Mbowe: CHADEMA haikupokea mwaliko wa kwenda Ikulu kuzungumza na Rais Magufuli

Hata hivyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Salum Hamduni, alikaririwa na vyombo vya habari juzi, akisema hajapokea taarifa zozote za kutokea kwa vurugu katika mkutano wa Mbunge wa Hai.

Kila siku wanazuia Mikutano kwa sababu ya intelligence inawaambia kuwa kutakuwa na machafuko/fujo .... sasa vitu ambavyo viko so obvious ambavyo hata bibi yangu kule kijijini anajua. Mkuu wa Police anadai hana habari .... This is Pathetic!!
 
Anachotakiwa ajibu hoja za watu wa hai amewaletea maendeleo gani mpaka sasa?
Maendeleo huletwa na serikali, mbunge hushiriki kupanga bajeti ya maendeleo na kuikabidhi serikali kwa utekelezaji, usijifanye haulijui hili.
 
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, amezungumzia kuitwa Ikulu kwa baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa nchini na uamuzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kumfuta uanachama aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe.

Jumanne, Mshauri Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad, aliitwa Ikulu jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mazungumzo na Rais John Magufuli.

Mbali na Maalim Seif, viongozi wengine wa vyama vya upinzani waliokwenda Ikulu na kuteta na Rais siku hiyo ni Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahimu Lipumba, na Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia.

Baada ya viongozi hao kutoka Ikulu, kuliibuka mjadala kwenye mitandao ya kijamii kuhusu kutoonekana Ikulu siku hiyo kwa uongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini, Chadema.

Alipoulizwa kuhusu suala hilo jana, Mbowe alisema chama chake licha ya kubeba ajenda ya maridhiano ya kitaifa, hakikupata mwaliko wa Ikulu siku hiyo.

Mbowe pia alisema hafahamu ajenda walizoitiwa viongozi wengine wa vyama vya upinzani ambao siku hiyo walipata fursa ya kuteta na Rais Magufuli.

“Sisi (CHADEMA) hatujapokea mwaliko wowote wa simu au wa maandishi na hatujui wenzetu wamealikwa kwa utaratibu gani na ajenda ilikuwa ni ipi, labda wao ndiyo waeleze. Sisi tulishaongea hadharani na tulishaandika barua ya kutaka maridhiano ingawa mpaka sasa hatujajibiwa," alisema.

SAKATA LA MEMBE

Alipoulizwa kama chama chake kiko tayari kumpokea Membe baada ya kuvuliwa uanachama wa CCM, Mbowe alisema chama hicho sasa kina uzoefu wa kupata faida na hasara ya kuchukua wanachama kutoka chama tawala.

Alisema chama kimekuwa kikipokea makada hao wa CCM wasioijua na kuamini katika itikadi ya Chadema, bali kufuata maslahi binafsi, na sasa kimechukua tahadhari na hakina haraka ya kuwapokea.

“Chama chetu kimepata faida na hasara ya kuchukua wanachama kutoka Chama Cha Mapinduzi, 2015-2020 tumepata 'experience' (uzoefu) kubeba wanachama kutoka chama kingine ambao hawaijui itikadi yetu, lakini pengine wanaangalia maslahi ya muda mfupi," alifafanua.

Alisema Chadema sasa iko makini na haina haraka ya kupokea wanachama kutoka vyama vingine, lakini akasisitiza kuwa milango iko wazi na hakuna uadui wala urafiki wa kudumu katika siasa.

VURUGU JIMBONI
Vilevile, kiongozi huyo wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, alitoa ufafanuzi kuhusu vurugu zilizotokea wakati wa mkutano wake na wananchi Jimbo la Hai mkoani Kilimanjaro juzi.

Alisema vurugu hizo ni za kupangwa na kwamba anawafahamu wahusika wa vurugu hizo na nyendo zao.

Mbowe alisema watu hao walipelekwa eneo la mkutano kwa mabasi na walifika eneo dakika chache kabla ya kutimu saa 12 jioni, muda ambao alipaswa kuhitimisha mkutano wake.

Alisema vijana hao walifanya vurugu katika mkutano huo licha ya askari polisi kuwapo na waliwapa majina na namba za magari waliyotumia.

“Wale vijana walikuja mapema kwa kuletwa na mabasi maana ni vyema mkajua kwanza ‘back ground’ (historia). Hata namba za mabasi yaliyowaleta tunazo na tuliwakabidhi polisi.

“Katika muda wa saa 12 wakati wa harakati za kuaga na kufunga mkutano, wakaanza 'ku-shout' (kupiga kelele) na nakumbuka tuliwaambia polisi kuwa “kuna watu wameandaliwa na mnawajua, wanafanya vurugu na mmesimama nao katikati hapo,” alisema.

Mbowe aliongeza kuwa baada ya vurugu hizo, aliwaomba wanachama wake kutojibu mapigo ili kuepusha uvunjifu wa amani katika eneo hilo, badala yake kutoa vifaa vyao vilivyotumika katika mkutano huo na kuondoka kwa kuwa muda wa mkutano ulikuwa umekwisha.

Hata hivyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Salum Hamduni, alikaririwa na vyombo vya habari juzi, akisema hajapokea taarifa zozote za kutokea kwa vurugu katika mkutano wa Mbunge wa Hai.
Inawezekana majibu ya kesi yao yanajulikana hivyo hawatakuwa uraiani, hawahitajiki.
 
Mbowe ni kiongozi wa chama cha upinzani wa kweli, utamlinganishaje na hao wachumia tumbo?

In God we Trust
 
Ubarikiwe sana mkuu
1. Maendeleo huletwa na Mbunge au serikalini?

2. Serikali nimetoa asilimia ngapi ya budget kama ilivopangwa na kuamliwa na Bunge?

In God we Trust
 
ndiyo anatakiwa awaambie wananchi wake kuwa nimefanya hiki na nmenymwa hiki na serikali
Naona tayari laana ya mlio watesa na kuwajeruhi imeanza na kupukutisha ubongo wako

In God we Trust
 
Anachotakiwa ajibu hoja za watu wa hai amewaletea maendeleo gani mpaka sasa?
Pesa za maendeleo zipo halimashauri ya wilaya acheni kupeleka wavuta Bangi kuwasumbua wapinzani
 
Mbowe should grow up! Rais sio sawa na wabunge wake wakina Sugu!

Mbowe anatakiwa kumuandikia Rais barua ya kuomba kuonana nae.... tena kwa adabu!

Mbowe aache tabia za kina Lema za kuongea na Rais kupitia mitandao!
 
Mtu yoyote akikosoa chadema amenunuliwa?

Dk Slaa aliwakosoa chadema akawahoji hao mnaopokea ni asset au liability? Akaambiwa ni Dk mihogo amenunuliwa na ccm lakini leo Mbowe na wazee wa chadema wanajuta hadharani kupokea pokea wanachama hovyo.
Chadema badala ya kujibu hoja za Mbatia wanajificha kwenye kichaka cha amenunuliwa na ccm!!!!

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
"Hakuna uadui wala urafiki wa kudumu katika siasa" Hivyo milango ipo wazi kwa Membe kuhamia Chadema hawana tena uadui nae,ndiyo maana wengine wametoka chadema na kuhamia Ccm hawana uadui tena na chama tawala.
 
Back
Top Bottom