Uchaguzi 2020 Mbowe ashindwa kutetea Ubunge wake katika Jimbo la Hai

Uchaguzi 2020 Mbowe ashindwa kutetea Ubunge wake katika Jimbo la Hai

HAMY-D

JF-Expert Member
Joined
Sep 18, 2011
Posts
7,149
Reaction score
3,825
WanaJF,

Katika hali ambayo ilikuwa inatarajiwa na wengi ni kwamba Mgombea Ubunge wa Jimbo la Hai kupitia tiketi ya CHADEMA ambae pia ni Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa amegaragazwa vibaya sana kwa kuambulia kura 27,000 tu wakati mshindani wake Mgombea wa jimbo hilo kwa tiketi ya CCM amefanikiwa kujizolea kura zaidi ya 80,000.

B0AC0CE1-374B-47C7-86CE-F79623D233BC.jpeg

148D330B-00E5-48B4-A2C3-F8397D9B0B36.jpeg

Mgombea Ubunge kupitia CCM Saashisha Mafuwe, ameibuka mshindi katika Jimbo la Hai kwa kupata kura 89,786 huku mpinzani wake Freeman Mbowe wa CHADEMA akipata kura 27,684.

Hivyo ametangazwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Hai.


Kitendo cha Mbowe kukataliwa vibaya na wanaHai kwenye uchaguzi huru na haki kunatoa somo kwa wana CHADEMA na Watanzania kwa ujumla kuwa picha halisi ni kwamba Mbowe amechokwa na ushindi wake ndani ya chaguzi mbalimbali ndani ya CHADEMA unawezekana kwa sababu ya magumashi tu na sio vinginevyo.

Maamuzi ya wanaHai yamefanya Watanzania tuelewe kiundani kuwa bwana Mbowe bila shaka yoyote amekuwa akilazimisha kuendelea kuongoza CHADEMA na usanii wake wa kujifanya anakubalika umekuwa EXPOSED!

Kwa heshima kubwa nitumie nafasi hii kuwapongeza wana Hai kwa maamuzi sahihi na pia kuwapongeza CCM kwa kuukata mkorosho jimboni hai kwa kutumia Topaz tu.

Pole sana Bwana Mbowe.
 
Ujinga mtupu, eti uchaguzi huru na haki!. umejaribu kutengeneza mazingira ili Mbowe aonekane hafai.

Kumbe mmeshinda kwa kujaza kura feki kila kona, Mbowe ni mwamba kawasumbua hamna hamu nae mpaka mmesaidiwa na tume.

Wametangaza matokeo haraka haraka usiku mnene kuogopa reaction ya wapiga kura, then asubuhi mapema defender zitaanza kuzunguka jimbo zima la Hai kuwatisha wapiga kura.

Ndio maana Ndugai alikuwa anachekelea bungeni wapinzani hawatarudi, kumbe huu mpango wa kujaza kura feki ndio ulikuwa kwenye vichwa vyao.

Mngeweza kumtoa hata roho, bora mmemuachia roho yake.
 
Back
Top Bottom