Mbowe ametumia ujana wake wote kuitesekea CHADEMA kwa jasho na machozi

wacha mdomo wake na makelele yake yamnyooshe sasa automatically, ili aianze 2025 bila cheo lakini pia ugombeaji urasi kupitia chadema asahau kabisa yaani..
Ule mdomo wake umemponza sana na ukurupukaji wake. Michango yenyewe ya Gari imeshindikana kupatikana halafu leo eti anataka kutunishiana misuli na Mwamba na Jabali la siasa za Upinzani hapa Nchini
 
nimefanikiwa kunyukana na mwenzako tlaatlaah kwa wakati mmoja ila nyuzi tofauti. Mnafanana nyuzi zenu kumshadidia mbowe na kumbondea lissu huku nyie nyote mkionekana ni ccm kindakindaki mnaoandika upupu
Umenyukanaje naye? Unaelewa maana ya kunyukana.
 
Mwl Nyerere aliondoka mwenyewe kwenye utumishi uliotukuka Ikulu kwa 24 (years). Akaita kung'atuka, msemo maarufu hata leo. Nasi tungeiga nyayo zake. Usultani wa kufia madarakani wa akina Mugabe, Museveni na Kagame ni kutojiamini na labda kulinda maovu yako madarakani. Hata ukomo wa uongozi wa miaka 10 Tanzania ni juhudi za Mwl Nyerere.
 
Mitano Tena ni kauli mbiu ya CHURA KIZIWI,huko CCM
 
Nkimsikiliza mboe ktk press zake ni kama namsikiliza JOAN MWAIPAJA akiwa insta live
 
Subiri Mwamba achukue uongozi kwa ajili ya kukivusha chama hapo Mwakani na kuendelea kukijenga na kukipeleka kwa wananchi zaidi
 
Ama kweli ukiona adui yako akikusifia jiangalie mara mbilimbili wapi umekosea!!?
 
Subiri Mwamba achukue uongozi kwa ajili ya kukivusha chama hapo Mwakani na kuendelea kukijenga na kukipeleka kwa wananchi zaidi
angalia sana usije ukabadili id kwa aibu endapo mbowe atachukua fomu kuchuana na mama kwenye uchaguzi mkuu ujao. Utaandika nini, si utaonekana mwehu kumsigina mbowe wakati ulishampamba?
 
Ule mdomo wake umemponza sana na ukurupukaji wake. Michango yenyewe ya Gari imeshindikana kupatikana halafu leo eti anataka kutunishiana misuli na Mwamba na Jabali la siasa za Upinzani hapa Nchini
tuombe uzima tufike mwaka kesho tuone utaandika nini endapo mbowe atagombea urais against mama
 
Mama atapita bila kupingwa Mwakani.
labda kina lissu wasigombee kupitia huko kwingine, je unaonaje kusiwe na kampeni kwa urais kwa mama kwa kuwa atapita bila kupingwa halafu hela za kampeni zake mkajenge nyumba za walimu vijijini?
 
labda kina lissu wasigombee kupitia huko kwingine, je unaonaje kusiwe na kampeni kwa urais kwa mama kwa kuwa atapita bila kupingwa halafu hela za kampeni zake mkajenge nyumba za walimu vijijini?
Lissu hana sifa za kugombea Urais
 
Lissu hana sifa za kugombea Urais
Toa angalau sababu tatu tu,, kwa nini Mbowe (Chadema) unampenda unampigania awe mwenyekiti na Lissu humpendi unamkashifu asiwe mwenyekiti (Chadema) na wote ni washindani/wapinzani wa CCM. Na yeyote akigombea na akashinda urais wa Tanzania wewe mwana ccm utafaidika na nini na wakati sio mwana Chadema.
 
TISS inatumika kama jumuiya ya ndani ya CCM.
Huu ushuzi uliouandika ni ushahidi namna gani mfumo na dola yote kuwekeza mapandikizi ndani ya vyama vya upinzani

Nilishasema awali, CCM inafutwa kwa kasi sana na anayefanyakazi hiyo ni Mungu mwenyewe. Jambo la kwanza amewaondolea watawala ufahamu, hekima na kuondoa kauli ndani ya ndimi zao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…