Mbowe: CHADEMA haikupokea mwaliko wa kwenda Ikulu kuzungumza na Rais Magufuli


Kwa hiyo anakiri Dr Slaa alikuwa na UZOEFU kuliko yeye na Tundu Lisu wake?
Maana aliwauliza Lowasa ni Asset au Liability?
Pengine Mbowe hakuelewa swali lilimaanisha nini, lakini hata Lisu naye hakuelewa?
 
Mtu yoyote akikosoa chadema amenunuliwa?

Dk Slaa aliwakosoa chadema akawahoji hao mnaopokea ni asset au liability? Akaambiwa ni Dk mihogo amenunuliwa na ccm lakini leo Mbowe na wazee wa chadema wanajuta hadharani kupokea pokea wanachama hovyo.
Chadema badala ya kujibu hoja za Mbatia wanajificha kwenye kichaka cha amenunuliwa na ccm!!!!

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Anachotakiwa ajibu hoja za watu wa hai amewaletea maendeleo gani mpaka sasa?
Haya ni mambo ambayo ameyafanya Mbowe Hai kwa uchache.
1. kukarabati wodi namba moja machame hospital na kutoa vitanda vya kisasa.
2.kukarabati masama dispensary kubadilisha magodoro na kujenga tanuru la kuchomea taka.
3.kuotesha miti barabara kuu za Hai ipo na inaonekana.
4.alitoa magari mawili ya kubebea wagonjwa kwa hospital ya Hai.
5.alitoa gari la kisasa la kubebea takataka pamoja greda iliyozinduliwa na jpm akiwa waziri wa ujenzi.
6.kipande Cha lami kutoka Bwani to machame km kama 3 ni Mbowe aliomba kwa mhe kikwete
7.mbowe alitoa computers shule zote za sekondari Hai
8.mbowe aliwalipia pre form Jimbo zima mwaka 2000s
9.mbowe alikarabati soko la Mula na kuweka moramu barabara ya km 2 2016.
10.mbowe ametoa michango binafsi kwa taasisi mbali mbali Hai
 
Yeye awajibu watu wa Hai, nini amefanya Hai kwa miaka 5.
 
Wenzie wao ndio waliomba kuonana na Rais tena kwa barua kadhaa wa kadhaa

Seif Sharif anasema aliandika barua tatu ndio akakubaliwa, the same to Mbatia na Lipumba

Mbowe aandike barua kwa adabu sio utoto wa kuandika barua kwa Rais huku unaitupia mtandaoni hata kabla haijafika kwa Afande Amirijeshi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kumbe angeitwa angeenda... sasa kwanini walioitwa wakaenda waitwe wasaliti?
 
Watia huruma kwa kukaukiwa hoja.
 

Tukio hilililipangwa na mjinga. Alipanga lifanyike na akawapa hoja za kuongea ndio maana wanarudia maneno yale yale wakati tukio halikwenda walivyopanga au kutarajia.Sasa kwa sababu wamekaririshwa wanashindwa ku twist iliku reflect haliilivyooenda mpaka warudikwa programmer awape software nyingine. Kazi kweli kweli.
 
Kuna upande wa pili wa kwa nini Mbowe hajaitwa Ikulu. Ni wazi kuwa Raisi Magufuli anamjua Mbowe, kwamba sio mtu wa kuyumbishwa na kutishwa kirahisi na hamwogopi Magufuli kama viongozi wengine wa kisiasa ambao wakiitwa tu na Raisi wanaenda wanatetemeka na kusema ndio Mheshimiwa Raisi kwa kila kitu wanachoambiwa.

Raisi Magufuli anajua wazi akimwita Mbowe Ikulu inatakiwa iwe kujadili hoja za msingi sio kumpa maagizo au kumtisha au hata kutaka kumnunua. Akaona ni bora tu amwache, labda kwa sasa, hadi atakapofikiria namna nzuri ya kuongea na Mbowe kistaarabu. Magufuli anajua wazi inabidi ajipange vema ili kuongea na Mbowe.

Katika utawala wa awamu ya tano, viongozi wengi wa upinzani wamekuwa wanasiasa jina tu, wanatishwa au kununulika kirahisi sana. Wapo wachache ambao bado wana msimamo kama kina Mbowe, Mdee, Tundu Lisu nk. Hawa sio aina ya "malaya malaya" kama alivyosema Nyerere huko nyuma, na hilo liko wazi sana kwa Magufuli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…