Mchakato ndani ya kamati kuu ndani ya Chadema umekamilika ambapo kamati kuu ya Chama hicho imechagua watu watatu kwenda kwenye baraza kuu la Chama.
Katika kura zilizopigwa ndani ya kamati kuu, Ndugu Nyalandu amepata kura nyingi zaidi kuliko Lissu.
Hata hivyo tafsiri ya kura hizi ni kuwa Kamati kuu ya Chadema ambayo ndiyo uongozi wa Chadema hauamini kuwa Lissu ni mgombea bora kuliko Nyalandu.
Yaani kamati kuu ya Chadema kiufupi haiamini kuwa Ndugu Tundu Lissu anaweza kuwa rais mzuri kuliko ndugu Lazaro Nyalandu.
Hii maana yake ni kwamba Uongozi wa Chadema, umetuma Meseji kwa Wanachadema na Watanzania kuwa, Uongozi huo ungependa ndugu Nyalandu ndiye awe mpeperusha bendera ya chama hicho dhidi ya Rais Magufuli.
Sasa ni jukumu letu sisi wananchi kuanza kujiuliza, kuwa Uongozi wa Chadema umeona kasoro gani kwa Tundu Lissu hadi usiamini kuwa yeye ndiye anayefaa zaidi kuwa mgombea kuliko mwanachama yeyote wa CHADEMA katika waliotia nia?
Huenda uongozi wa Chadema una kitu ulichokiona kwa ndugu Lissu kiasi kwamba kupitia kura zao unatuma meseji kwetu kuwa Lissu si bora kuliko Nyalandu. Je ni kitu gani hicho?
Mimi nafikiri kuwa yule aliyeko jikoni ndiye anayejua joto lililoko huko, Sasa kama Uongozi wa juu wa Chadema haumuoni Lissu kama namba moja, je ni sahihi sisi kuanza kumuona kuwa ni mtu sahihi?
Nadhani maamuzi haya ya kamati kuu ni mawazo ya kutufikirisha sana sisi wapiga kura. Hii ni. meseji ya dhahiri kwetu kutoka kwa uongozi wa CHADEMA kuwa, kwenye uchaguzi huu ujao, miongoni mwa wagombea, uongozi huo unaamini kuwa kuna mtu ndani ya Chadema na nchi hii mwenye sifa zaidi kuliko Lissu anayepaswa kuwa raisi La sivyo kwa nini haukumpa kura nyingi zaidi Lissu kushinda wengine?
Tutafakari!