCM toka Enzi za mwalimu mpaka sasa bado wamekalia madaraka hadi wanaota kutu, hiyo huoni? Acha unafiki

Mawazo kama haya ni mfu na lengo kubwa ni kubomoa chama. Ujinga unaofanywa na ccm na cdm mnataka muufanye. Badilikeni jamani acheni kusema mbona ccm hawako hivi. Badaye mkipewa nchi mtakuwa mnaiba, mkiulizwa mtasema mbona na ccm walikuwa wanaiba. Jitambueni..
 
Ni wazo zuri mkuu kwa sababu cdm wanahubiri democracy na wanadai wao ni zaid ya ccm. Wanapaswa kuonesha democracy kwa vitendo ndani ya chama na sisi tutakuwa na imani na wanachokisema majukwaani. Tofauti na hapo ni propaganda zilezile...
 
heading inaonyesha Mbowe amepoteza sifa , ndani haionyeshi kama amepoteza sifa au kitu kingine chochote ! Sijakuelewa , kama kupoteza sifa maana yake ni kukipeleka chama juu basi tuendelee naye , kuanzisha media za cdm ni wazo zuri bali kuna kitu usichokijua , mchakato wa vibali unaweza kuchukua hata miaka 10 ! usiulize kwanini .
 
Asante kwa kuamua kusoma peji hii. Naamini utajadili hoja ukiwa na fikra huru na c utumwa wa fikra.

Natambua mchango mkubwa wa mbowe katika kuijenga Chadema. Amefanikisha mipango mingi mizuri kama kuanzisha kanda, M4c na kuongeza wanachama. Pia kajitahidi sana kutatua migogoro mingi ya ndani bila kufukuza mtu. Kwa ujumla C mtu wa Visasi na anabusara kubwa sana juu ya uongozi.
Kwa sasa kwa heshima ya Mbowe naomba aandae utaratibu wa kumkabithi chama Kamanda mwingine anayeaminika uwenyekiti lakini asiwe Dr Slaa au Zitto.
SABABU ZA KUACHIA UONGOZI.;-

Uongozi mzuri ni kuacha madaraka Kistaarabu tena ukiwa bado unapendwa na unanguvu na kubaki kama mshauri.

2. Kuondoa dhana ya kung'ang'ania madaraka ndani ya Chadema.
3. Mbio nzuri ni za kupokezana vijiti ili atakaepokea aongeze kasi, mbinu na ari kufikia mabadiliko ya kweli.
4. Inaweza kupunguza propaganda kadhaa zidi ya Chadema
5. Tuweke tofauti kidogo na wapinzani kwa kukabidhiana madaraka bila kupinduana na kutokuwa na wafalme katika vyama kama ilivyo kwa NCCR, TLP, CUF NA UDP. Na ndio sifa ya Chadema toka awali. Alianza Mtei akaja Makani na Sasa mbowe tena kwa makabidhiano ya Amani

Hapo juu inaonesha wazi kuwa wewe myewewe hauko huru kifikra na maamuzi yako!.Hatufanyi jambo ili kuwafurahisha watu au taasisi, bali tunafanya mambo kwa kuangalia matunda chanya. Ko kusema mbowe atoke, naamini umekurupuka. kajipange upya fikra zako.

Kiongozi mpya awe na sifa zifuatazo

1. Awe Mwanaharakati na amedhamilia Kuikomboa Tz. Apimwe kwa alivyofanikiwa kuidhiti CCM jimboni kwake ata uchaguzi ukirudiwa leo CCM wasiambue kiti cha udiwani ata kimoja kwenye jimbo hilo. Kama ilivyokuwa kwa Wangwe na sasa Arusha. Hai kuwa na madiwani wengi wa CCM ni dosari kubwa sana kwa Mbowe

2. Awe na uvumilivu mkubwa sana wa kisiasa hasa za ndani ya CHADEMA ASIWE NA HASIRA AU KISASI AU MTAZAMO HASI KWA WATU WANAOTOFAUTIANA MITAZAMO. Hapa Mbowe alifanikiwa sana. Ila Zitto, Lema, Slaa, Lissu labda wafundwe sana ndipo wafikie sifa hii

3. Asiwe na maslahi binafsi Muwazi na mkweli na mwenendo usiotia mashaka.

Haujasomeka unataka nini?. Uongozi ni swala nyeti sio la kurukia rukia. Unajua mbowe amepata wapi uvumilivu ulosema hapo juu?. Kinachaigharimu CCM sasa ni kubandika uongozi wa kina Nape, mwigulu wakati hata hawajui nini wanaenda kufanya. Chadema we need time and very strong analysis of prons and cons before any move ahead.

CHADEMA LAZIMA ITAWALE MEDIA ZOTTE KWA NGUVU ZA MICHANGO YA UMMA KAMA MATANGAZO YA SERA ZAO kwenye magazeti, mikutano yao ya kitaifa kuwekwa laivu kwenye TV NA REDIO VIPEPERUSHI NA CD. Si kilamtu anaYEkwenda kwenye mikutano ya hadhara na haya mabomu yanavyorushwa HIVISASA.

Kitu nachojua MBOWE HAWEZI kukubali Chadema ijitangaze kwenye media au kumiliki media zake yani Redio, Tv stesheni na Gazeti kwani KUKIFANYA hivyo ni kuua soko la Media Zake na anachofanya ni kulinda Soko la Magazeti yake na Redio yake binafsi alizonazo Zinazouza habari za CHADEMA ZAIDI.

Nachochujua Chadema ilichobakiza hadi kuchukua nchi ni kumiki media zake tu. Hatua ambayo mbowe hawezi na baadhi ya wanamageuzi wenyefikira huru huweza kumuhisi kuwa ni Pandikizi na labda kaishakula vya watu na lengo lake sasa ni kuidumaza chadema. Yani ilipofikia ndipo hapohapo na hii kumkamatakamata ni kama maigizo tu ndani ya democrasia yetu. Kwani naona kama amepoooza

Point zako hazieleweki;anyway kila mtu ana fikra zake. Huenda utakuja na hoja badae
 
Mkuu,

Nikupongeze kwa kuwa huru na kuachana na utumwa wa fikra kama walivyo mashabiki wengine.

Hoja yako ni ya msingi sana, na nitoe rai yangu kwa wana CHADEMA kusu uhuru wa mawazo, ni vyema ukawa huru.

Kwa mwana CCM yeyote suala la Mbowe kuondoka katika safu ya uongozi CDM ni furaha tele. Kamanda anawanyima raha kweli kweli. Hatoki mtu hapo mpaka kazi ya kuikomboa nchi toka kwenye makucha ya mafisadi imekamilka. Endeleeni kusubiri ni lazima mngooke safari hii. Hatuna mchezo na hatudanganyiki.
 
Matatamani sana Magamba amewapeleka puta kama sasa mnataka apumzike, bado hajachoka labda muongeze nguvu za TLP, CUF, NCCR na UDP; lakn dafu hamfui, maana CDM ni nguvu ya wananchi sasa hao vibaraka watasaidia nini mwanachi akishasema, muwaulize wakoloni mwananchia aliposema TANU ilikuwaje
Yaani hawa jamaa akili zao hazina kumbukumbu kabisa maana toka mfumo wa vyama vingi uanza CDM imetoa wenyevitu na CCM toka ianzishwe imetoa wenyeviti 4 tu.
 
Back
Top Bottom