Uchaguzi 2020 Mbowe anaweza kupata fedheha Uchaguzi huu

Joined
Jul 19, 2020
Posts
39
Reaction score
128
MBOWE ANAWEZA KUPATA FEDHEHA UCHAGUZI HUU

Na Thadei Ole Mushi

Mwaka huu Mh Mbowe kabla hata ya Kampeni kuanza alifanya mkutano mmoja kwenye Jimbo lake la Hai maeneo ya Tambarare akaulizwa Swali Moja na wakazi wa Tambarare kuwa umetufanyia nini kwa miaka kumi ya Ubunge? Swali lile hakuweza kulijibu na badala yake paliibuka vurugu kubwa hadi mkutano kuvurugika Kabisa.

Ni Mara Chache Sana kwa Mkoa wa Kilimanjaro Mbunge wa Jimbo kukaa kwa zaidi ya miaka kumi kwenye Jimbo Hilo hilo. Nilidhani Mbowe baada ya kukutana na Swali lile la umetufanyia nini angelichukua hatua mapema ya kutafuta mrithi wa Jimbo Hilo kupitia Chadema.

Kadri Muda unavyozidi kwenda asilimia za Mbowe kurudi Bungeni zinaendelea kupungua. Mfano Kura zingepigwa leo Mafue mgombea wa CCM anashinda kwa asilimia zaidi ya 60. Ukiachana na Siasa za kiitikadi watu wa Hai wana mahitaji yao ya msingi ambayo wanataka yatimizwe au yatatuliwe.

Kwenye Urais Hali ya Mambo imeshajionyesha kuwa mshindi ni JPM, Kama nilivyowaambia kuwa Kabila la wachaga ni Opportunist wanajua kabisa kuwa kumchagua Mbowe Ni kukaa nje ya Mfumo kwa miaka mingine mitano. Watakaa nje kwa miaka mitano kwa kuwa Rais Magufuli ameshatamka wazi wazi kuwa msimu huu Ni win win Situation "Nipe Nikupe".

Itakuwa Fedheha Sana Mbowe kustaafishwa Siasa kwa kushindwa kwenye box la Kura. Dalili zipo wazi kabisa hata Lissu alipokwenda Hai Mapokezi na mikutano yake haikuwa na watu wengi. Dalili nyingine ya kushindwa ni JPM kuungwa mkono na watu wenye Ushawishi Kama Askofu Shoo. Kibaya zaidi wafanyabiashara wa Hai mwaka huu wapo kimya na shughuli zao hivyo Mbowe kabakia Mwenyewe na team yake tu.

Uchagani huwa tunasema Mangi huwa hanuniwi. Mambo si marahisi Sana Hai kama ilivyozoeleka, ule upepo wa Kaka Mbowe Kama mwaka huu hauvumi. Ujio wa JPM mkoani Kilimanjaro umeibomoa kabisa Ngome ya Upinzani.

Tusubiri tuone!

Ole Mushi
0712792602
 
Nini maana ya kuweka namba za simu?
Mtu tangu 2016 yeye kila andishi lake mwishoni kunakuwa na namba!!
Mwenyezi Mungu Muumba alivyotuambia kwenye Mwanzo.

Mwanzo 3 : 16 - 19.
16.Kisha akamwambia mwanamke,
“Nitakuzidishia uchungu wa kuzaa, kwa uchungu utazaa watoto.
Hata hivyo utakuwa na hamu na mumeo,naye atakutawala.”

17.Kisha akamwambia huyo mwanamume,“Kwa kuwa wewe umemsikiliza mkeo,ukala matunda ya mti ambayo nilikuamuru usile;kwa hiyo, kwa kosa lako ardhi imelaaniwa.

Kwa jasho utajipatia humo riziki yako,
siku zote za maisha yako.

18.Ardhi itakuzalia michongoma na magugu,nawe itakubidi kula majani ya shambani.

19.Kwa jasho lako utajipatia chakula
mpaka utakaporudi udongoni ulimotwaliwa;maana wewe ni mavumbi, na mavumbini utarudi.”

Wanaume tunatakuwa tule kwa jasho,sio kubebwabebwa kama kinda la ndege.
 
..kampeni za CCM Kilimanjaro zimethibitisha kwamba Magufuli ni mbaguzi.

..Magufuli alitakiwa azungumze lugha ya upatanisho badala ya kuzungumza maneno ya vitisho, na ubaguzi.

..Wananchi walihitaji kupewa MATUMAINI, badala yake wameambulia VITISHO.
 
Sijasikia lugha za upatanisho ktk hotua za mgombea wa Chadema, ACT wala CUF. Kwaniimiwe kwa mgombea wa CCM tu?
 
Acha uongo wewe.
Wewe ndio ulikuwa kinara wa kuandika sijui CDM imekuwa mara 2020 uchaguzi mwepesi kwa CCM. Mara sijui LISSU hawez kurudi TZ akirudi anakesi liko wapi??

Saasisha huyo hata kuongea tuu jana ndio kwa mara ya kwanza kufungua mdomo utafananisha na Mbowe?
 
Polisi wenu alimwambia hawezi shinda uchaguzi! Kwa minajili hiyo polisi watakataa vipi hawahusiani na ccm pia kusimamia wizi wa kura? Samia akaenda mbali na kusema hata wakipigia upinzani kura , ccm ndio itaunda serikali ,hamuoni ccm mna mbeleko za kutosha huku mkijifariji mnakubalika wakati mikutano yenu watumishi wanapewa order kuhudhuria kwa lazima.
 
Yule polisi alimwambia ukweli mbowe

Sent from my SM-A910F using JamiiForums mobile app

Tangu lini Polisi OCD aamue kura za mgombea wa Ubunge?
Nyie subirini matokeo 28 Okt,2020 na Ole WENU: Ole Sabaya, Ole Mushi na Ole OCD matokeo yoyote kinyume na matakwa ya Wananchi Hai VIDEO YA OCD NI EVIDENCE TOSHA ITAKAYOTUMIKA ICC KUWASHUGHULIKIA!!
 
MBOWE ANAWEZA KUPATA FEDHEHA UCHAGUZI HUU

Na Thadei Ole Mushi

Mwaka huu Mh Mbowe kabla hata ya Kampeni kuanza alifanya mkutano mmoja kwenye Jimbo lake la Hai maeneo ya Tambarare akaulizwa Swali Moja na wakazi wa Tambarare kuwa umetufanyia nini kwa miaka kumi ya Ubunge? Swali lile hakuweza kulijibu na badala yake paliibuka vurugu kubwa hadi mkutano kuvurugika Kabisa.

Ni Mara Chache Sana kwa Mkoa wa Kilimanjaro Mbunge wa Jimbo kukaa kwa zaidi ya miaka kumi kwenye Jimbo Hilo hilo. Nilidhani Mbowe baada ya kukutana na Swali lile la umetufanyia nini angelichukua hatua mapema ya kutafuta mrithi wa Jimbo Hilo kupitia Chadema.

Kadri Muda unavyozidi kwenda asilimia za Mbowe kurudi Bungeni zinaendelea kupungua. Mfano Kura zingepigwa leo Mafue mgombea wa CCM anashinda kwa asilimia zaidi ya 60. Ukiachana na Siasa za kiitikadi watu wa Hai wana mahitaji yao ya msingi ambayo wanataka yatimizwe au yatatuliwe.

Kwenye Urais Hali ya Mambo imeshajionyesha kuwa mshindi ni JPM, Kama nilivyowaambia kuwa Kabila la wachaga ni Opportunist wanajua kabisa kuwa kumchagua Mbowe Ni kukaa nje ya Mfumo kwa miaka mingine mitano. Watakaa nje kwa miaka mitano kwa kuwa Rais Magufuli ameshatamka wazi wazi kuwa msimu huu Ni win win Situation "Nipe Nikupe".

Itakuwa Fedheha Sana Mbowe kustaafishwa Siasa kwa kushindwa kwenye box la Kura. Dalili zipo wazi kabisa hata Lissu alipokwenda Hai Mapokezi na mikutano yake haikuwa na watu wengi. Dalili nyingine ya kushindwa ni JPM kuungwa mkono na watu wenye Ushawishi Kama Askofu Shoo. Kibaya zaidi wafanyabiashara wa Hai mwaka huu wapo kimya na shughuli zao hivyo Mbowe kabakia Mwenyewe na team yake tu.

Uchagani huwa tunasema Mangi huwa hanuniwi. Mambo si marahisi Sana Hai kama ilivyozoeleka, ule upepo wa Kaka Mbowe Kama mwaka huu hauvumi. Ujio wa JPM mkoani Kilimanjaro umeibomoa kabisa Ngome ya Upinzani.

Tusubiri tuone!

Ole Mushi
0712792602
Hakuna huo ni upepo tu unapita.
 
Back
Top Bottom