Mbowe anavyozidi kumshukuru Rais Samia tunajifunza nini?

Sote tunakumbuka katika mkutano wa kwanza wa tangu kuruhusiwa tena kwa mikutano ya kisiasa nchini, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Aikaeli Mbowe, alitumia muda mrefu sana kumshukuru na kumuongelea Rais Samia Suluhu Hassam, maswali yalikuwa mengi miongoni mwa wana-CHADEMA na Watanzania wanaofuatilia siasa lakini hilo lilipita.

Baada ya Mikutano kadhaa, CHADEMA wamefika kwenye moja ya maeneo ambayo wamekuwa na wafuasi wengi kiasi, huko TUNDUMA mkoa wa MBEYA ambapo hapa napo Mwenyekiti Mbowe amemwagia sifa Rais Samia kwa kuruhusu mikutano ya hadhara ambayo ameeleza kuwa ina tija si tu kwa wanachama wa chama chake bali pia kwa wananchi wote. Pia Mbowe amelitaka amelipongeza Jeshi la Polisi kwa kusimamia amani ya nchi kwa kuilinda mikutano yao bila kutumia nguvu.

Je, Mwenyekiti Mbowe kuendelea kutumia majukwaa ya CHADEMA kumpongeza na kumshukuru Rais Samia ni sawa.? na je tunajifunza nini kwa anayoyafanya Mbowe?

View attachment 2529543
Mbowe siku hizi uwezo wake UMESHUKA sana.

Hana HOJA Kabisa.

Sijui ni UZEE au waliokuwa wanasaidia hawapo siku hizi.

Yupo kwenye deteriorating mode.

Hata kina Sugu, Msigwa na Mnyika hawana hoja.

Mara nyingi wanaongea wakiwa mitumbo mikubwa wanahrmea juu juu Kama wanataka kuanguka.

Sasa hivi CDM inategemeana umaarufu tu. Hoja HAKUNA
 
Hebu tupe wazo lako alitakiwa afanyeje? Akidiss uongoz itakua CDM wana kauli mbaya, wakisema ukwel hata kama unauma wataambiwa waseme kwa stara, wakizungumza wanachokiamin wanaambiwa wana vurugu hawaitakii amani nchi yetu!! Sasa hapa kutoa pongezi nalo linajadiliwa.... This is bongo nyoso!!
 
Labda rais atawaingiza Chadema katika serikali. Nakumbuka wakati wa Bill Clinton,waziri wa ulinzi alikuwa Republican. Hapa sidhani mpinzani anaweza kupewa cheo kikubwa,lakini the only explanation kwa watu hawa kumsifu rais ni kwamba they want to keep the door open in case someone wants to approach them.
 
Sote tunakumbuka katika mkutano wa kwanza wa tangu kuruhusiwa tena kwa mikutano ya kisiasa nchini, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Aikaeli Mbowe, alitumia muda mrefu sana kumshukuru na kumuongelea Rais Samia Suluhu Hassam, maswali yalikuwa mengi miongoni mwa wana-CHADEMA na Watanzania wanaofuatilia siasa lakini hilo lilipita.

Baada ya Mikutano kadhaa, CHADEMA wamefika kwenye moja ya maeneo ambayo wamekuwa na wafuasi wengi kiasi, huko TUNDUMA mkoa wa MBEYA ambapo hapa napo Mwenyekiti Mbowe amemwagia sifa Rais Samia kwa kuruhusu mikutano ya hadhara ambayo ameeleza kuwa ina tija si tu kwa wanachama wa chama chake bali pia kwa wananchi wote. Pia Mbowe amelitaka amelipongeza Jeshi la Polisi kwa kusimamia amani ya nchi kwa kuilinda mikutano yao bila kutumia nguvu.

Je, Mwenyekiti Mbowe kuendelea kutumia majukwaa ya CHADEMA kumpongeza na kumshukuru Rais Samia ni sawa.? na je tunajifunza nini kwa anayoyafanya Mbowe?

Mkuu 'benzemeah', binafsi sioni ubaya wowote wa Mbowe kutoa shukrani kwa mazuri yanayoonekana anayeshukuriwa kayafanya, kama hilo la kuwapumzisha polisi kuwakandamiza vyama vya upinzani.
Lakini naona wewe, kama ilivyo wengi wetu tumepofushwa na hayo mazuri, na kusahau kwamba CHADEMA tayari wametekwa, kupitia kwa Mwenyekiti wao.

Inashangaza kwamba hukumbuki kutuwekea ya msingi yaliyozungumzwa kwenye mikutano hiyo (kama yapo), mbali ya hizo sifa unazosema Mbowe anazimwaga.

Hebu tueleze kuhusu hayo mengineyo yanayoihusu CHADEMA yenyewe, mbali au nje ya mazungumzo ya maafikiano yanayosemwa sana na hiki chama cha upinzani.
Ninakusikiliza mkuu.
 
Mbowe siku hizi uwezo wake UMESHUKA sana.

Hana HOJA Kabisa.

Sijui ni UZEE au waliokuwa wanasaidia hawapo siku hizi.

Yupo kwenye deteriorating mode.

Hata kina Sugu, Msigwa na Mnyika hawana hoja.

Mara nyingi wanaongea wakiwa mitumbo mikubwa wanahrmea juu juu Kama wanataka kuanguka.

Sasa hivi CDM inategemeana umaarufu tu. Hoja HAKUNA
Ninaweza kusema, bila ya woga wowote wa kujikanganya, kwamba kuna kila sababu ya Lissu kurudi alikotokea haraka haraka.
Ile CHADEMA iliyokuwepo, haipo tena.
 
Kuwa mpinzani sio kupinga kila kitu
Hata sumu inaua na kuokoa
 
Back
Top Bottom