Uchaguzi 2020 Mbowe anavyomfitini Tundu Lissu, Nyalandu ashinda kura za maoni

Uchaguzi 2020 Mbowe anavyomfitini Tundu Lissu, Nyalandu ashinda kura za maoni

Tusha kugundua nia yako ni ipi juu ya kutaka Membe aungwe mkono na cdm ili agombee yeye.

Ungtaka hivyo ungetumia njia za kiungwana kuliko kuwananga na kuwaona viongozi wa cdm kuwa hawaelewi majukumu yao kichama.

Kwa taarifa yako ni kuwa viongozi wa cdm wanajua nini wanafanya na hata hao wagombea awe Lissu awe Nyalandu wanelewa nini kinafanyika huko kwenye kamati kuu.
Tatizo unaleta vitu personal katika mada.
Mada imehoji suali la msingi.

Mada inahoji maamuzi ya kamati kuu ya Chadema juu ya kumpa kura nyingi Nyalandu kuliko Lissu.

Wewe unaleta mambo ya vyama vingine.

Mimi siyo ACT, mimi namkubali Bernad Membe au Lissu, haijalishi kama hao watu wangegombea kupitia CCM, ACT au CHAUMA mimi niko nao!

Inaniuma kuona Uongozi wa CHADEMA unamuona Nyalandu ni bora kuliko Lissu.

Naamini Tatizo la nchi hii ni Jiwe, kwa hiyo mtu au taasisi yoyote inayomkwaza mtu mwenye chance za kumg'oa Jiwe, hiyo taasisi lazima niinyoshee kidole!

That is my point!
 
Misile nilikiwa nakuheshimu sana lakini leo umeonesha uwezo mdogo wa kung'amua Mambo. Kilichofanywa na Chadema ni camouflage. Yaani Diversion. Ktk maswala ya inteligensia ni aina fulani ya kumpoteza mwelekeo adui adhani A ni B kumbe A ni A tu .
Nadhani umenielewa.
Kwa akili yako unafikiri sasa pale kuna kisichojukikana hapo chadema?
 
Chadema hawana shida na Rais Ila wanataka kiongozi wa chama awe wakwao Wana sacos na kichaga tundulisu hawawez mpa Kwan wanajua baadae ataenda kua na nguvu na sacos kuibwa [emoji23][emoji23][emoji23]so wanaona ni Bora nyalandu
 
kuna wagombea ubunge na madiwani wengi wa CHADEMA hawana uwezo wa kuendesha kampeni , unadhani bila msaada kutoka kwa Nyalandu watashindaje? Nyalandu ndio tegemeo pekee la CHADEMA kwenye kugharamia uchaguzi

Kama ni hivyo kuwa cdm inategemea nguvu ya Nyalandu, hiyo itakuwa cdm au chama cha Nyalandu? Mimi sio muumini wa chama cha Nyalandu, ndio maana simsomi.
 
Lisu ana ushawishi kwako, lakini kwa wenye chama hana ushawishi, huo ndio ukweli, Nyalandu ni smart ana connection ulaya huko anao uwezo wa kufadhili kampeni zote za CHADEMA kuanzia udiwani, ubunge mpaka urais, unadhani Mbowe na wabunge wataacha kumuunga mkono

Uko sahihi sana kuwa ana ushawishi kwa wenye chama, ila wapiga kura ni sisi. Na sisi wapiga kura tulio wengi wa upinzani, hatuko tayari kurudia kosa la Lowassa fullstop.
 
Kifupi ni kwamba Nyalandu ana pesa kuliko Lisu hayo mengine ni jalamba tu
Mchakato ndani ya kamati kuu ndani ya Chadema umekamilika ambapo kamati kuu ya Chama hicho imechagua watu watatu kwenda kwenye baraza kuu la Chama.
Katika kura zilizopigwa ndani ya kamati kuu, Ndugu Nyalandu amepata kura nyingi zaidi kuliko Lissu.

Hata hivyo tafsiri ya kura hizi ni kuwa Kamati kuu ya Chadema ambayo ndiyo uongozi wa Chadema hauamini kuwa Lissu ni mgombea bora kuliko Nyalandu.

Yaani kamati kuu ya Chadema kiufupi haiamini kuwa Ndugu Tundu Lissu anaweza kuwa rais mzuri kuliko ndugu Lazaro Nyalandu.

Hii maana yake ni kwamba Uongozi wa Chadema, umetuma Meseji kwa Wanachadema na Watanzania kuwa, Uongozi huo ungependa ndugu Nyalandu ndiye awe mpeperusha bendera ya chama hicho dhidi ya Rais Magufuli.

Sasa ni jukumu letu sisi wananchi kuanza kujiuliza, kuwa Uongozi wa Chadema umeona kasoro gani kwa Tundu Lissu hadi usiamini kuwa yeye ndiye anayefaa zaidi kuwa mgombea kuliko mwanachama yeyote wa CHADEMA katika waliotia nia?

Huenda uongozi wa Chadema una kitu ulichokiona kwa ndugu Lissu kiasi kwamba kupitia kura zao unatuma meseji kwetu kuwa Lissu si bora kuliko Nyalandu. Je ni kitu gani hicho?

Mimi nafikiri kuwa yule aliyeko jikoni ndiye anayejua joto lililoko huko, Sasa kama Uongozi wa juu wa Chadema haumuoni Lissu kama namba moja, je ni sahihi sisi kuanza kumuona kuwa ni mtu sahihi?

Nadhani maamuzi haya ya kamati kuu ni mawazo ya kutufikirisha sana sisi wapiga kura. Hii ni. meseji ya dhahiri kwetu kutoka kwa uongozi wa CHADEMA kuwa, kwenye uchaguzi huu ujao, miongoni mwa wagombea, uongozi huo unaamini kuwa kuna mtu ndani ya Chadema na nchi hii mwenye sifa zaidi kuliko Lissu anayepaswa kuwa raisi La sivyo kwa nini haukumpa kura nyingi zaidi Lissu kushinda wengine?

Tutafakari!
 
wafuatao.

1. Freeman Mbowe.
2. Godbless Lema.
3. Halima Mdee.
4. Esther Bulaya
mkuu umeandika idadi ya wajumbe 29 sasa hesabu zako hazieleweki:

nyalandu 28
Lissu. 24
Dr mayrose23
Jumla kura zote 77
Umeandika upuuzi
Wapiga kura 28 walipewa karatasi 28 zikiwa na majina 8. Kila mpiga kura alitakiwa aweke TICK ✓ kwenye majina matatu tu. Karatasi zilipokusanywa Nyalandu alikuwa na TICK ✓ 28 Kutoka kwa wote. Lissu alikuwa na TICK ✓ 24 kutoka kwa hao 24 Kati ya 28. Na mwingine jina silijui alikuwa na TICK ✓ 23 kutoka kwa hao 23 Kati ya 28. Kumbuka walitakiwa wapatikane tatu bora Kati ya 8. Umeelewa!??
 
Unatakiwa kushtakiwa kwa kuhujumu uchumi wa chama. Kula buku saba bila kufanya chochote
 
We jamaa ulisoma hata hesabu ya vidudu?
Wapiga kura 28 walipewa karatasi 28 zikiwa na majina 8. Kila mpiga kura alitakiwa aweke TICK ✓ kwenye majina matatu tu. Karatasi zilipokusanywa Nyalandu alikuwa na TICK ✓ 28 Kutoka kwa wote. Lissu alikuwa na TICK ✓ 24 kutoka kwa hao 24 Kati ya 28. Na mwingine jina silijui alikuwa na TICK ✓ 23 kutoka kwa hao 23 Kati ya 28. Kumbuka walitakiwa wapatikane tatu bora Kati ya 8. Umeelewa!??
 
Yaani wafuasi wa Lissu ? Nyalandu mwenyewe kadhibitisha kwenye interview na Jenerali kuwa yeye amepata kura nyingi zaidi ya Lissu kamati kuu. Kaangalieni hiyo interview ameongea mambo mengi mazuri kwa Tz akipewa fursa. Nimegundua anaweza kuwa mgombea bora zaidi ya Lissu. Ubora wa Lissu ni tukio lililompata! Nashangaa kivipi ACT na Member wanasemwa eti wanaihujumu Chadema! Teh teh teh
 
Kila mjumbe alipiga kura tatu.
Nyalandu 28
Lissu 24
Majige 23
Iliyoharibika 1
TOTAL 76
Kila mjumbe alipiga kura 3,29×3=87
87-76=11,hizi kura zilienda kwa nani?
Nadhani kati ya kichwa chako na vidole,kuna kimoja hakikuwa na ushirikiano na mwenzake wakati unaformulate huu utopolo
 
Hivi Nyalandu karudisha Kdi ya CCM kama Membe?
Nauliza tuu
 
Back
Top Bottom