MBOWE ANAWEZA KUPATA FEDHEHA UCHAGUZI HUU
Na Thadei Ole Mushi
Mwaka huu Mh Mbowe kabla hata ya Kampeni kuanza alifanya mkutano mmoja kwenye Jimbo lake la Hai maeneo ya Tambarare akaulizwa Swali Moja na wakazi wa Tambarare kuwa umetufanyia nini kwa miaka kumi ya Ubunge? Swali lile hakuweza kulijibu na badala yake paliibuka vurugu kubwa hadi mkutano kuvurugika Kabisa.
Ni Mara Chache Sana kwa Mkoa wa Kilimanjaro Mbunge wa Jimbo kukaa kwa zaidi ya miaka kumi kwenye Jimbo Hilo hilo. Nilidhani Mbowe baada ya kukutana na Swali lile la umetufanyia nini angelichukua hatua mapema ya kutafuta mrithi wa Jimbo Hilo kupitia Chadema.
Kadri Muda unavyozidi kwenda asilimia za Mbowe kurudi Bungeni zinaendelea kupungua. Mfano Kura zingepigwa leo Mafue mgombea wa CCM anashinda kwa asilimia zaidi ya 60. Ukiachana na Siasa za kiitikadi watu wa Hai wana mahitaji yao ya msingi ambayo wanataka yatimizwe au yatatuliwe.
Kwenye Urais Hali ya Mambo imeshajionyesha kuwa mshindi ni JPM, Kama nilivyowaambia kuwa Kabila la wachaga ni Opportunist wanajua kabisa kuwa kumchagua Mbowe Ni kukaa nje ya Mfumo kwa miaka mingine mitano. Watakaa nje kwa miaka mitano kwa kuwa Rais Magufuli ameshatamka wazi wazi kuwa msimu huu Ni win win Situation "Nipe Nikupe".
Itakuwa Fedheha Sana Mbowe kustaafishwa Siasa kwa kushindwa kwenye box la Kura. Dalili zipo wazi kabisa hata Lissu alipokwenda Hai Mapokezi na mikutano yake haikuwa na watu wengi. Dalili nyingine ya kushindwa ni JPM kuungwa mkono na watu wenye Ushawishi Kama Askofu Shoo. Kibaya zaidi wafanyabiashara wa Hai mwaka huu wapo kimya na shughuli zao hivyo Mbowe kabakia Mwenyewe na team yake tu.
Uchagani huwa tunasema Mangi huwa hanuniwi. Mambo si marahisi Sana Hai kama ilivyozoeleka, ule upepo wa Kaka Mbowe Kama mwaka huu hauvumi. Ujio wa JPM mkoani Kilimanjaro umeibomoa kabisa Ngome ya Upinzani.
Tusubiri tuone!
Ole Mushi
0712792602