Mbowe anakosa sifa muhimu ya kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA. Ajiuzulu nafasi yake kwa maslahi ya chama na Taifa kwa ujumla

Imewaumiza sana. Hivi wewe Stroke ndio mwiguru nini?. Mnamuogopa Mbowe mno. Imekula kwako na bado sana ataendelea kuwa mwenyekiti.
 
Labda kwa maslahi yako binafsi.
 
Kama ambavyo hakuna mahakama iliyomhukumu.
 
Kama ambavyo hakuna inayosema ni gaidi.
 
Kwa hyo mandela nae angekosa sifa kuwa mwenyekiti na rais wa ANC
 
Unafanana sana na mashahidi wa mchongo.
 
Kwani Mbowe ndiye kakimbia mahakama?

Na je wewe kama mwanasheria tuambie tafsiri ya serikali kuweka mpira kwapani maana hapa unaelekea kutupotosha.
 
Hebu acha makelele pumzika mkuu, inaonekana umeumia sana hadi kutuandikia waraka, hukutegemea kama angeachiwa, ndio kashaachiwa na ataendelea kua mwenyekiti wao Chadema, ajiuzulu what for?

Sent from my vivo X6D using JamiiForums mobile app
Ujinga mtupu!
Kwa hiyo na CDM wakimtuhumu Bibi Mikopo kuwa ni gaidi na yeye ajiuzulu?
Kila mwenye akili anajua ile kesi ni ya UONGO, ya kisiasa, ya kughushi!
 
Kwa hiyo ukaona suluhisho ajiuzulu tu kwa sababu hakusafishwa.
 
ndugu Stroke linapokuja suala la kumsema MBOWE jiuzulu au kumsema vibaya mbowe utakula matusi yasiyo na idadi wafuasi wa mbowe nisawa kabisa na wafuasi wa MWAMPOSA au wa MFALME ZUMARIDI yaani hawajulkikani kama wana akili sawasawa au hawana akili kabisa wao ni kuropoka tu na kupandisha mashetani kama wale misukule wa zumaridi waache watakuharibia siku bure
 
Ugaid
I
Ugaidi aliutenda Magufuri kuua Wazanzibar wasio na hatia alaaniwe ahera na duniani.

Ugaidi aluutenda Mkapa kwa kuwaua wazanzibari wasiohatia, alijutia akaishia kuandika kitabu akijilaumu,

ikiwa alifanya toba ya kweli mbali ya kujilaumu, mwenyezi Mungu ampunguzie adhabu ya kaburi.

Haya tueleze ugaidi wa Mbowe amemdhuru nani?

Ccm imeongoza mauaji mangapi kwa wapinzani (hawajawa Magaidi)
Chadema wamelipa hata moja?!(Magaidi)
Siku wakilipa pengine mtawaita nani?
 
Sukuma gang hawajuagi sheria wanaamini katika manguvu tu!
 
Tuhuma siyo hatia ata Rais anatuhumiwa na wananchi kuiba kura lakini hakuna mahakama yoyote ambayo imetia hatiani kwa hiyo tuhuma unaweza kutuhumiwa mda wowote na mtu yoyote lakini utabaki kuwa mtakatifu mpaka pale utakapotiwa hatiani.Mandela alitiwa hatiani na akafungwa na bado alipotoka waafrika kusini walimchagua kuwa Rais.hii inaonyesha uwezo wako mdogo wa maswala ya kisiasa na maswala ya kisheria. Hata kama Mbowe angetiwa hatiani kwa kesi hii bado ulimwengu mzima ungepiga kelele aachiwe na bado angeendelea na harakati za siasa.Tuhuma ni tuhuma na pia hata mtu akitiwa hatiani bado Watu wanaangalia je amefungwa kwa haki au kwa mapungufu ya kisheria.
 
Wewe Ni wakala wa shetani na pia nimpiga ramli chonganishi nendeni mkatambike kwenye Kaburi ya dikteta uchwara na Mungu wa chaltle
 
Kuna tofauti kati ya tuhuma za mitaani na tuhuma ambazo zipo kwa kufuata utaratibu.

Jambo likishakuwa mahakamani linakuwa recorded.

Sasa rekodi za mahakama kuu ya Tanzania zinasema kwamba Mbowe alikutwa na kesi ya kujibu katika tuhuma za ugaidi.

Hakuna rekodi nyingine tofauti na hiyo.

Itoshe kusema kwamba Mbowe na Chadema nzima wamepigwa knock out na serikali ya CCM.
 

Hiyo mahakama Ingekuwa na heshima hiyo wangalau ungekuwa na point ya maana. Hata walioitoa hiyo kesi mahakamani wanajua hakukua na kesi bali siasa chafu ndani ya mahakama. Na kwa taarifa yako hiyo mahakama Ingekuwa huru, hiyo kesi wala isingevuka kwenye zile kesi ndogo ndani ya kesi. Labda hii porojo yako ukawape watu wa huko porini wenye uelewa mdogo ww mambo.
 
Pia ufahamu ya kuwa ushahidi wa utetezi nao upo palepale hata mkimfufua kayafa maana yeye ndiye mwl.wenu wa Chuki.
 
Matatizo yenu ndio hayo siku zote mnafanya maamuzi kwa hisia na kupenda kusikia mnayotaka kusikia kwa aina hiyo ya siasa mtaendelea kubakia wanaharakati siku zote.

CCM itaendelea kuwaburuza kwa muda mrefu ujao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…