LGE2024 Mbowe: CHADEMA haitajitoa katika uchaguzi Serikali za Mitaa. Wagombea wetu walioenguliwa kihuni warejeshwe

LGE2024 Mbowe: CHADEMA haitajitoa katika uchaguzi Serikali za Mitaa. Wagombea wetu walioenguliwa kihuni warejeshwe

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Wakuu,

Saa 5 asubuhi hii Mbowe kutema cheche Makao Makuu ya CHADEMA, Mikocheni, nini kitaendelea? Vuta sofa kwa updates.


===

Kwahiyo CHADEMA hapa ndio anaenda kuongea Mwenyekiti wa Chama? :BearLaugh: :BearLaugh: :KEKWlaugh: Suala la naksi nakshi na udambwi udambwi ndio kitu kiliwashinda kabisaa... mwendo wa ki-Hip Hop, utafikiri mnaongea na watu wa Chuga na Mbeya peke yako (No shade kwa watu wa mikoa hiyo🥲), hata kama ndio wagumu ndio hivi jamani?

chad.jpg
===

Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika, amesema;

"Kauli ya Waziri wa TAMISEMI, Mchengerwa, kuhusu uchaguzi huu wa Serikali za Mitaa, vijiji na vitongoji, taratibu ambazo zinazoendesha uchaguzi huu, na utaratibu unaondelea katika uchaguzi huu, kwamba vyama vyote vya siasa 19 zilishirikishwa na kukubaliana katika hatua mbalimbali kuhusiana na yanayoendelea, niseme tu katika hatua hii ya awali kauli hiyo ya Waziri Mchengerwa ni kauli ya uongo, ni kauli ya upotoshaji ya kukiingiza chama cha CHADEMA kuwa kilikubaliana kikanuni, kiutaratibu, kikatiba na ufharimu, uovu, wizi na ukiukaji wa haki unaoendelea kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa."

"CHADEMA tulipinga hila hizo kwa kuchukua hatua kuhakikisha uchaguzi huu ni huru na wa haki. Tangu mwaka 2021, tumekuwa tukidai Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi. Baadaye, tukaingia kwenye mazungumzo ya maridhiano kwa mwaka mzima, sambamba na maandamano, tukisisitiza kwamba kabla ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa kufanyika, marekebisho ya Kikatiba na ya Sheria yahakikishe uchaguzi wa haki."

"Hoja mahsusi ni kwamba uchaguzi wa Serikali za Mitaa usisimamiwe tena na TAMISEMI, bali na Tume Huru ya Uchaguzi, na usitumie kanuni mbovu za uchaguzi, bali utengenezewe mifumo huru na ya haki."

"Katika mazungumzo ya maridhiano ajenda yetu kubwa ilikuwa ni kutaka kupatikana kwa Katiba Mpya, Tume Huru ya Uchaguzi na marekebisho ya kutaka uchaguzi uwe huru na wa haki nchini, pamoja na viambatanisho vingine vya kukwamua mchakato wa Katiba tuliwasilisha (kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa) mapendekezo mahsusi ya marekebisho ya Katiba na sheria ili kuhakikisha uchaguzi wa serikali za mitaa unakuwa huru na haki, mapendekezo haya hayakufanyiwa kazi na serikali kabisa pamoja na kukumbusha kwa nja mbalimbali"

"Serikali ikapeleka bungeni miswada mitatu ya Sheria: (i) Mswada wa Tume Huru ya Uchaguzi, (ii) Mswada wa Sheria ya Uchaguzi wa Udiwani, Ubunge na Urais, na (iii) Mswada wa Marekebisho ya Sheria ya Vyama vya Siasa. Tukaipinga miswada hii, tukaenda bungeni na kutoa maoni, lakini maoni yetu yakapuuzwa. Sheria mbovu zikapitishwa na Rais akasaini, na tulipinga, lakini walizidi kuendelea nazo."

"Uchaguzi huu unaosimamiwa na TAMISEMI, ukiondoa Waziri Mchengerwa ambaye ndiye msimamizi mkuu, unahusisha timu ya usimamizi inayojumuisha maafisa wa TAMISEMI, maofisa wa ofisi ya msajili mkuu wa vyama vya siasa, maofisa wa ofisi ya Waziri Mkuu, na watumishi wa idara ya usalama wa taifa."

"Sisi CHADEMA hatujakubaliana na TAMISEMI kuhusu hatua yoyote inayohusiana na utaratibu huu mbovu wa usimamizi wa uchaguzi. Kwanza, uchaguzi unasimamiwa na Waziri wa TAMISEMI, pili, kanuni ni mbovu na zenye mapungufu, ratiba ya uchaguzi imetolewa vibaya, na usimamizi wa uchaguzi unafanywa na watu wasiokuwa huru, ambao wamehusika na engua engua za wagombea katika maeneo mbalimbali na ubovu mkubwa katika uandikishaji wa wapiga kura."

Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe, amesema;

"Waangalie viongozi wetu nchi nzima, wanachama na wananchi maelfu kwa maelfu wanaamini kwenye chama hiki, Rahi zao wanasema ninyi viongozi tokeni semeni (kuhusu mwenendo wa uchaguzi wa serikali za mitaa 2024) tunajiuliza viongozi tuseme nini, ujenzi wa demokrasia sio jambo jepesei kama wengi wanavyofikiria kuiona CHADEMA imefika hapa ilipofika imepitia mengi mazito, maumivu, jasho, damu, vifo, vifungo nk"

"Hii kazi hatuifanyi kama furahaa, hii kazi tunaifanya kama adhabu, wote wanalipigania Taifa lao ili Watanzania wote tuwe na nchi salama ya kuishi, hiki chama kimejengwa kwa maumivu mazito sana hadi kimefika kuweza kujiita au nyie mkakiita chama kikuu cha upinzani kina mchanganyiko wa jasho jingi, watu wengi wamevuja jasho lao"

"Kama chama hiki (Chama cha Demokrasia na Maendeleo -CHADEMA) tulifika kilele chetu kwenye uchaguzi wa mwaka 2015, itakumbukwa kuwa wakati huo chama hiki kilishafika hatua ya kuwa na Wabunge 72 kwenye Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hakuna chamam chochote nchi hii kilishafikisha idadi hiyo ya Wabunge, kwa sababu ya jasho na damu na maumivu ambayo tumeyapitia wote huku kila mmoja akiwa na mchango wake"

"Chama kilifikisha Madiwani 1104 yani wakati Magufuli (Hayati Dkt. John Magufuli, aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya tano) anatoa katazo la kufanya kazi za siasa tayari CHADEMA ilikuwa na Madiwani 1104"

"Inawezekanaje viongozi wa chama kimoja (Chama cha Mapinduzi -CCM) na serikali yake unakuta wako kwenye vitongoji vyote, vijiji vyote na mitaa yote, halafu anasikika au anatokea kiongozi mmoja wa CCM anajisifu anasema eti sisi wapinzani (CHADEMA na wengineo) hawakua na wagombea, sisi (CHADEMA) tulikuwa na wagombea nchi nzima, wewe na serikali yote uliyonayo lakini licha ya kuwa umejibebesha Wabunge wote, Madiwani wote, Halmashauri zote, una vijiji vyote, una Polisi wote na mashirika ya ummma yote, unakuja kumfunga mwenzio kamba asiweze kipigana, wewe una unfair advantage halafu unajigamba badala ya kuona aibu"

"Yaani Chama cha Mapinduzi (CCM) hawaoni aibu kupambana na vyama vya upinzani ambavyo havina fedha, havina vitendea kazi, havina magari, watu wanajitolea lakini wao wanalipwa kwa kodi zetu bado wanaweza kuasimama eti wanajiweza wakajigamba eti wamepita kwa asilimia miabmoja wakati Dunia nzima inaona wakiengua watu wetu, haya mambo yanaaudhi wanaolia ni wengi, na wengi wanalia wanasema Mwenyekiti (Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa) tujitoe kwenye uchaguzi (wa serikali za mitaa 2024), wengine wanalia wanasema tutapambana mpaka hatua ya mwishio, sisi (CHADEMA) Kamati Kuu yetu tulikaa kikao cha Kamati Kuu Mtwara tarehe 06/03/2024 na likatoka azimio la Kamati Kuu ambalo tulilitoa kwamba tushiriki uchaguzi huu"

"Amesema watu wana mawenge, kuna mnyukano mfano wa Lema (Godbless Lema, Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Kaskazini) na Mheshuimiwa Benson Kigaila ambaye ni Naibu Katibu Mkuu CHADEMA Tanzania Bara (akacheka), ukishakuwa na chama cha siasa kisichokua na minyukano hicho chama ni mfu, kuna wakati viongozi wanapotea wanakwenda kidogo mbali lakini siasa ndiyo ilivyo kwani mkiwa kwenye siasa mkawa mnakubaliana asilimia mia moja siku zote hiyo safari hamtoboi"

"Kuna wakati tunateleza, Mbowe anaweza akateleza, Makamu anaweza akateleza kauli, Katibu Mkuu anaweza akateleza kauli lakini kwamba tuna mnyukano?, tumejenga hiki chama (CHADEMA) kwa maumivu makubwa, na sisi wote tumeshaapa tutakilinda chama hiki kwa gharama yoyote ile kwa hiyo kama kuna mtu anafikiria eti kuna mgogoro CHADEMA ambao utakigawa chama, tuko wamoja watu watanyukana tu"
 
Bila shaka makamanda wataisubiria kwa hamu kubwa sana hiyo hotuba yake. Maana huwaambii kitu kwa huyo Kamanda wao Mkuu wa chama.
 
Wakuu,

Saa 5 asubuhi hii Mbowe kutema cheche Makao Makuu ya CHADEMA, Mikocheni, nini kitaendelea? Vuta sofa kwa updates.


===

Kwahiyo CHADEMA hapa ndio anaenda kuongea Mwenyekiti wa Chama? :BearLaugh: :BearLaugh: :KEKWlaugh: Suala la naksi nakshi na udambwi udambwi ndio kitu kiliwashinda kabisaa... mwendo wa ki-Hip Hop, utafikiri mnaongea na watu wa Chuga na Mbeya peke yako (No shade kwa watu wa mikoa hiyo🥲), hata kama ndio wagumu ndio hivi jamani?


Wewe ni mchawi!
 
Utadhani mnamsubiri Diva fulani kama Maria Carey, kumbe mwenyekiti wa chama cha siasa.

Mkutano umetangazwa saa tano sasa hivi inaelekea saa sita, hovyo kweli.
 
Nachotaka kusikia ni kujitoa kwenye uchaguzi huu wa kipumbavu.
 
Kama ni kweli:

CHADEMA chini ya mwenyekiti mwingine, CCM watamkumbuka Mbowe.

Lissu ndio anafaa kumrithi Mbowe, ila wasipkuwa makini, uchaguzi wa Mwenyekiti unaweza kukivuruga chama. na ukawa mwanzo wa makundi ndani ya chama.

Ataechaguliwa wakati ukifika, ashinde kwa haki vinginevyo watavurugana.

Pia, CHADEMA wawe makini na mapandikizi kutoka CCM na hela za Mama Abdul kuanzia sasa mpaka siku ya uchaguzi.
 
Wakuu,

Saa 5 asubuhi hii Mbowe kutema cheche Makao Makuu ya CHADEMA, Mikocheni, nini kitaendelea? Vuta sofa kwa updates.


===

Kwahiyo CHADEMA hapa ndio anaenda kuongea Mwenyekiti wa Chama? :BearLaugh: :BearLaugh: :KEKWlaugh: Suala la naksi nakshi na udambwi udambwi ndio kitu kiliwashinda kabisaa... mwendo wa ki-Hip Hop, utafikiri mnaongea na watu wa Chuga na Mbeya peke yako (No shade kwa watu wa mikoa hiyo🥲), hata kama ndio wagumu ndio hivi jamani?


Na iwe hivyo.

Kuna Ukweli usiopingika kwamba Freeman Mbowe amekuwa kikwazo cha ustawi na maendeleo ya Chama chao hicho cha Chadema kwa miaka ya hivi karibuni. Mimi binafsi sipo huko Chadema na wala sipo CCM, isipokuwa ni Muumini mkubwa sana wa masuala ya HAKI, MAENDELEO na DEMOKRASIA.
Mimi ni mtu mwenye fikra huru na mitazamo huru kabisa, lakini dosari hii nimeiona ipo kwa upande wa chama hicho cha Chadema.

Aidha, Inavyoonekana ni kweli kabisa kwamba Kuna mvurugano ndani ya Chadema. Kiini cha kuwepo kwa mvurugano huu huko Chadema kwa maoni yangu ni kutokana na namna Mwenyekiti wa Chama chao hicho Freeman Mbowe kukosa misimamo inayoeleweka kuhusiana na Siasa za nchi hii kwa sasa. Siyo siri hata kidogo, Mbowe akiwa Kama Kiongozi wa Chama Chao hicho, amekuwa ni mtu ambaye Hana msimamo unaoeleweka hali hii imesababisha mkwamo na kuyumba kwa Wanachama wa chama hicho.

Mbowe amekuwa ni mtu asiyeaminika tena kwa sasa ndani ya Chama Chao hicho, watu wengi kwanza wanamchukulia kama ni Mamluki wa Chama tawala ambaye amejipachika kwenye Vyama vya upinzani kwa 'kazi maalumu ya kuvuruga vyama vya upinzani' ili kukinufaisha chama tawala.

'Engine' ya treni ikiharibika mabehewa yote kabisa ya treni nayo huyumba na kusimama.'
 
Hate ..
Kwamba Mwenyekiti wa Chama cha siasa sio mtu muhim?

Your thinking process, duh
Nimesema sio mtu muhimu au analeta mambo ya diva.

Tangazo la mkutano wao ilikuwa saa tano, umeanza saa sita. Sasa ili uone kero kama ulikuwa unafuatilia you tube toka saa tano.

Anyway ngoja niwasikilize washaanza kulałama kama unafuatilia.
 
Wakuu,

Saa 5 asubuhi hii Mbowe kutema cheche Makao Makuu ya CHADEMA, Mikocheni, nini kitaendelea? Vuta sofa kwa updates.


===

Kwahiyo CHADEMA hapa ndio anaenda kuongea Mwenyekiti wa Chama? :BearLaugh: :BearLaugh: :KEKWlaugh: Suala la naksi nakshi na udambwi udambwi ndio kitu kiliwashinda kabisaa... mwendo wa ki-Hip Hop, utafikiri mnaongea na watu wa Chuga na Mbeya peke yako (No shade kwa watu wa mikoa hiyo🥲), hata kama ndio wagumu ndio hivi jamani?

===

Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika, amesema kauli ya Waziri wa TAMISEMI, Mchengerwa, kuhusu uchaguzi huu wa Serikali za Mitaa, vijiji na vitongoji, taratibu ambazo zinazoendesha uchaguzi huu, na utaratibu unaondelea katika uchaguzi huu, kwamba vyama vyote vya siasa 19 zilishirikishwa na kukubaliana katika hatua mbalimbali kuhusiana na yanayoendelea, niseme tu katika hatua hii ya awali kauli hiyo ya Waziri Mchengerwa ni kauli ya uongo, ni kauli ya upotoshaji ya kukiingiza chama cha CHADEMA kuwa kilikubaliana kikanuni, kiutaratibu, kikatiba na ufharimu, uovu, wizi na ukiukaji wa haki unaoendelea kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

CHADEMA tulipinga hila hizo kwa kuchukua hatua kuhakikisha uchaguzi huu ni huru na wa haki. Tangu mwaka 2021, tumekuwa tukidai Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi. Baadaye, tukaingia kwenye mazungumzo ya maridhiano kwa mwaka mzima, sambamba na maandamano, tukisisitiza kwamba kabla ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa kufanyika, marekebisho ya Kikatiba na ya Sheria yahakikishe uchaguzi wa haki.

Hoja mahsusi ni kwamba uchaguzi wa Serikali za Mitaa usisimamiwe tena na TAMISEMI, bali na Tume Huru ya Uchaguzi, na usitumie kanuni mbovu za uchaguzi, bali utengenezewe mifumo huru na ya haki.


CHADEMA Kushiriki kwenye Uchaguzi siyo njia sahihi kwao, lakini pia hata kususia uchaguzi siyo njia sahihi kwao ya kufanya Siasa sahihi kwa hapa Tanzania hivi sasa.

THE WAY FORWARD:
Njia iliyo sahihi zaidi ya kufanya Siasa sahihi kwa hapa Tanzania kwa Sasa ni Moja tu: nayo ni KUDAI NA KUPIGANIA UPATIKANAJI WA KATIBA MPYA ILIYO NZURI.
Kupatikana kwa Katiba Mpya iliyo nzuri ndio itajenga Msingi Bora na ulio imara kabisa wa kufanikisha Mambo mengine yote kabisa yaliyo mazuri ikiwemo na hilo suala la Chaguzi za Siasa ambalo hao Chadema na Wapinzani wengine wamekuwa wakililalamikia miaka yote tangu Tanzania ipate Uhuru.

NB: Hakuna Jambo lolote lile lililo zuri ambalo linaweza kufanikiwa kwa Sasa hapa Tanzania bila ya kupatikana kwa Katiba mpya iliyo nzuri kwanza, never!
 
Hoja mahsusi ni kwamba uchaguzi wa Serikali za Mitaa usisimamiwe tena na TAMISEMI, bali na Tume Huru ya Uchaguzi, na usitumie kanuni mbovu za uchaguzi, bali utengenezewe mifumo huru na ya haki.

Serikali ikapeleka bungeni miswada mitatu ya Sheria: (i) Mswada wa Tume Huru ya Uchaguzi, (ii) Mswada wa Sheria ya Uchaguzi wa Udiwani, Ubunge na Urais, na (iii) Mswada wa Marekebisho ya Sheria ya Vyama vya Siasa. Tukaipinga miswada hii, tukaenda bungeni na kutoa maoni, lakini maoni yetu yakapuuzwa. Sheria mbovu zikapitishwa na Rais akasaini, na tulipinga, lakini walizidi kuendelea nazo.

"The right cannot be given as a gift by the oppressor, it must be demanded by the oppressed."

Dr. Martin Luther King Jr.


Aidha, CCM Kamwe haitaweza kuleta Katiba Mpya nchini Tanzania na wala haiitaji kuwe na Katiba Mpya hapa nchini kwa sababu hii Katiba iliyopo hivi Sasa ni yao na wameitunga wao wenyewe, isipokuwa Wananchi wengine wa Tanzania walio wengi zaidi ndio wanahitaji kuwa na Katiba yao mpya kwa sababu tangu nchi hii ipate Uhuru wake kutoka kwa Wakoloni kamwe Wananchi hao hawajawahi kuwa na Katiba yao bali muda wote na miaka yote hiyo wamekuwa wakitumia Katiba ya Watu wa CCM.
 
Back
Top Bottom