Waislamu ni Wazalendo, Wakristo ni Wabaguzi
· Ubaguzi ulimtoa MalimaCCM
· CUF kama TANU
· Chadema: Damu ya Muislamuhaikupewa thamani!
Na Kazi Msemakweli
Watanzania wana dini au imani zao mbalimbali lakini papo hapo ni wafuasi wa vyama mbali mbali vya siasa vilivyosajiliwa kwa misingi ya kisekula. Kwa kifupi,usekula maana yake ni itikadi isiyojali dini.
Lakini swali gumu ni je, watu wenye dini wanawezaje kuepuka imani zao pale wanaposhughulika na siasa? Jawabu la swali hili linahitaji utafiti mpana wa siasa za Tanzania kuanzia TAA, TANU, CCM hadi kuja Vyama vya Upinzani mwaka 1992
TANU na Dini
Tanganyika African National Union-TANU au Chama cha Umoja wa Kitaifa waTanganyika, kimsingi, kilikuwa ni chama cha kisiasa. Lakini waliounda chama hicho walikuwa na dini zao ambapo, bila shaka, hisia za dini zilikuwa na nafasi yake katika harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika.
Harakati hizo, kwa kiasi kikubwa, zilisukumwa na machungu ambayo Waislamu waliyahisi chini ya watawala wa Kikoloni ambao hawakuwa mbali na Wamishenari wa Kikristo katika kujenga maisha ya kijamii. Waislamu walikuwa ni jamii iliyotengwa na Mkoloni hasa hasa katika elimu, ambapo aliyetaka elimu,alilazimika kuchagua moja, dini au elimu. Baadhi wakabatizwa na kuritadi kwa sababu hiyo.
Siasa za Mkoloni zilienda sanjari na harakati za ubatizo za Wamishenari.Kwa kiasi kikubwa, hii ilikuwa ni kampeni ya kuritadisha Waislamu japo piailiwalenga wapagani. Kwa hali hiyo, Muislamu wa Koloni la Tanganyika lililokuwa na idadi kubwa ya Waislamu, si tu alikuwa na hisia za kupigania uhuru wa mtu mweusi au Mtanganyika, bali yeye alikuwa na ziada ya hisia za kuondokana na manyanyaso kwa sababu ya imani yake.
Kama inavyobainika katika kumbukumbu za historia ikiwa ni pamoja na maandiko na picha, jamii kubwa iliyounda nguvu ya kuikomboa Tanganyika ilikuwa ni ile ya Waislamu. Masheikh wakubwa na mashuhuri wakiwa na kanzu na kofia zao,na akina mama wakiwa na mabaibui yao walishiriki moja kwa moja katika harakati hizo.
Kwa mantiki hiyo, tayari inatosha kuthibitisha kuwa imani ya dini ilikuwa na nafasi katika siasa za ukombozi za Tanganyika zilizozaa vyama vya TAA na baadae TANU. Hata hivyo, ukali wa imani ya dini ulipozwa au kuzimuliwa sana na uzalendo wa Waislamu wa Tanganyika.
Waislamu waliojenga nguvu kubwa ya kisiasa chini ya vyama hivyo, walipozwa na nyoyo za uzalendo lakini nukta muhimu ni kuwa siasa hizo zilikuwa na uhusiano na imani za dini, na ndiyo kusema, TAA na TANU vilikuwa ni vyama vya siasa vilivyokuwa na uhusiano wa moja kwa moja na dini.
Historia ya Tanganyika haiwezi kuufuta ukweli kuwa udini wa Waislamu katika kutafuta uhuru ulisaidia mno kujenga nguvu za siasa za TANU ambayo, katika uchambuzi huu, tunaihesabu kama chama cha kwanza cha siasa baada ya uhuru.
Hata hivyo, udini wa Waislamu, licha ya kujenga nguvu kubwa ya chama hicho,bado haukuwa na chembechembe za ubaguzi dhidi ya Watanganyika wa imani nyingine. Licha ya wingi wao wa kanzu na kofia, bado Waislamu hawakujitambulisha kwa imani zao bali walisimama kama Watanganyika kwa maslahi ya Tanganyika.
Na laiti kungelikuwa na udini wa kumtenga Mtanganyika wa dini nyingine,Mwalimu Nyerere asingekuwa na nguvu ya kura za kumshinda Muislamu ndani ya TAAna TANU. Tofauti ya maoni juu ya uamuzi wa kumwachia Nyerere kuwa Rais wa TANU,ni uthibitisho wa ukweli kuwa Waislamu walisimamia siasa zaidi wakiamini kuwaTanganyika huru isingelikuwa tena na ubaguzi dhidi ya watu wa dini zote.
Hapa pana mambo matatu ya kuzingatia; mosi, kuwemo kwa idadi kubwa ya Waislamu katika chama cha siasa hivi leo kusiwe jambo la kushangaza kwani hiyo ndiyo historia ya siasa za Tanzania. Wakati fulani, na, pengine, hata sasa,Chama cha Upinzani, CUF, kilivurumishiwa propaganda za udini eti kwa sababu ya wingi wa Waislamu wenye kanzu na kofia katika mikutano yake jangwani au Kidongochekundu.
Pili, historia ya nguvu za kisiasa za Waislamu haioneshi ubaguzi wa kidini.Hii ina maana kuwa chama chenye Waislamu wengi si tishio kwa umoja na mshikamano wa Kitaifa, badala yake ni chachu ya mshikamano wa Kitaifa. Waislamu walijitolea kwa hali na mali kuijenga TANU, walimsaidia Nyerere hata katika mahitaji ya kawaida, lakini bado hawakufanya yote hayo kwa ajili ya kujenga himaya ya udini wala kujenga tabaka tawala la watu wa dini moja.
Kumkaribisha Mkatoliki Julius Nyerere, na kumpa uongozi ni ushahidi kuwa chama chochote chenye Waislamu wengi ni neema kwa wananchi wote bila kujali dini zao. Tatu, Kwa kuitazama historia ya siasa za Tanganyika,chama kinaweza kabisa kujengeka na kupata nguvu ya kuleta mabadiliko ya kitaifa kwa nguvu ya Waislamu.
Kwa upande mwingine, TANU, kama chama cha siasa, haikukosa uhusiano na dini nyingine tofauti na Uislamu. Hii ni dini ya Kikristo ambayo ni ya pili kwa ukubwa Tanzania baada ya Uislamu. Hata hivyo, uhusiano huu sasa ulikuwa na chembe chembe za ubaguzi.
Kwa maneno mengine, tofauti na uhusiano chanya wa Waislamu na TANU,Uhusiano wa Wakristo na TANU ulikuwa hasi. Uhusiano huu uliokuwa na chembechembe hasi ndio ulioleta hitilafu ya mfumo wa utawala Tanzania.
TANU, mikononi mwa Mwalimu Nyerere,ikawa na mwelekeo tofauti ambao Masheikh waliojaribu kuukosoa, walijikuta matatani. Almarhum Sheikh Hassan Bin Amir alisombwa msobe msobe kurejeshwa Zanzibar, Masheikh bara wakapata misukosuko hii na ile kwa sababu ya vuguvugu la upinzani dhidi ya mwelekeo wa siasa za Kikristo Tanganyika.
Nembo ya Bikira Maria na Kichanga Yesu katika sarafu ni moja ya maeneo yaliyowashitua Masheikh. Lakini tukibaki ndani ya Chama, Dkt. Sivalon, katika kitabu chake, Kanisa Katoliki na Siasa Tanzania, anatoboa siri kuwa Kanisa Katoliki lilianzisha Idara ndani ya chama cha TANU ambayo jukumu lake la msingi lilikuwa ni kupambana na Waislamu Tanzania mbali ya itikadi ya kikomunisti.
Mkurugenzi wa Idara hii alikuwa ni Fadha Schildknecht kati ya mwaka 1959 hadi 1966. Kanisa likiwa ndani ya chama cha TANU lilitoa ripoti kuwa Uislamu ulikuwa unastawi kwa kasi sanaTanzania hali ambayo ingeudhoofisha Ukristo.Tofauti na Waislamu waliotumia dini kukinufaisha chama hicho, Wakristo, kinara akiwa Mwalimu Nyerere, walitumia Chama kuimarisha dini.
Matokeo yake, Sivalon anaweka bayana kuwa, wakajivunia matunda haya; kwamba mwaka 1970, Wakatoliki waliunda asilimia 70 kati ya asilimia 75 ya Wabunge Wakristo wa kuchaguliwa. Waislamu walikuwa vipofu wa dini lakini Wakristo hususan Wakatoliki walijitazama kwa kioo cha dini.
Kwa kifupi, mkondo wa siasa ukabadilika. Hapa kuna mambo matatu ya kuzingatia, mosi, Wakristo, kwa kigezo cha Mwalimu Nyerere, ni wadini sana.Kwamba, kwao, dini ndiyo kigezo cha maamuzi yao ya kisiasa.
Na badala ya kuweka mbele uzalendo, kipaumbele chao ni Ukristo na hasa hasa Ukatoliki. Kuliweka wazi zaidi hili, Waskristo ni wabaguzi na wanawahesabu Waislamu kama maadui. Sasa hili ni jambo la hatari kwa umoja na mshikamano wa Kitaifa.
CCM na Dini
Kikiwa chama-mrithi wa TANU, Chama cha Mapinduzi-CCM kilizaliwa mwaka 1977.Kuzaliwa kwa chama hiki kipya kulihitimisha miongo miwili na ushee ya chama chaTANU. Uhusiano wa chama hiki na dini ulichukua zaidi mkondo hasi wa ubaguzi wakidini.
Kinadharia, CCM ilijitokeza machoni mwa Watanzania kama chama halisi cha kisiasa lakini ndani kikabeba ajenda ya siri ya udini. Fukuto la mapambano ya kudai haki sawa kwa wote miongoni mwa Waislamu lilitokana na mwenendo huo wa CCM kutumikia ajenda ya siri.
Marehemu Profesa Kighoma Ali Malima akajitokeza kama shujaa wa mapambano ya kudai haki sawa kwa wote ndani ya chama chake hicho. Jitihada za Profesa huyo zilikosa mwitiko wa Chama chake. Malima alionekana tatizo siku zote kwa sababu ya kukemea ubaguzi dhidi ya Waislamu na upendeleo kwa Wakristo.
Mapambano yake ya kisiasa ni ushahidi wa kutosha kuwa CCM ilikosa mizani sahihi ya kisiasa kwa sababu ya ajenda ya siri iliyofichwa ndani ya mfumo wa utawala. Wakati Waislamu wakiamini katika siasa za uzalendo chini ya CCM,Wakristo wakapata fursa ya kuimarisha mfumo wa ubaguzi ulioleta athari kubwa kwa Waislamu katika maeneo ya elimu na utawala.
Sivalon amebainisha kuwa, kwa jinsi mfumo wa utawala ulivyofungamana na Ukristo ikawa vigumu kubaini lipi la Kanisa na lipi la serikali. Mtu anaweza kuuliza kwa nini ulaumu chama kwa mambo yaliyotendwa na serikali. Jibu ni rahisi kuwa chama ndicho kilichoshika hatamu zote za uongozi na serikali ilikuwa ni chombo tu cha utekelezaji. Isitoshe,Mwalimu Nyerere aliyeweka mbele Ukristo na hasa Ukatoliki wake alikuwa na nafasi zote mbili. Yeye ndiye aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama na ndiye pia aliyekuwa Rais. Lakini tukibaki na shahidi mkuu wa ubaguzi wa Wakristo dhidi ya Waislamu ndani ya CCM, Prof. Malima, tunaweza kurejea kidogo nyuma kuona jinsi hali ilivyokuwa hadi alipofikia uamuzi wa kujitoa katika chama hicho.