Mbowe: CHADEMA tunaamini kwamba umaskini ni laana na kila mwanachadema ni tajiri rohoni mwake

Mbowe: CHADEMA tunaamini kwamba umaskini ni laana na kila mwanachadema ni tajiri rohoni mwake

Duniani Kote umasikini ni laana, Eti Magufuli anajiita Rais wa wanyonge wakati anaiba pesa za walipa kodi"

Unyonge pia ni laana jamii zingine ukizaliwa zeluzelu au kilema wanakuua.

Izo ni dalili kuwa mnyonge ni laana kubwa sana.
 
Lkn sidhani kama alilisha kwa kununua chakula nafikiri alifanya miujiza kama wavuvi kupata samaki wengi n.k. Isitoshe kama Yesu alizaliwa kwenye Utajiri, huo utajiri ukitokea wapi kwani Baba yake Josefu alikuwa ni Seremala na siyo Mfalme, sasa huo Utajiri ulitokea wapi?
Kimiujiza akitaka pesa anaenda kwa samaki kuchukua .Maseremala aliyekuambia ni maskini nani? Nenda keko uone Wana Hadi maprado.Yusuf alikuwa na pesa ndio maana herode alipotaka kuua Yesu alitimka yeye na familia kwenda kuishi Misri miaka.
 
Kimiujiza akitaka pesa anaenda kwa samaki kuchukua .Maseremala aliyekuambia ni maskini nani? Nenda keko uone Wana Hadi maprado


Dunia hiyo aliyozaliwa Yesu Useremala haukuwa kazi ya kukupa Utajiri, Matajiri walikuwa ni Wafalme waliomiliki ardhi kubwa na Mahekalu, Josefu hakuwa tajiri!
 
Mimi nashangaa mtu anapojivunia umaskini. Utajiri ni baraka ndiyo maana watu ambao walimpendeza Mungu, aliwapa utajiri kwa sababu utajiri ni baraka na neema.

Mtazame Ibrahim alifanywa kuwa tajiri na Yahwe.

Mtazame Ayoub alivyotajirishwa na Mungu baada ya kumshinda shetani.

Mtazame Suleman alivyotajirishwa na Mungu baada ya kuomba hekima ya kuwahukumu watu kwa haki.

Ni aibu kwa kiongozi kujitangaza kuwa ni kiongozi wa watu maskini. Kazi ya kiongozi ni kujenga kundi la kumuunga mkono. Kiongozi anayetaka kuungwa mkono na maskini atakazana kutengeneza maskini wengi ili awe na wengi wa kumwunga mkono.

Kiongozi anayefurahia kuwaongoza watu matajiri atajitahidi kupunguza kundi la watu maskini ili awe na watu wengi matajiri ambao watafurahi naye katika utajiri wao.

Utajiri mbaya ni ule utokao kwa shetani lakini utajiri wa haki ni tunda la upendo wa Mungu.
 
Mbona makatibu wa wilaya na mikoa mnawafanyisha kazi bila malipo yaani mnawatia umasikini!!
Kifupi ni kwamba hamna mipango wala vipaumbele.. kama mngekuwa mnawalipa watumishi wenu na kwa wakati ningewaelewa.

Lakini wengi hawalipi na wanaolipwa wanakaa mamiezi bila malipo halafu mkipata mnaenda kutanua mimi siwaelewi.
Hamna tofauti na yule jamaa anaenunua ndege wakati wanafunzi hawajalipwa fedha za kujikimu wamegeuka makahaba na vibenten kama watumishi wenu
It is shame

Anayoyafanya Mbowe yatatunyima uhalali wa kuikosoa serikali bila kunyooshewa kidole
Opposition was meant to be the best option.. a model.. yaani kioo cha kukitazama serikali na chama tawala.
 
Dunia hiyo aliyozaliwa Yesu Useremala haukuwa kazi ya kukupa Utajiri, Matajiri walikuwa ni Wafalme waliomiliki ardhi kubwa na Mahekalu, Josefu hakuwa tajiri!
Uongo Yusuf alikuwa na passport alikuwa Mtu international herode alipotaka kuua mtoto Yusuf selemala tajiri aliondoka na familia kuishi nje ya nchi misri akakaa miaka .Angekuwa lofa asingekuwa na Hui uwezo
 
Dunia hiyo aliyozaliwa Yesu Useremala haukuwa kazi ya kukupa Utajiri, Matajiri walikuwa ni Wafalme waliomiliki ardhi kubwa na Mahekalu, Josefu hakuwa tajiri!
Yesu hakuwa maskini. Alikuwa tajiri moyoni mwake ndiyo maana alimdharau hata shetani aliyetaka ampe utajiri alimradi tu amsujudie. Kwa nini alikataa? Kwa sababu kile ambacho shetani alitaka kumpa kilikuwa ni kidogo sana ukilinganisha na utajiri aliokuwa nao.

Kuna maskini anaweza kuwalisha wanaume zaidi ya 5,000; wakala na kushiba? Kumbuka hiyo idadi haikujumuisha idadi ya wanawake na watoto. Unakumbuka wayahudi walitaka kumkamata Yesu ili awe mfalme wao? Mfalme gani huwa yupo kwenye kundi la watu maskini?

Inaonekana umekosa hata ile elementary knowledge of theology.
 
Laana ni nini?

Kiongozi wa kisiasa akiwaambia watu umasikini ni laana, anaweza kuwafanya waamini kwamba sababu ya umasikini wao haitokani na wao wenyewe kutofanya juhudi, inatokana na laana.

Hili ni wazo linaloweza kuwafanya watu wasitafute suluhisho sahihi la kumaliza umasikini wao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bams,


Ni kweli mimi siyo Mwanatheolijia, lkn mbona kama unanichanganya? Upande mmoja unaongelea utajiri wa rohoni hapo hapo unasema alikuwa tajiri wa mali na kulisha watu 5000, sasa kipi ni kipi? Au alikuwa vyote tajiri wa roho na mali? Na kama alikuwa na Mali Yesu aliitoa wapi?
 
Uongo Yusuf alikuwa na passport alikuwa Mtu international herode alipotaka kuua mtoto Yusuf selemala tajiri aliondoka na familia kuishi nje ya nchi misri akakaa miaka .Angekuwa lofa asingekuwa na Hui uwezo


Unaongelea miaka > 2000 iliyopita unalitambua hilo lakini?
 
Unaongelea miaka > 2000 iliyopita unalitambua hilo lakini?
Nchi zaxwenzetu toka zamani kuingia ilikuwa kwa visa .Lazima mtawala wa eneo akukubali.walikuwa hadi na mafuta ya taaa kumbuka mfano wa wanawali kumi pia wakikuwa na mghorofa enzi zacYesu na walivaa nguo sio magome ya miti. Na walikuwa na fedha zao Kama shekeli nk
 
Sisi wasukuma tuna amini ng'ombe ni utajiri magari, na makorokoro mengine hayana maana kwetu kama hauna ng'ombe

Sent using Jamii Forums mobile app


Ni sawa kwa kuwa ndio kipimo chenu cha utajiri na hivyo mwenye n’gombe wengi ndo tajiri lkn huko alikozaliwa Yesu utajiri haukupimwa hivyo.
 
Sasa huko tunakoenda siko
Kutumia jina la Mungu na Yesu kwa kauli za kisiasa ni ujinga na upumbavu
Mungu anaposema
" Usilitaje Jina la Mungu bure" maana hatamhesabia mtu kuwa hana hatia kwa kulitaja bure. Ndio kama hii. Kauli za wana siasa ni puuzi na uongo kuliko maelezo. Kauli kama hizi na zilizopita mf
1. Haki sawa kwa wote
2. Uchumi wa kati 2020
3. Maisha bora kwa kila mTz
4. Kujaza watu Mapesa
5. Utajirisho
6. Utawala wa sheria
Na zingine ni kwa wajinga tu ndio husikiliza. Sera hizo slogan. Ukitaka uwe tajiri FANYAKAZI, FANYAKAZI
Serkali haikupi hela inajenga miundo mbinu basi hela tafuta mwenyewe, tena kauli hii kama Cdm wataitumia 2020 watabata kura below 10% kwa mtu mwenye elimu yake haiingii kwa vijijin Magu wanamkubali japo hawana hela

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asilimia kubwa ya watanzania hali zao za kimaisha siyo nzuri na kwa ujumla ni masikini.

Wapo wachache tu ambao walikuwa wamejaaliwa kimaisha kama wazazi wa Mbowe ambao vizazi vyao ndivyo vinaendelea kuwa na maisha yenye afadhali kwa sababu ya vile walivyorithi na wachache wametafuta kwa jasho lao wenyewe.

Katika hali ya kuwasononesha masikini wa Tanzania leo katika mkutano wa Chadema unaoendelea Mwenyekiti wao Mbowe amesema umasikini wa Watanzania ni laana.

Mbowe tunakuuliza sisi masikini wa Tanzania tumepewa laana na nani? Na Mwenyezi Mungu muumba? Unataka ukabidhiwe nchi ili uongoze wengi waliolaaniwa.

Je ndiyo maana mlitukimbia katika uchaguzi wa serikali za mitaa ambapo huko ndipo kuna masikini wengi ili tusiwaambukize laana zetu?

CHADEMA JARIBUNI KUCHUJA KAULI ZENU ILI MREHEMEWE.
 
Back
Top Bottom