OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 53,868
- 121,001
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema miaka saba iliyopita ilikuwa ya bonde la maumivu makali kwa wananchi wote.
Alitaja maumivu hayo akihusisha wale waliofungwa magerezani na watumishi waliofukuzwa kwa kigezo cha vyeti feki.
Mbowe aliyasema hayo jana mkoani Njombe alipokuwa akiwahutubia wananchi mkoani humo, ikiwa ni mwendelezo wa mikutano ya hadhara baada ya kuruhusiwa hivi karibuni.
“Wako walionyang’anywa mali, Tanzania ikageuzwa kuwa Taifa la mateso, wananchi wakaishi kwenye hofu, lakini kwa wiki moja tuliyofanya mikutano ya hadhara, nikiliangalia Jeshi la Polisi silielewi mbona limekuwa na ubinadamu hivyo,”alisema Mbowe.
Alisema miaka saba iliyopita jeshi hilo halikuwa hivyo, lakini wanashukuru kwa sasa hali hiyo imebadilika na wanaamini kiongozi wa nchi anatengeneza vyombo vya dola kwa kuzingatia misingi ya kujali haki kwa wote.
“Tunachokiona leo ni Tanzania tunayoipenda Chadema tukizungumza, polisi wapo wanalinda amani na wanasikiliza sera.Tulifika hatua polisi wetu walionekana maadui kwa wananchi na raia, walikuwa wanawaombea mambo mabaya,”alisema.
My Take
Awamu ya Magufuli ni ya hovyo, ni kama awamu ya Nduli kule Uganda