Uchaguzi 2020 Mbowe anavyomfitini Tundu Lissu, Nyalandu ashinda kura za maoni

Uchaguzi 2020 Mbowe anavyomfitini Tundu Lissu, Nyalandu ashinda kura za maoni

Kwitululu

Member
Joined
Mar 30, 2020
Posts
62
Reaction score
124
Ndugu wana bodi.

Kupitia vyanzo vyangu makini vya kimtandao nimepokea taarifa kuwa kamati kuu ya CHADEMA imefanya uamuzi kwa kupiga kura. Uamuzi wa kupendekeza nani awe mpeperusha bendera mkuu wa CHADEMA katika uchaguzi wa mwaka huu 2020. Yaani mgombea Urais.

Ukweli ni kwamba kati ya watu 8 waliorudisha fomu ni watu wawili tu wenye ushindani.
1. Mh Tundu Lissu
2. Mh Lazaro Nyalandu.

Hawa wote ni wenyeji wa mkoa wa Singida na wote ni wajumbe wa kamati kuu ya chadema taifa.

Binafsi nilishitushwa sana kiasi cha kubadilisha mapigo ya moyo wangu baada ya kuona matokeo ya kura za maoni za kamati kuu ya CHADEMA.

Kilichonishitua ni kuona ``think tank`` ya CHADEMA inaamini Mhe Lazaro Nyalandu ni bora kuliko Mhe Tundu Lissu aliyekinga chama kwa damu yake na risasi 16 ambazo mpaka sasa hatujajua Kama kweli zilikuwa zinampiga au malaika walitega migongo yao ndio ikapigwa lisasi kwa niaba yake? Kwasababu mpaka sasa watanzania na wanachadema bado wanajiuliza huyu jamaa aliponaje!!

Bila kutia chumvi yafuatayo ni matokeo ya tatu bora za maoni ya kamati kuu ya CHADEMA

KURA ZA WAGOMBEA URAIS JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

KAMA ZILIVYOPIGWA NA KAMATI KUU YA CHADEMA, DAR ES SALAAM, JULY 22, 2020

*IDADI YA KURA ZILIZOPIGWA - 29*
*KURA ILIYOHARIBIKA - 1*
*IDADI YA KURA HALALI -28*

*Lazaro S. Nyalandu - 28* ( 100%)
*Tundu Antipasi Lissu - 24* (86%)
*Dr. Mayrose K. Majinge - 23* ( 82%)

Haya ndiyo majina yatakayo kwenda Baraza Kuu la CHADEMA.

Baada ya matokeo haya nikaanza upelelezi kujua nini kimejiri Kaka Tundu Lissu azidiwe kura na mh Lazaro Nyalandu.

Uchunguzi wangu umebaini kuwa Mhe Aikael Mbowe na Nduguye Mhe Godbless Lema ndiyo walikua nyuma kuhakikisha kuwa Lazaro Nyalandu anamzidi kura za maoni Mhe Tundu Lissu katika maoni ya Kamati kuu.

Kwa ufupi naambatanisha chat za Whatsapp kati ya Mhe Lema na Mhe Mbowe baada ya matokeo ya kura hizo.

Na nina ushahidi thabiti watu wanne waliomnyima kura Lissu ni wafuatao.

1. Freeman Mbowe.
2. Godbless Lema.
3. Halima Mdee.
4. Esther Bulaya.

Pia nichukue wasaa huu kuwajulisha Mhe Esther Matiko na kaka Patrick Ole Sosopi kuwa makini katika siasa zao ndani ya chadema Mwamba hawatazami kwa jicho rafiki.

Wajumbe wa baraza kuu na mkutano mkuu wa chadema taifa wanaopinga mpango wa Mwamba kumuunga mkono Lazaro Nyarandu na ambao wanamuunga mkono mh Tundu lissu,mjiandae pia kisaikolojia yajayo yanafurahisha.

Sasa nimeanza kuamini kwanini wanachama wa chadema na viongozi wengi walikuwa wanatimkia vyama vya Nccr mageuzi na ccm wakisema Kuna tatizo naona sasa linaanza kuwa dhahiri machoni kwa watanzania na wanachama wa chadema.

Ni wenu.
 
CCM mlianza na vitisho vya kumzuia Lissu asije Tanzania mkafeli, mkaja na thread za Lissu kukamatwa akifika mkafeli, mkaja na thread za Membe kugombea na sio Lissu mkafeli sasa mnakuja na thread za Mbowe na Lissu.

Nawaambieni Lissu ni mpango wa Mungu. Ni bora mkakaa muda huu kujipanga mtakiendeshaje Chama chenu baada ya Lissu kukabidhiwa nchi na serikali na watanzania hapo October 2020.

Mtake msitake Lissu ndo raisi wenu hapo October 2020.
 
Duuu....yajayo yanafurahisha....

huu unaweza kuwa uchangonishi.....umetaja majina ya wachaga tu, Bulaya umemweka ili kufukia dhamira yako ovu ya ukabila.


hizo kura zilipigwajepigwaje, maana wajumbe 29, mara mwingine 28, mwingine 24, sijaelewa kabisaaa...
 
Duuu....yajayo yanafurahisha....

huu unaweza kuwa uchangonishi.....umetaja majina ya wachaga tu, Bulaya umemweka ili kufukia dhamira yako ovu ya ukabila.


hizo kura zilipigwajepigwaje, maana wajumbe 29, mara mwingine 28, mwingine 24, sijaelewa kabisaaa...
Kila mjumbe alipiga kura tatu.
 
CCM mlianza na vitisho vya kumzuia Lisse asije Tanzania mkafeli, mkaja na thread za Lissu kukamatwa akifika mkafeli, mkaja na thread za Membe kugombea na sio Lissu mkafeli sasa mnakuja na thread za Mbowe na Lissu.

Nawaambieni Lissu ni mpango wa Mungu. Ni bora mkaa muda huu kujipanga mtakiendeshaje Chama chenu baada ya Lissu kukabidhiwa nchi na serikali na watanzania hapo October 2020.

Mtakuwa msitake Lissu ndo raisi wenu hapo October 2020.




Hii habari ya kusema mpango wa Mungu sio nzuri.......,mnamfanyaga kuwa Mungu ni mwongo....hata Lowasa mlidai mpango wa Mungu......kiko wapi....yuko wapi? Mungu gani labda?
 
Back
Top Bottom