Pre GE2025 Mbowe amvaa Dkt. Slaa kisa Tundu Lissu, adai "mpiga debe wa CCM hapaswi kutufundisha CHADEMA"

Pre GE2025 Mbowe amvaa Dkt. Slaa kisa Tundu Lissu, adai "mpiga debe wa CCM hapaswi kutufundisha CHADEMA"

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
"Tunaona watu ambao walishaondoka CHADEMA huko miaka ya nyuma kama akina Dkt Wilbroad Slaa ambao walikimbia CHADEMA wakaenda Chama cha Mapinduzi wakapewa na zawadi ya ubalozi, eti leo naye amekuwa ndiye mpiga debe mkubwa wa Makamu Mwenyekiti wangu kutaka apewe Mwenyekiti wa chama na kubeza na kutweza watu na wengine wa vyama vingine vya upinzani"- Freeman Mbowe, Mwenyekiti CHADEMA
View attachment 3197182
View attachment 3197312
Soma, Pia

Freeman Mbowe: Dkt. Slaa na wanaojiita Tanzania Diaspora wanapanga kufanya mapinduzi ndani ya CHADEMA

Willibrod Slaa: Anachopigania Tundu Lissu ni kuisafisha CHADEMA
Slaa aliupata upadre kwa bahati mbaya tusimlaumu sana
 
Mkuu ameshindwa kujibu hoja za msingi anatafuta public sympathy, kajixhokea tu.
Kwanini wengine wa CCM wakimuunga mkono Mbowe inasemwa amehongwa, lakini Lissu akiungwa mkono na Dk. Slaa na Mch. Msigwa (wote CCM) inaonekana ni sawa?

Hivi mnafikiri kuna mtu mwenye akili timamu mnaweza kumlaghai hapo?
 
"Tunaona watu ambao walishaondoka CHADEMA huko miaka ya nyuma kama akina Dkt Wilbroad Slaa ambao walikimbia CHADEMA wakaenda Chama cha Mapinduzi wakapewa na zawadi ya ubalozi, eti leo naye amekuwa ndiye mpiga debe mkubwa wa Makamu Mwenyekiti wangu kutaka apewe Mwenyekiti wa chama na kubeza na kutweza watu na wengine wa vyama vingine vya upinzani"- Freeman Mbowe, Mwenyekiti CHADEMA
View attachment 3197182
View attachment 3197312
Soma, Pia

Freeman Mbowe: Dkt. Slaa na wanaojiita Tanzania Diaspora wanapanga kufanya mapinduzi ndani ya CHADEMA

Willibrod Slaa: Anachopigania Tundu Lissu ni kuisafisha CHADEMA
Hivi mbona wakati wa uchaguzi mkuu kura mnaomba mpaka wanaccm? Huu unafiki wa Hali ya juu
 
Lakini kwenye field Mbowe ndo mpiga debe wa ccm kuliko huyo Slaaaa ambae Kwa Sasa ccm yenyewe haitaki hata kumsikia.
 
Kwani ulikuwa unasikia Radio gani au TV gani wewe? Nimemsikia Mbowe mwanzo mwisho.

Amekidhi haja kwa majibu yake. Composed, not emotional and very wise

..Na hilo ndio tatizo lake kubwa.

..kutokuwa emotional wakati wa dhuluma inajenga picha kwamba mhusika hajali.

..tabia hiyo ndiyo inayowakera wanachama na kuamua kwenda na Tundu Lissu.
 
Back
Top Bottom