Mbowe: CHADEMA haikupokea mwaliko wa kwenda Ikulu kuzungumza na Rais Magufuli

Mbowe: CHADEMA haikupokea mwaliko wa kwenda Ikulu kuzungumza na Rais Magufuli

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,881
Reaction score
6,377
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, amezungumzia kuitwa Ikulu kwa baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa nchini na uamuzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kumfuta uanachama aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe.

Jumanne, Mshauri Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad, aliitwa Ikulu jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mazungumzo na Rais John Magufuli.

Mbali na Maalim Seif, viongozi wengine wa vyama vya upinzani waliokwenda Ikulu na kuteta na Rais siku hiyo ni Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahimu Lipumba, na Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia.

Baada ya viongozi hao kutoka Ikulu, kuliibuka mjadala kwenye mitandao ya kijamii kuhusu kutoonekana Ikulu siku hiyo kwa uongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini, Chadema.

Alipoulizwa kuhusu suala hilo jana, Mbowe alisema chama chake licha ya kubeba ajenda ya maridhiano ya kitaifa, hakikupata mwaliko wa Ikulu siku hiyo.

Mbowe pia alisema hafahamu ajenda walizoitiwa viongozi wengine wa vyama vya upinzani ambao siku hiyo walipata fursa ya kuteta na Rais Magufuli.

“Sisi (CHADEMA) hatujapokea mwaliko wowote wa simu au wa maandishi na hatujui wenzetu wamealikwa kwa utaratibu gani na ajenda ilikuwa ni ipi, labda wao ndiyo waeleze. Sisi tulishaongea hadharani na tulishaandika barua ya kutaka maridhiano ingawa mpaka sasa hatujajibiwa," alisema.

SAKATA LA MEMBE

Alipoulizwa kama chama chake kiko tayari kumpokea Membe baada ya kuvuliwa uanachama wa CCM, Mbowe alisema chama hicho sasa kina uzoefu wa kupata faida na hasara ya kuchukua wanachama kutoka chama tawala.

Alisema chama kimekuwa kikipokea makada hao wa CCM wasioijua na kuamini katika itikadi ya Chadema, bali kufuata maslahi binafsi, na sasa kimechukua tahadhari na hakina haraka ya kuwapokea.

“Chama chetu kimepata faida na hasara ya kuchukua wanachama kutoka Chama Cha Mapinduzi, 2015-2020 tumepata 'experience' (uzoefu) kubeba wanachama kutoka chama kingine ambao hawaijui itikadi yetu, lakini pengine wanaangalia maslahi ya muda mfupi," alifafanua.

Alisema Chadema sasa iko makini na haina haraka ya kupokea wanachama kutoka vyama vingine, lakini akasisitiza kuwa milango iko wazi na hakuna uadui wala urafiki wa kudumu katika siasa.

VURUGU JIMBONI
Vilevile, kiongozi huyo wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, alitoa ufafanuzi kuhusu vurugu zilizotokea wakati wa mkutano wake na wananchi Jimbo la Hai mkoani Kilimanjaro juzi.

Alisema vurugu hizo ni za kupangwa na kwamba anawafahamu wahusika wa vurugu hizo na nyendo zao.

Mbowe alisema watu hao walipelekwa eneo la mkutano kwa mabasi na walifika eneo dakika chache kabla ya kutimu saa 12 jioni, muda ambao alipaswa kuhitimisha mkutano wake.

Alisema vijana hao walifanya vurugu katika mkutano huo licha ya askari polisi kuwapo na waliwapa majina na namba za magari waliyotumia.

“Wale vijana walikuja mapema kwa kuletwa na mabasi maana ni vyema mkajua kwanza ‘back ground’ (historia). Hata namba za mabasi yaliyowaleta tunazo na tuliwakabidhi polisi.

“Katika muda wa saa 12 wakati wa harakati za kuaga na kufunga mkutano, wakaanza 'ku-shout' (kupiga kelele) na nakumbuka tuliwaambia polisi kuwa “kuna watu wameandaliwa na mnawajua, wanafanya vurugu na mmesimama nao katikati hapo,” alisema.

Mbowe aliongeza kuwa baada ya vurugu hizo, aliwaomba wanachama wake kutojibu mapigo ili kuepusha uvunjifu wa amani katika eneo hilo, badala yake kutoa vifaa vyao vilivyotumika katika mkutano huo na kuondoka kwa kuwa muda wa mkutano ulikuwa umekwisha.

Hata hivyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Salum Hamduni, alikaririwa na vyombo vya habari juzi, akisema hajapokea taarifa zozote za kutokea kwa vurugu katika mkutano wa Mbunge wa Hai.
 
1. Maendeleo huletwa na Mbunge au serikalini?

2. Serikali nimetoa asilimia ngapi ya budget kama ilivopangwa na kuamliwa na Bunge?
ndiyo anatakiwa awaambie wananchi wake kuwa nimefanya hiki na nmenymwa hiki na serikali
 
Kuna maswala muhimu sana ambayo Mbowe, amesahau kuyazungumzia, kwa maana kwamba ni wapi amefikia kuhusiasa na ahadi alizozitoa jimboni kwake, nini kimemkwamisha na ana mpango gani wa kuzitimiza au hatoweza kuzitimiza ahadi zake.
 
Anachotakiwa ajibu hoja za watu wa hai amewaletea maendeleo gani mpaka sasa?
Maendeleo aliyoyafanya Mbowe Hai hakuna mbunge wa ccm aliyefika hata robo yake , wewe watu wamekupuuza tu ndio maana haujibiwi , na bila shaka huijui Hai , Hai kuna magari ya kuzoa taka yanayotumika Ulaya , siyo matrekta kama ya DSM , Mbowe ndiye mtu pekee aliyekarabati hospitali kwa hela zake na kuweka vitanda na magodoro mapya hospitali nzima kwa hela zake mwenyewe

Hayo ni machache sana kati ya mengi mno ! usione tumenyamaza
 
We ungekuwa mbunge ungechukua mshahara wako kwenda kujenga barabara, hospitali, shule, kuchimba maji nk.

Kodi zinazolipwa kazi yake nini? Shule mwasoma kuingiza matope akilini au kuondoa ujinga?
Kwa maana nyingine wabunge huwa wanatudanganya kuhusu majukumu Yao ..KAZI Yao moja tuu..kutunga Sheria tuu.
 
Back
Top Bottom