Mbowe: CHADEMA tunaamini kwamba umaskini ni laana na kila mwanachadema ni tajiri rohoni mwake

Mbowe: CHADEMA tunaamini kwamba umaskini ni laana na kila mwanachadema ni tajiri rohoni mwake

Tuwekee hapa hilo andiko!
Nimepigia rangi ya blue

USSR
Screenshot_20191218-083754.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yesu hakuwa maskini. Alikuwa tajiri moyoni mwake ndiyo maana alimdharau hata shetani aliyetaka ampe utajiri alimradi tu amsujudie. Kwa nini alikataa? Kwa sababu kile ambacho shetani alitaka kumpa kilikuwa ni kidogo sana ukilinganisha na utajiri aliokuwa nao.

Inaonekana umekosa hata ile elementary knowledge of theology.
Unajua msione watu tunakimbilia kwa akina mwamposya na mitume na manabii kuwaacha nyie na mdigrii yenu Koko ya theolojia vichwani mko weupe

Familia ya Yusuf walikuwa ukoo wa kifalne ukoo wa Daudi Mfalme kasome mathayo sura ya kwanza kuhusu ukoo wa Yesu na hakuna ukoo wa kifalme uliokuwa maskini hata Koo zetu za machifu wetu wa kiafrika Koo zao hazikuwa maskini.Kusema Yesu alikuwa maskini kwanza Ni kufuru.yesu Ni Mungu na Kama ni Mungu hajawahi kuwa maskini na hatarajii kuwa maskini.Mungu sio maskini

Pili Shetani kila analoongea Ni la uongo .Yesu alitamka wazi kuwa shetani ni baba wa uongo Wala kweli haimo ndani yake
Hivyo Shetani alipomwambia Yesu kuwa nisujudie nitakupa vyote vijazavyo dunia Yesu alimimua sababu vyote vijazavyo.ulimwengu Ni Mali ya Mungu sio ya Shetani.Shetani hana kitu kabisa.Ndio maana Yesu akamjibu kuwa Kama mtu anataka kupata vyote amsujudie Mungu tu mwenye vyote

Kwa hiyo wewe na hiyo theolojia koko unaamini Shetani alikuwa na kitu Cha kumgawia Yesu ambaye Ni Mungu ? Hizo elimu zenu za kijinga za theoljia kaeni nazo wenyewe mdaganyane huko huko mnakosomea waumini tulishawashtukia mnatulisha matango pori
 
Kuna maskini anaweza kuwalisha wanaume zaidi ya 5,000; wakala na kushiba? Kumbuka hiyo idadi haikujumuisha idadi ya wanawake na watoto. Unakumbuka wayahudi walitaka kumkamata Yesu ili awe mfalme wao?

Mfalme gani huwa yupo kwenye kundi la watu maskini?

Inaonekana umekosa hata ile elementary knowledge of theology.
Eee hizo theojia koko mnzosoma zinatisha.Kwa hiyo kila tajiri lazima awe Mfalme?
Kwa hiyo Mfano Tajiri Reginald Mengi alipokukuwa kwenye kundi la watu maskini viwete,vilema ,vipofu nk hakuwa tajiri alikuwa maskini? Reginald Mengi alikuwa tajiri katikati ya maskini kwa kengo la kuwasaidia maskini

Na Yesu alikuwa Tajiri mkubwa alikaa katikati ya maskini kuwasaidia kwa kuwaponya magonjwa yao kuwalisha ,kuwasaidia kiuchumi mtano Petro alihangaika kuvua hakupata kitu akaenda kwa Yesu akamsaidia kumnyanyua uchumi wake kimiujiza kwa kumpa utajiri wa ghafla kwani alivua samaki wengi ajabu.

Argument zako zinanifanya nizidi kuidharau elimu ya theolojia
 
Natafuta kujua tuna jiaandaaje kuwa matajiri kama hatuwekezi kwebye vitu.

Kweli Div 0 inaobekana kweupeeeee..

Kwakauli hii lazina kuwe na tabaka la walionacho na wasio nacho. Mwisho wa siku lazima matajiri watawachukia maskini na kuona wana wanyonya.
"MUDA UTAONGEA"

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Eti wanachama wanahoji kwanini chama kimeenda kutumia mamilioni ya fedha kukodi ukumbi wa Mliman City na kuacha kumbi nyingine za bei nafuu halafu Mbowe anajibu kwamba CHADEMA ni watu wa viwango na wanachukia umasikini halafu watu wanashangilia.

Iko wapi tofauti kati ya Magufuli anayenunua ndege na Mbowe anayepeleka Kamati kuu pale Mlimani City kwenye ukumbi wa mamilioni?

Ndege zinaponunuliwa watu wanahoji kwamba zina faida gani kwa mwananchi wa hali ya chini ambaye hana uwezo wa kupanda ndege?

Sasa na mimi nataka kuhoji kwamba kufanyia Mkutano pale Mlimani City kwenye Ukumbi wa mamilioni kuna faida gani kwa mwana CHADEMA wa kawaida au kiongozi wa CHADEMA kwenye ngazi ya shina au tawi ambaye siyo Mjumbe wa kamati kuu? Hivi haya mamilioni si yangeweza kuwajengea ofisi ya Chama hawa viongozi wa mashina na Matawi katika kata zao? Hivi hayo mamilioni yangeweza kujenga ofisi ngapi za Wilaya au Mkoa?

Yaani kweli chama kisicho na ofisi kinaenda kukodi ukumbi wa Million 130 wakati hakina hata jengo moja la ofisi? Yaani chama kinakodi ndege ya kuwapeleka kina Lema CCM Kirumba kwenye sherehe za Uhuru wakati chama hicho hicho hakina hata jengo moja la ofisi halafu wanachama wanashangilia tu kama Majuha?

Kweli nimeamini CHADEMA kuna wajinga na Malofa.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siyo kweli, Yesu alizaliwa kwenye hali Duni kwa sababu maalumu, na ndo maisha yake yote aliishi kama mtu wa kawaida na maisha Duni asiyependa makuu, aliishi na masikini, yule ni Mungu iweje ashindwe kutatua tatizo dogo kama hilo la kukosa nafasi kama alitaka kuzaliwa kwenye Hekalu kama Mfalme?
Kila alilofanya lilikuwa na kusudio fulani.
 
Mleta mada una hoja ya msingi, lakini ukumbuke hao unaowauliza hayo ,wanaulizwa swali moja tu, "kwa nini hawajengi angalau ofisi moja tu ya makao makuu tokea miaka ya 2000 had I sasa" na swali hilo halijawahi kuwa na jibu, kwa nini udhani wanastahili kuulizwa maswali zaidi yeye muelekeo huo huo? Huoni no kuwatwishwa mzigo wasiostahili?
 
Yani kabisa unaugua vidonda vya tumbo kwa CHADEMA kufanyia Mkutano Mlimani City..!!!
Hahahahahahahaha
 
Mkuu..awamu hii imetuletea wehu wa kila aina..
CHADEMA kufanyia Mkutano pale Mlimani City kuna watu wamepata ulcers kama huyu mbwiga mleta uzi.
umeoana eh! Yaani mbwiga huyu sijui katokea wapi! Wao ndege imewaleta bure wajumbe wao, hilo hawalioni. yanashupalia vitu vidogo!
 
Etwege,
kwa ID yako lazima utakuwa ni mburula wa kiwango cha parmanent head damage; lakini ukikua utaelewa tofauti baina ya hayo unayoyaongelea!
 
DJ izo ndizo sehemu anapo wapigia Nyumbu, baadae anawaambia Chama kilikua hakina fedha nikatoa pesa zangu za mfukoni. Ndiomaana hakuna mwaka utapita bila Chadema kudaiwa ba DJ. Kwa mkutano kama uo ana uhakika wa kula ruzuku ya kutosha kwa kisingizio cha matumizi ya mkutano.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom