Mbowe: CHADEMA tunaamini kwamba umaskini ni laana na kila mwanachadema ni tajiri rohoni mwake

Mbowe: CHADEMA tunaamini kwamba umaskini ni laana na kila mwanachadema ni tajiri rohoni mwake

Alizaliwa Holi la ngombe sio kwa sababu pesa walikuwa hawana Bali nyumba ya wageni ilikuwa imejaa .Kasome Biblia Tena sababu ya Yesu kuzaliwa holini haikuwa sababu ya kuwa wazazi wake walikuwa maskini
sijui kama atarudi,akirudi huyu ni mbishi
 
Na ndivyo ninavyoelewa mimi kwamba Yesu hakuwa tajiri Mali kama wengine wanavyodai na kulikuwa na sababu kwa nini aliamua iwe hivyo, kwani yeye ni Mungu angeweza kuamua kuzaliwa popote pale hata juu ta dhahabu lkn aliamua zizini ili wengi wetu tuweze kujihusisha naye kwa kuwa ni kama mmoja wetu.
Mmoja wenu wa Nani ? Yesu sio maskini mwenzio .Nguo alizokuwa akivaa Ni za kitajiri mno kiasi kuwa siku ya kusulubiwa Askari wa kirumi waluomsulubisha baada ya kufa waliamua kugawana.Angekuwa alikuwa maskini mvaa nguo za kimasikini Askari wale wasingezigombania.Nani angeweza gombania nguo za maskini Tena Askari aliyeajiriwa na serikali?

Hata kuzikwa Yesu alizikwa na matajiri sio maskini.Yusuf wa Arimataya tajiri wa yerusalem ndie alichukua maiti ya Yesu kwenda kumzika kaburi la kitajiri

Yesu alizaliwa eneo lahotelini hakuzaliwa wodini au nyumbani.Nyumba ya wageni ilikuwa imejaa full sababu umati ulikuwa umejaa pale kutoka sehemu mbalimbali kwenda kuhesabiwa .

Maskini gani huzaliwa hotelini?

Hata kabla ya kufa alimwaga zinga la karamu inaitwa karamu ya mwisho haukuwa mlo wa kawaida Ni karamu ya nguvu Yaani farewell party ya uhakika karamu sio chakula Cha maskini
 
YEHODAYA,

Lkn Yesu kabla ya kuteswa na kufa ambapo alijua aliwaambia wafuasi wake kwamba wamtunze na kumhudumia mama yake, sasa kwa nini wamtunze kama alizaliwa na aliacha utajiri, isitoshe Luka 9:58 inasema ,, Yesu akasema, Mbweha wana Mapango, na ndege wana viota, lakini mwana wa mtu hana mahali pa kupumzika” alimaanisha nini? Kwa nini alisema hivyo kama alikuwa ni tajiri?
 
Luka 9:58 inasema ,, Yesu akasema, Mbweha wana Mapango, na ndege wana viota, lakini mwana wa mtu hana mahali pa kupumzika” alimaanisha nini? Kwa nini alisema hivyo kama alikuwa ni tajiri?
Kasome kitabu Cha ufunuo uone mbinguni kwake kulivyo Kuna majumba ya dhahabu nk ndiko Yesu alitokea.Kabla ya kuja Duniani.

Alipofika hapa Duniani akaona hakuna hata nyumba moja ya hadhi yake ndio akasema hana haoni zote takataka tu

Ni sawa na bilionea namba moja Duniani Billy gates aje kijijini kwenu Sidhani Kama ataiona nyumba ya hadhi yake ya kulaza kichwa chake na kupumzika
 
YEHODAYA,


Nimeuliza jinsi ulivyoelewa hiyo Luka 9:58, Yesu alimaanisha nini? Isitoshe kufananisha Mbinguni na Duniani kwa maoni yangu siyo sahihi kwani sidhani kama Mbinguni kuna hali kama hii ya Duniani na kwamba kipimo cha utajiri wa Mbinguni ni sawa na kipimo tunachotumia hapa Duniani, nafikiri utajiri unaoongelewa wa Mbinguni ni mwingine kabisa na hauhusiani na Mahekalu na dhahabu za Duniani isitoshe Yesu ni Mungu hivyo kila kitu ni mali yake Mbingu na Ulimwengu wote hivyo sidhani kama ni sawa kupima utajiri wake sawa na binadamu tunavyopima kwamba dhahabu na hekalu kwani hivyo vyote kwake siyo kitu, kulinganisha na uwezo wake wa kuumba.
 
Bams,
Tuna tofautiana na wewe kwenye masuala kadhaa ya kisiasa lakini ulichoandika leo ni mahubiri ya jumapili yaliyokamilika.

Mwambie mhudumu akiongezee kinywaji nakuja kulipa nikimaliza kuongea na simu. God bless whatever you are doing right now in your life 👍👍.
 
Mbowe alipata 0 shuleni ndio maana anaongea vitu vya kuota ,wangekuwa matajiri wa roho wasingejiuza kwa bei ndogo

Mbowe tajiri akaiuza chadema kwa lowasa

USSR

Sent using Jamii Forums mobile app

Mbona unajichumia dhambi ya kujitakia kabisa ndugu yangu?

Be honest rafiki yangu; Una uhakika na hiki ulichokiandika?

Mimi nakukatalia kwa 100% juu ya uhusiano wa umasikini na Roho/nafsi ya mtu.....

Kama hujui, ni kuwa, matendo yako yote yanayithibitika kwa macho ya mwili wa mtu, kwanza yanaanzia ndani ya nafsi/moyo/roho ya mtu huyo....

Kila yanayokupata ni matokeo ya jinsi ulivyo ndani....

Wasimamizi na watunga sera zetu za kiuchumi na kijamii ni CCM na ndiyo wanaoongoza serikali....

Huwezi kutenganisha kila hali ilivyo leo ktk nchi yetu bila kuihusisha na CCM...

Kama ni umasikini wa Watanzania, huwezi kuutenga na Sera na mipango ya maendeleo ya CCM maana ndiyo wenye dhamana ya uongozi wa nchi hii tangu mwaka 1961...!!

Kwa hiyo Freeman A. Mbowe ni kichwa na brighter than your imaginations....

Obviously, wewe ndiye uliyepata Division Zero ktk kusoma kwako....

Arguments zako tu zinathibitisha hili!!

Pole sana....
 
Hoja ya 3 upo sahihi.
..wananchi hawapaswi kujiona WANYONGE.

..wakishajiona wanyonge kisaikolojia watajisalimisha kwa viongozi na kuvumilia uzembe na hata ukatili wa viongozi waliowachagua.

..waTz tuna tatizo la KUOMBA badala ya KUDAI haki na mahitaji yetu toka kwa viongozi.

..chanzo chake ni viongozi kwa muda mrefu kuwaita wanancho wanyonge mpaka imefika mahali sasa wananchi wanaamini wao ni wanyonge na wanastahili huruma.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Alizaliwa Holi la ngombe sio kwa sababu pesa walikuwa hawana Bali nyumba ya wageni ilikuwa imejaa .Kasome Biblia Tena sababu ya Yesu kuzaliwa holini haikuwa sababu ya kuwa wazazi wake walikuwa maskini
"Wazazi" wa Yesu ni kina nani kwa mujibu wa Biblia?
 
Omulasil,
Kuna wakati uwa najiuliza "hivi inawezekanaje taasisi za dini zilizo kubwa zenye utajiri wa kutosha zinashindwa kusaidia waymini wao huduma za jamii bure"?

Mfano elimu bure,kuwajengea makazi bure,afya bure na hata mikopo yenye unafuu.
Kwa haraka haraka wananchi wanahitaji unafuu wa maisha na faraja ya kuishi.
Kama umaskini ni laana vipi wale wanaopata ridhiki zao kupitia viongozi maskini,je wanagawana?
 
Ukikiangalia kwa makini kisa cha viongozi wa Daruso waliosimamishwa masomo utagundua kuwa chanzo chake ni umaskini.

Kwamba viongozi hawa maskini walikuwa wanawatetea wanafunzi wenzao maskini waliowaweka madarakani ili wapewe mikopo yao iliyo halali kwa mujibu wa sheria kwa wakati.

Rais Magufuli alishasema fedha za wanafunzi mabilioni ya shilingi zimeshapelekwa Bodi ya Mikopo ili wanafunzi wapewe kwa wakati na kuwaacha wajikite na shughuli za masomo tu.

Inawezekana pale Bodi ya Mikopo au UDSM kuna maskini ambao wamezitamani hizo fedha na hivyo kuwacheleweshea Maskini wenzao ambao ni wanafunzi.

Anatokea waziri wa serikali inayowajali wanyonge na maskini wakiwemo anawasimamisha viongozi wa Daruso ambao ni maskini lakini wameshapata mikopo yao ila wana kiherehere cha kuwatetea maskini wenzao ambao ni wanafunzi.

Kiukweli hapa nimeuona zaidi umaskini wa roho kwani fedha za wanafunzi tayari zipo. Kwanini hawapewi?

Nimejikuta tu natafakari. Hivi laana ni nini?

Kwenye Biblia tunaelezwa laana ilileta ukoma, yaani inalaaniwa roho unadhurika mwili tena ngozi.

Maendeleo hayana vyama!
 
Kuna wakati uwa najiuliza "hivi inawezekanaje taasisi za dini zilizo kubwa zenye utajiri wa kutosha zinashindwa kusaidia waymini wao huduma za jamii bure"?
Mfano elimu bure,kuwajengea makazi bure,afya bure na hata mikopo yenye unafuu.
Zitakufa hakuna binadamu asiyependa dezo.Ukitangaza chochote dezo dini yako itafurika watu kuliko umati wa Mohamed au Yesu kila mmoja akijinadi kuwa mfuasi mwaminifu kwako aliye tayari hata kufa kwa ajili yako kumbe mwongo anafuata dezo!!! Hata Yesu aliwafokea wafuata dezo akasema ninyi mnanifuata tu kwa kufuata chakula ninachowapa hamna lolote nyie.

Ukitaka dini yako ujaze matapeli tangaza dezo ya hivyo ulivyosema kafungue dini yako hata Leo uone utakavyojaza
 
Au pesa zimechukuliwa kaenda kulipwa yule mkulima wa South. Tumegomboa ndege yetu kwa pesa za mikopo ya wanafunzi.
 
..Mwalimu NYERERE alisema Tz ina MAADUI watatu ambao wanapaswa kupigwa VITA, na moja ya maadui hao ni UMASIKINI.

..Katika suala hili Mzee Mbowe anafuata wasia aliotuachia Baba wa Taifa kwamba tukatae na tuupige vita umasikini.
 
Back
Top Bottom