benzemah
JF-Expert Member
- Nov 19, 2014
- 1,533
- 3,187
Sote tunakumbuka katika mkutano wa kwanza wa tangu kuruhusiwa tena kwa mikutano ya kisiasa nchini, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Aikaeli Mbowe, alitumia muda mrefu sana kumshukuru na kumuongelea Rais Samia Suluhu Hassam, maswali yalikuwa mengi miongoni mwa wana-CHADEMA na Watanzania wanaofuatilia siasa lakini hilo lilipita.
Baada ya Mikutano kadhaa, CHADEMA wamefika kwenye moja ya maeneo ambayo wamekuwa na wafuasi wengi kiasi, huko TUNDUMA mkoa wa MBEYA ambapo hapa napo Mwenyekiti Mbowe amemwagia sifa Rais Samia kwa kuruhusu mikutano ya hadhara ambayo ameeleza kuwa ina tija si tu kwa wanachama wa chama chake bali pia kwa wananchi wote. Pia Mbowe amelitaka amelipongeza Jeshi la Polisi kwa kusimamia amani ya nchi kwa kuilinda mikutano yao bila kutumia nguvu.
Je, Mwenyekiti Mbowe kuendelea kutumia majukwaa ya CHADEMA kumpongeza na kumshukuru Rais Samia ni sawa.? na je tunajifunza nini kwa anayoyafanya Mbowe?