Eti wanachama wanahoji kwanini chama kimeenda kutumia mamilioni ya fedha kukodi ukumbi wa Mliman City na kuacha kumbi nyingine za bei nafuu halafu Mbowe anajibu kwamba CHADEMA ni watu wa viwango na wanachukia umasikini halafu watu wanashangilia.
Iko wapi tofauti kati ya Magufuli anayenunua ndege na Mbowe anayepeleka Kamati kuu pale Mlimani City kwenye ukumbi wa mamilioni?
Ndege zinaponunuliwa watu wanahoji kwamba zina faida gani kwa mwananchi wa hali ya chini ambaye hana uwezo wa kupanda ndege?
Sasa na mimi nataka kuhoji kwamba kufanyia Mkutano pale Mlimani City kwenye Ukumbi wa mamilioni kuna faida gani kwa mwana CHADEMA wa kawaida au kiongozi wa CHADEMA kwenye ngazi ya shina au tawi ambaye siyo Mjumbe wa kamati kuu? Hivi haya mamilioni si yangeweza kuwajengea ofisi ya Chama hawa viongozi wa mashina na Matawi katika kata zao? Hivi hayo mamilioni yangeweza kujenga ofisi ngapi za Wilaya au Mkoa?
Yaani kweli chama kisicho na ofisi kinaenda kukodi ukumbi wa Million 130 wakati hakina hata jengo moja la ofisi? Yaani chama kinakodi ndege ya kuwapeleka kina Lema CCM Kirumba kwenye sherehe za Uhuru wakati chama hicho hicho hakina hata jengo moja la ofisi halafu wanachama wanashangilia tu kama Majuha?
Kweli nimeamini CHADEMA kuna wajinga na Malofa.
Sent using
Jamii Forums mobile app