Mbowe: CHADEMA tunaamini kwamba umaskini ni laana na kila mwanachadema ni tajiri rohoni mwake

Mbowe: CHADEMA tunaamini kwamba umaskini ni laana na kila mwanachadema ni tajiri rohoni mwake

Kukusaidia tu Yesu alilisha maelfu bure .Lofa hawezi kulisha watu maelfu Kama Yesu alivyofanya.Anayekuambia Yesu alikuwa maskini mwongo mkubwa
Yesu alijinyenyekeza kwa jamii ili upendo alioufundisha uweze kueleweka vyema.

Hakuwa na sababu ya kuishi kitajiri kwani ujumbe wake ni wa kila mtu. He was humble.
 
Matajiri gani wakati ndo chama pekee kinacholialia wanachama wake kuchuuzwa kama maparachichi?
 
Mleta mada una hoja ya msingi, lakini ukumbuke hao unaowauliza hayo ,wanaulizwa swali moja tu, "kwa nini hawajengi angalau ofisi moja tu ya makao makuu tokea miaka ya 2000 had I sasa" na swali hilo halijawahi kuwa na jibu, kwa nini udhani wanastahili kuulizwa maswali zaidi yeye muelekeo huo huo? Huoni no kuwatwishwa mzigo wasiostahili?

Je ukijenga halafu ukazuiwa kutumia utafanyaje?Kama bendera tu wanaambiwa shusheni, ofisi pia si wataambiwa fungeni?Kwa hiyo ya kukodisha ukifungiwa unahamia sehemu nyingine


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Ni kweli mimi siyo Mwanatheolijia, lkn mbona kama unanichanganya? Upande mmoja unaongelea utajiri wa rohoni hapo hapo unasema alikuwa tajiri wa mali na kulisha watu 5000, sasa kipi ni kipi? Au alikuwa vyote tajiri wa roho na mali? Na kama alikuwa na Mali Yesu aliitoa wapi?
Utajiri wa mwili huanzia katika roho, fikra na mamlaka. Yesu hakuwa na haja ya kutembea na utajiri wa mwili ili aonekane ni tajiri. Utajiri wake ulikuwa katika mamlaka yake ya Kimungu.

Shetani aliutazama mwili wa Yesu, akaamini ni maskini, akadhani anaweza kumhadaa kwa kutumia umaskini wa mwili ulioonekana wazi.

Yesu alipooneshwa na shetani utajiri ambao angeupata kama angemsujudia aliuona ni takataka akilinganisha na utajiri wake uliopo katika roho na mamlaka yake. Mamlaka yake yalimwezesha kupata chochote, wakati wowote na mahali popote.

Leo Magufuli anaweza kula michembe, akasafiria baiskeli, asiyemjua atamwona ni maskini, anaweza hata kujaribu kumhadaa kwa kumpa sahani ya wali, lakini nina imani itaitupilia mbali maana yeye ni tajiri wa mamlaka. Ana uwezo wa kuitisha V8 wakati wowote na akaletewa chakula kizuri akipendacho.

Yesu alizaliwa katika mazingira duni siyo kwa sababu alikuwa maskini maana Baba yake wa mbinguni anamiliki kila kilichopo. Yesu aliye tajiri na mfalme alizaliwa katika uduni ili awafikie walio duni, nao waamini wanaweza kushiriki utajiri wa Mungu wakimfuata yeye aliye tajiri katika vyote, anayeweza kuwabariki kwa utajiri wa roho na mwili.
 
senzighe, Kwa hiyo kwa akili yako, umaskini ni baraka? Hata tuendapo makanisani au misikitini, tunaambiwa, 'mliobarikiwa kuwa na mali, mrudishieni Mungu sehumu ya mali zenu'.

Ni hakika umaskini ni laana lakini haimaanishi maskini amelaanika maana maskini wa leo anaweza kuwa tajiri wa kesho. Ugonjwa ni mbaya, lakini mtu mgonjwa siyo mbaya, ni wa kuonewa huruma, ni wa kusaidiwa.

Tatizo la watanzania wengi wanatumia ujinga kuielekeza hoja katika uovu wao badala ya kuutafuta werevu ili kuielewa hoja.
 
Inashangaza mnapenda majengo mazuri mazuri ndo maana mnafanyia mkutano wenu Mlimani City,ila makao makuu yenu sasa hata nyumba ya bibi yangu kule somanda ni nzuri na ina hadhi kuliko makao makuu yenu.Kweli hiki chama ni saccos,mnapenda vizuri ila jengo la chama libaya.Nyumba zenu za kuishi nzuriiiiiiiiiii.
 
Alizaliwa Holi la ngombe sio kwa sababu pesa walikuwa hawana Bali nyumba ya wageni ilikuwa imejaa .Kasome Biblia Tena sababu ya Yesu kuzaliwa holini haikuwa sababu ya kuwa wazazi wake walikuwa maskini
Mkuu huko sahihi. (Luka 2:7 akamzaa mwanawe,kifungua mimba,akamvika nguo za kitoto,akamlaza katika hori ya kulia ng'ombe,kwa sababu hawakupata nafasi katika nyumba ya wageni.)
 
USSR,
.Weka ushahidi, lakini kama huwa basi utakuwa hauna tofauti na mwanamke m'mbeya tu
 
Bams,
Na ndivyo ninavyoelewa mimi kwamba Yesu hakuwa tajiri Mali kama wengine wanavyodai na kulikuwa na sababu kwa nini aliamua iwe hivyo, kwani yeye ni Mungu angeweza kuamua kuzaliwa popote pale hata juu ta dhahabu lkn aliamua zizini ili wengi wetu tuweze kujihusisha naye kwa kuwa ni kama mmoja wetu.
 
Back
Top Bottom