Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 28,722
- 20,610
Ndugu zangu Watanzania,
Huyu Mwamba apewe Maua yake tu,apewe heshima yake tu.Atambulike na watu wote angali hai kuwa ndiye Mwamba aliyetumia ujana wake wote Kuitesekea na kuijenga CHADEMA kwa jasho na Machozi.Ametumia Muda wake wote kwa ajili ya chama.
Inasikitisha sana unapoona Mwana CHADEMA asiye jitambua akiongelea Puani kuwa Mwamba Amekaa Sana Madarakani na kwamba ilitakiwa apumzike. Hivi bila Mwamba Mbowe jabali la Siasa za Upinzani kukaa muda mrefu akiitumikia CHADEMA kwa jasho na machozi mnafikiri CHADEMA ingekuwepo? Mnafikiri kingekuwa chama kikuu cha upinzani hapa Nchini?mnafikiri ingefikia hatua ya kuongoza kambi ya upinzani Bungeni pamoja na kuongoza halmashauri za majiji kama Mbeya,Arusha ,Dar na Mwanza kama ambavyo ilifanya?
Mnafikiri kama siyo kukaa muda mrefu madarakani na kutafuta wanachama kwa jasho na Damu kila kona ya nchi hii CHADEMA ingeweza kuwa na ushawishi kwa vijana ? Mnafikiri kama siyo umadhubuti wa Mbowe na misimamo yake kungekuwa na bendera za CHADEMA zikipepea mitaani?
Hamjiuliza Kwani wakina Nccr Mageuzi wapo wapi? Akina cuf wapo wapi? Wana wanachama wangapi? Mnafikiri ni gharama kiasi gani Mwamba Ameilipia kwa chama kuweza kukua na kuteka hisia za watu? Mnafikiri ametumia pesa na rasilimali zake kiasi gani kuijenga CHADEMA?
kama siyo ushawishi wa Mwamba mnafikiri ni vipi matajiri , wafanyabiashara na watu mbalimbali kama ilivyokuwa akina Sabodo wangeweza isaidia CHADEMA kwa hali na Mali?
Embu Fikiria ilifika Wakati Mwamba na Jabali la siasa za upinzani alikuwa na Uwezo wa kurusha Helikopta zaidi ya Mbili angani kwa wakati mmoja kwa ajili ya kuimarisha chama ambapo zote zilikuwa zinafanya kazi ya kupishana angani na kuzunguka maeneo mbalimbali kuwafikia watanzania na kueneza sera na Misimamo ya chama.
Mnafikiri helikopta hizo zilikuwa zinatumia Maji kupaa angani? Mnajua gharama zake kwa saa moja achilia mbali kwa siku kwa helkopta kuwepo angani na kufika kilomita kwa kilomita katika mikoa mbalimbali hapa Nchini? Ni Mwamba na Jabali huyu wa siasa za upinzani ndiye aliyefanya watanzania wengine wakazifahamu hata helkopta.
Huyu Mwamba na Jabali la siasa za upinzani ndiye aliamusha morali ya vijana wengi sana hapa Nchini kugombea nafasi za uongozi na kupata ubunge bungeni na hata Udiwani halmashauri. Ni yeye ndiye alifanya vijana wadogo kwa wakati huo kama vile Mheshimiwa David Silinde, Halima Mdee,Zitto Kabwe,John Mnyika,Upendo Peneza,Sugu,Joshua Nasari ,Peter Lijuakali na wengine wengi kuingia bungeni wakiwa vijana wadogo.
Ni huyu mwamba aliwatoa uoga vijana juu ya kuogopa kugombea kama huna hela.maana siku za nyuma watu waliamini kuwa ni wazee pekee na wenye hela ndio walikuwa na sifa ya kuwa wabunge .Lakini Mwamba alibadilisha dhana hiyo na kupanda mbegu mpya kabisa kwa vijana na fikira za watanzania na hatimaye vijana kuanza kuaminika na kuchaguliwa na kuchagulika na kuungwa mkono na watanzania.
Ni huyu mwamba na Jabali wa siasa za upinzani alileta na kuinua mioyo ya vijana wengi sana kuipenda siasa na kujihusisha na siasa na kuanza kupiga kura na hata kushiriki sana kwenye mikutano ya kisiasa. Ni vipi unaweza kushindwa kutambua mchango wa huyu Mwamba hapa Nchini? Ni vipi huyu Mwamba unaweza kusema anatumika na CCM? Hivi kweli huyu Mbowe aliyetupa taabu wana CCM kuvaa sare zetu na kukatisha pale Mwanjera Mbeya na kuanza kuzomewa useme leo anatumika na CCM? Huyu Mbowe aliyekaa mahabusu kuliko mwenyekiti yeyote yule wa upinzani leo hii useme anatumika na CCM?
Huyu huyu Mbowe Aliyetumia rasilimali zake kwa hali na mali kuijenga CHADEMA leo useme anatumika na CCM? Hivi unayesema hivyo una akili kichwani mwako kweli? Unajua mateso aliyopitia huyu Mwamba? Unajua hasara na vitu alivyopoteza kwa ajili ya CHADEMA? Unafahamu marafiki aliopoteza na kukimbiwa na kusalitiwa kwa yeye kuendelea kuwa na misimamo yake ya kuitumikia CHADEMA? Unajua maumivu na majeraha aliyopata kwa ajili ya Kuitesekea CHADEMA?
Tukubali tukatae .lakini ukweli utabakia kuwa wana CHADEMA wapo sahihi kabisa kumpigia magoti Mwamba na kumuomba Agombee uenyekiti.wana CHADEMA wanajua nafasi hiyo ni ya msalaba na mwenye uwezo wa kubeba msalaba huo wa mateso ni huyu Mwamba na Jabali wa siasa za Upinzani hapa Nchini Mheshimiwa Freeman Mbowe ambaye wanajua hawezi watelekeza wala wakimbia wala kuutua au kuubwaga chini msalaba na kukimbia Nchi.Ndio maana wana CHADEMA wameamua hadi kumchangia pesa kwa ajili ya kuchukulia Fomu.
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.