Uchaguzi 2020 Mbowe anavyomfitini Tundu Lissu, Nyalandu ashinda kura za maoni

Ila lisu kwa sasa asinge chukua fomu ya uraisi kwasasa U PM utamfaa sana
 
Mleta mada mbona hujaweka hizo charts manadiki mkubwa unataka gombanisha watu sio ndo ulivyo tumwa? Mataga bana[emoji23][emoji23]
 
Mleta uzi huu kama ni mwanamume anataka kutufanya tuamini kuwa Mungu anafanya makosa......!!!!!!

Sijui kama atanielewa hapa, kama hajanielewa, tafadhali mtafsirieni.
 
Binafsi Lissu asipopewa nafasi ya kugombea. Naachana na Chadema rasmi
Tundu Lissu hata akipitishwa atakusaidia nini, huo ni ubinafsi wa Kisiasa.
Kwanza Lissu ana Kesi mahakamani na bado haijaamuliwa akipigwa ban ya 40yrs.

Nyongeza: Nina Kusudia Kumfungulia Kesi Tundu Lissu ya Kuidhalilisha nchi yetu Umoja wa Mataifa.
Na Kesi nitaitem sehemu ya uhujumu Uchumi maana aliathilii mpaka shughuli za utalii na kusababisha vijana kukosa ajira
 
Kwa kifupi ni kuwa kila jinabla mtia nia lilikuwa na Ndiyo au Hapana. So kwenye jina la Nyalandu wajumbe wote wali tick Ndiyo (28 out of 28 =100%; Jina la Lissu, wajumbe 24 waliweka Ndiyo, wanne Hapana, n.k
 
Hizo hesabu sijazifahamu, kura 28 kati ya kura 28 alizopata Nyalandu maana yake ni asilomia 100, sasa hizo za Lissu 24 kazipata wapi?
 
kuna wagombea ubunge na madiwani wengi wa CHADEMA hawana uwezo wa kuendesha kampeni , unadhani bila msaada kutoka kwa Nyalandu watashindaje? Nyalandu ndio tegemeo pekee la CHADEMA kwenye kugharamia uchaguzi
Leo laki si pesa unaitetea chadema?? Kwamba unaipenda au?? Maajabu duniani hayataisha
 
kuna wagombea ubunge na madiwani wengi wa CHADEMA hawana uwezo wa kuendesha kampeni , unadhani bila msaada kutoka kwa Nyalandu watashindaje? Nyalandu ndio tegemeo pekee la CHADEMA kwenye kugharamia uchaguzi
Huo utopolo wako, kapeleke kule Lumumba, mchumiatumbo mkubwa!!!!
 
Kama hayo matokeo ni ya kweli na maelezo kuwa Mbowe na Lema wamemnyima kura Lissu, basi kuanzia leo, nitawaheshimu sana Lema na Mbowe kwa kuona mbele.
Mwezi Oktaba mwaka huu, Rais atakayetangazwa ni Magufuli. Awe ameshinda au ameshindwa, Magufuli atatangazwa kuwa mshindi na Tume ya Uchaguzi, aliyoichagua yeye mwenyewe.
Nafasi sahihi ya Upinzani kutwaa dola ni mwaka 2025.
Wagombea Urais wa Serikali ya Muungano mwaka huu, watakuwa wasindikizaji tu.
Upinzani ujipange kumsaidia Maalim Seif Shariff Hamad Zanzibar baada ya kufikia makubaliano ya pamoja.
Makubaliano ni muhimu ili Zanzibar iwe chachu ya Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi.
Katika miaka mitano ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar, 2010 - 2015, Maalim Seif Sharif Hamad na wenzake akina Duni Haji walijisahau kushughulikia Tume Huru ya Uchaguzi, matokeo yake wakakipata cha moto kwenye Uchaguzi wa 2015.
Huku Tanzania Bara namuona Membe akiwa na nafasi ya kuongea mambo mengi kwenye jukwaa yanayoweza kurekebisha baadhi ya ubabe wa Magufuli.
Tundu Lissu ni kete muhimu sana ya Upinzani 2025.
Hongera sana Mbowe na Lena kwa kuliona hilo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…