Mbowe: CHADEMA haijawahi kuibiwa kura katika uchaguzi wowote ila hushindwa ka sababu ya msingi dhaifu

Mbowe: CHADEMA haijawahi kuibiwa kura katika uchaguzi wowote ila hushindwa ka sababu ya msingi dhaifu

comte

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2011
Posts
9,019
Reaction score
6,825
Mbowe alisema wazo la “Chadema Msingi” ambayo ilikuwa na lengo la kuwasajili wanachama wapya kuanzia ngazi ya chini, alilipata akiwa gereza la Segerea baada ya kusoma kitabu cha mwanazuoni kutoka taasisi ya NDI, Jean Sharp kinachoitwa “From dictatorship to democracy: How to fight dictatorship”.

Mbinu hiyo imekuwa ikiipatia CCM ushindi kwenye chaguzi mbalimbali kwa sababu chama hicho kimejijenga kuanzia ngazi ya chini ya Balozi wa Nyumba Kumi ambako ndiko kuna wapigakura wengi.

Kwa bahati mbaya, Chadema ilikuwa imejikita zaidi kwa wanachama wa ngazi za kati na juu, hasa waishio mijini na watu maarufu na kuwasahau maelfu ya wananchi ambao wanaishi vijijini bila kufikiwa na vyama vya upinzani.
===

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimekuwa kikiimarika kila kukicha tangu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1992 na tangu kishiriki kwa mara ya kwanza katika uchaguzi mkuu uliohusisha vyama vingi mwaka 1995.

Mkakati wa Chadema kujiimarisha kuanzia ngazi ya chini huenda ukatoa ushindani mkubwa kwa CCM katika chaguzi zijazo na kukiwezesha chama hicho kuvuna viongozi wengi wa serikali za mitaa, wabunge na madiwani.

Chama hicho kimeanza hamasa zake za kujijenga upya kwa wananchi kupitia kampeni maalumu ya “Tunasonga Kidijitali” yenye lengo la kuhamasisha wanachama wao kulipa ada ya uanachama kwa njia ya kielektroniki.

Chadema kidijital inatajwa mbinu ya kujibu na kubana CCM inayotumia mfumo wa balozi wa nyumba 10 ambao uongozi unaanzia ngazi za chini tofauti na ilivyokuwa chama hicho kikuu cha upinzani.

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na viongozi wengine wa chama wanazunguka katika kanda zote 10 kuelezea mpango wa chama hicho kujiendesha kwa michango ya wanachama wake, pia, kushinikiza kuundwa kwa Tume Huru ya Uchaguzi na Katiba mpya.

Miaka mitano ya Serikali ya awamu ya tano ilikuwa michungu kwa vyama vya upinzani nchini kutokana na mbinu mbalimbali zilizokuwa zikitumika kuvidhoofisha, hata hivyo, Chadema ilianzisha sera ya ‘Chadema msingi’ ili kuwafikia wananchi wengi.

Chama hicho kilizindua sera hiyo kama mbinu ya kuvuta wanachama kwa njia ya kidijitali baada ya Mbowe kutoka mahabusu Machi 2019 akiwa amekaa gerezani kwa siku 104 kuanzia Novemba 23, 2018 hadi Machi 7, 2019.

Mbowe alisema wazo la “Chadema Msingi” ambayo ilikuwa na lengo la kuwasajili wanachama wapya kuanzia ngazi ya chini, alilipata akiwa gereza la Segerea baada ya kusoma kitabu cha mwanazuoni kutoka taasisi ya NDI, Jean Sharp kinachoitwa “From dictatorship to democracy: How to fight dictatorship”.

Mbinu hiyo imekuwa ikiipatia CCM ushindi kwenye chaguzi mbalimbali kwa sababu chama hicho kimejijenga kuanzia ngazi ya chini ya Balozi wa Nyumba Kumi ambako ndiko kuna wapigakura wengi.

Kwa bahati mbaya, Chadema ilikuwa imejikita zaidi kwa wanachama wa ngazi za kati na juu, hasa waishio mijini na watu maarufu na kuwasahau maelfu ya wananchi ambao wanaishi vijijini bila kufikiwa na vyama vya upinzani.

Chadema sasa imerudi na sera mpya ya “Tunasonga Kidijitali” ambayo inafanana na ile ya “Chadema Msingi” kwa sababu lengo ni lilelile la kujenga chama kuanzia ngazi ya chini na wanachama kuchangia uendeshaji wa chama chao.

Juni 10 akiwa Morogoro, Mbowe alibainisha kwamba lengo la kuanzisha sera hiyo ni kuwatambua na kuwasajili wanachama wao nchi nzima kwa njia ya kidijitali ambayo pia itasaidia kukusanya kikamilifu mapato yanayotokana na michango ya kadi.

Alisema kuwa kupitia usajili wa kidijitali kutasaidia kuwa na idadi kamili ya wanachama wao nchi nzima.

“Ni bora kuwa na wanachama wachache waaminifu na waliokuwa tayari kukichangia chama kuliko kuwa na wanachama wengi ambao uanachama wao hautambuliki na hawalipii kadi zao na wengine hawana kabisa,” alisema Mbowe.

Kutokana na mazingira ya kisiasa yalipo sasa, chama hicho kitajiimarisha zaidi kuelekea uchaguzi mkuu ujao na pia kitapata fedha za kukiwezesha kuwafikia wananchi waliopo vijijini, hasa wakati huu ambao chama hicho hakipati ruzuku ya kutosha.

Mchambuzi wa siasa, Andrew Bomani anasema Chadema imefikia hatua nzuri ya kufikiria kujitegemea kimapato badala ya kutegemea ruzuku kuendesha chama, jambo ambalo anasema limevikwamisha vyama vingi.

Anasema wakijipanga vizuri watafanikiwa katika mpango huo kwa sababu chama kinaendeshwa na wanachama wenyewe na kwamba hatua hiyo ya kutafuta mapato itaongeza hamasa ya viongozi kutafuta wanachama wapya.

“Ni hatua nzuri, tena naona wamechelewa sana, ilitakiwa waanze siku nyingi huko nyuma. Sasa ni kama wanaanza upya, wana kazi kubwa ya kuhamasisha wanachama wao,” anasema Bomani ambaye aliwahi kuwa kiongozi wa UDP.

Bomani anasema wanachama wana nafasi kubwa katika uendeshaji wa chama, hivyo anaona Chadema watafanikiwa katika mpango huo wakiwa ni chama kikuu cha upinzani nchini ambacho kinashindana na CCM.

Kwa upande wake, mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk Faraja Kristomus anasema ana fikra chanya kuhusu uamuzi wa Chadema kwa sababu kitapata idadi kamili ya wanachama wake nchi nzima ambayo itakiwezesha kujitathmini.

Anasema wanachama wengi wa chama hicho wako maeneo ya mijini na wana kipato cha kati, hivyo kuanza kutumia mfumo wa kidijitali kutawasaidia kuwafikia wanachama wao wengi zaidi kwa wakati mmoja.

“Siku hizi siasa nyingi zinafanyika kidijitali, unaweza kuwafikia watu wengi zaidi kupitia mitandao, kwa hiyo nadhani ni jambo zuri,” anasema Dk Kristomus.

Hata hivyo, anasema wasiwasi wake ni namna Chadema watakavyoweka wazi taarifa zao za mapato yanayotokana na ada za uanachama. Anasema wakifanikiwa katika hilo, watawavutia wanachama wengi zaidi.

Kuhusu kupata wanachama wapya, Dk Kristomus anasema ana wasiwasi kama matumizi ya kidijitali yatawasaidia kwa sababu wananchi, hasa wa vijijini wanapenda kumwona mtu, wamsikilize na wamuulize maswali.

“Ni vigumu sana kupata wanachama wapya kupitia mfumo wa kidijitali, lazima wafike kwa wananchi, la sivyo, watapata wanachama ambao wanafuata mkumbo,” anasema mwanazuoni huyo.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT), Robert Katabi anasema hizi ni zama za kidijitali na vyama vya siasa ikiwemo CCM vinatakiwa kutumia mtaji wa wananchi wao kuendesha chama.

Anasema hawawezi kuendelea kutegemea ruzuku kutoka serikalini wakati kuna fursa kubwa kwenye ulimwengu wa teknolojia ikiwa ni pamoja na kueneza itikadi za chama na kupata fedha za kuendesha chama.

“Matokeo ya hiki wanachokifanya Chadema yataonekama muda siyo mrefu, ni jambo kubwa ambalo linafanyika nchi za wenzetu. Kinachotakiwa ni matumizi mazuri ya fedha zitakazokusanywa na siyo fedha hizo zisababishe mgogoro mwingine,” anasema.

Chanzo: Mwanachi
 
Watasema yote waliyomsingizia mwendazake. Nafsi zitawasuta mpaka kufa kwao.

Juzi tena alisema chadema ilishindwa kwa sababu ilisimamisha wagombea dhaifu kuanzia urais mpaka chini
Screenshot_2021-06-08-15-28-19-1.png

Hahahaha Mbowe kawanyoosha!! Inabidi muokoteze maneno ya kujitia moyo.
 
Kusonga Kidijitali ili kuwapata wananchama wa ngazi za chini (nadhani wengi hawa wapo vijijini) sasa hii kusonga kidijitali kutawafikia huko ?
 
Sasa zile kelele za kura feki??

Jamani jamani jamani...!,

R.I.P JPM
 
Chadema, ni chama cha kutetea maslahi ya watu wa kanda ya Kasikazini
 
Hakuna mahala kwenye hiyo article Mbowe kasema hicho kitu..... Mbona mnapenda kupotosha?
Mkuu sina namna yoyote ya kukusaidia zaidi ya kukwambia uwe na imani na Mbowe
 
Mtatengeneza Sana habari za kuwapa faraja enyi push gang. Hamna chenu awamu hii. Hampendwi na wenzenu wale wa ccm asilia na ccm mtandao.

So far, hili kundi la push gang watu wameanza kujichomoa taratibu. Si mnawasikia akina Gambo?..

Push gang kwishaaa! Sasa hivi hata covid-19 wanathaminiwa ndani ya ccm kuliko push gang. Ndiyo maana kule Mwanza Covid-19 Nusrat Hanje alipewa nafasi ya kuongea mbele ya mama.
 
Mimi sijui Mbowe kasemaje au ana mtazamo gani juu ya chaguzi, lakini ishu ya wizi wa kura siwezi kusubiri hadi Mbowe au mpinzani yeyote aseme.

Ukweli ni kwamba wizi wa kura upo kila uchaguzi, lakini 2020 ulipitiliza. Hata marehemu walipiga kura. Anayekataa akatae, lakini nilipata fursa ya kusimamia kakituo kamoja bush huku.

Aisee ule ulikuwa uchaFuzi mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Eti amesoma kitabu jinsi ya kupambana na udikteta. Hapo kwanza kashakosea kwa sababu anaanza kwa kupotoshwa na propaganda za magharibu kwa sababu ccm haiongozi nchi kidikteta. Pia ameaminishwa ccm haipendwi inaiba kura. Yote hayo sio sahihi.
 
Nafsi zinawasuta Sana ccm, sishangai mkiandika huu utumbo na kupotosha.
 
Nina akili huenda kuliko huyo aliyeandika hayo, sihitaji kuongozwa na mtazamo wake.
 
Back
Top Bottom